Je, ni kweli kuwa kuna wizi katika malipo ya luku?

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Ngd. wana JF, nimekuwa nikisikia kuwa malipo ya LUKU yanabadirika badirika kila mara. Nimefanya ufatiliaji na kugundua ni kweli. Kuna siku unaweza kupewa units nyingi na wakati mwingine ukapewa pungufu tu.

Nilipoulizia Tanesco kwa njia ya simu nikaambiwa inatakiwa ndani ya mwezi ununue mara moja kwa maana kwamba ukinunua mwisho wa mwezi inaongezeka! Sikujua kigezo kinachotumika.

Mnisaidie kuhusu hili suala. KUNA wizi jamani???
 
Hata mimi hii ishu ilikua inanichanganya sana hapo zamani
mpaka siku moja niliamua kumvaa mhudumu na ilikua kasheshe kubwa sana mpaka jamaa wengine kwenye mstari wakaingilia.

Ilikua ishu kama ya kwako, nilinunua umeme na ukawa na units ndogo sana kulinganisha na nilionunua awali ambapo nilikua nimeenda
na receipt yake. Kiasi cha fedha kile kile ila units tofauti, jamaa alijitahidi kunielewesha japokuwa kwa wakati huo sikumuelewa na nilikua
na jazba sana ila baadae baada ya kutulia nikaona ina make sense. Ni hivi...

Huwa kuna wanaita service charge ambayo inafanyika mara moja kwa mwezi. Hii service charge wakata kwenye malipo yako ya luku utakayofanya mara ya kwanza ukienda kununua umeme mwezi mpya ukianza. Hivyo basi kwa mfano kama utanunua umeme wa Tsh 15,000 utapatiwa units za umeme wa Tsh 10,000 na ile Tsh 5000 itakuwa ni service charge. Kama utaenda wakati mwingine wowote
katika mwezi huo huo kununua umeme tena wa mfano wa Tsh 15,000 utapatiwa units za sawa na Tsh 15,000 kama kawaida na hakuta
kuwa na malipo ya ziada.

So niliona tatizo kubwa la hawa jamaa wa Tanesco ni utoaji wa taarifa kwa wateja na kuwaelimisha mambo
yanakwendaje lakini unaweza kuta wahusika na huduma kwa wateja wanakaa kimya tu ili kutumia nafasi hii kujinufaisha wao binafsi kwa kufanya makato kichini chini.

Hope nimekusaidia kidogo mkuu
 
Ninavyofahamu mimi ni kwamba, kuna monthly charges, kwa hiyo mara ya kwanza unaponunua ndani ya mwezi unakatwa monthly charges na hivyo kupelekea umeme unaoupata kuwa mdogo.

Ila LUKU nyingine utakazonunua baada ya hapo zitakuwa poa, mpaka mwezi uishe tena.
 
Kila mwezi unapewa unit 50 ambazo unazinunua kwa bei ndogo. Zinazozidi baada ya unit 50 unanunua kwa bei ya juu kidogo.
 
Back
Top Bottom