Je, ni kweli kuuza kitu/vitu au mali yako ili utatue shida ni laana?

Umomi

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
677
983
Hanari Wanajamvi la JamiiForums,

Katika maisha kuna changamoto nyingi sana. Kawaida kila mtu huwa anazitatua changamoto kwa namna yake. Kuna baadhi ya watu wanasema "ulichonacho ndiyo msaada wako" huu ni msemo nimekuwa nikiusikia toka nipo utotoni.

Pia katika maisha huwa wengi wetu tunaanza kumiliki vyombo vya ndani kwanza Kama kitanda godoro, tv n.k lakini shida nazo huwa hazishi kabsa.

Sasa eti nasikia kuuza vyombo vya ndani, mifugo au hata kiwanja kutatua shida yako ni laana?

Naomba kuwasilisha
 
Vyombo vya ndani sawa, lakini mifugo ndiyo yenyewe mkuu watu wamesoma kwa kuuza mifugo kuku, mbuzi, bata, mpaka gongo halafu wewe unasema laana?
 
Na Mimi nilitaka kudhibisha kuwa kuuza vitu vya ndani ni laana hata Kama unahama mkoa kwenda mkoa? Na Ni kwanini iwe laana?
 
Laana ya nini sasa! Kitu ununue mwenyewe, halafu ukaamua mwenyewe kukiuza! Sasa kwa nini upate hiyo laana! Yaani hata kama hicho kitu umekichoka, hutakiwi kukiuza kwa imani potofu za kupata laana!
Mkuu naomba niwe muwazi mfano umeenda kuweka kambi sehemu labda kwa muda wa mwaka mzima, bahati nzuri Mungu kakujalia ukapata labda ukanunua kitu Kama tv n.k ila ghafula ukiuza Ni laana?
 
Binafsi niliambiwa usipende kuuza vitu unavyomiliki kama hakuna uhitaji wa kufanya hivyo, mfano kama umenunua simu mpya nguo mpya au TV mpya wapatie watu wako wa karibu wanao kuzunguka kama vile wadogo zako kaka zako usipende kuuza vitu unavyomiliki tabia hiyo sio nzuri.
 
Na Mimi nilitaka kudhibisha kuwa kuuza vitu vya ndani n laana hata Kama unahama mkoa kwenda mkoa? Na Ni kwanini iwe laana?
Lakini inategemea, kuna vitu vingine huwezi beba eti kisa laana hakuna kitu kama hicho lakini vipo vitu ambavyo kweli lazima ujiulize, mfano bila sababu unaanza kuuza vitu vya ndani!
 
Binafsi niliambiwa usipende kuuza vitu unavyomiliki kama hakuna uhitaji wa kufanya hivyo, mfano kama umenunua simu mpya nguo mpya au TV mpya wapatie watu wako wa karibu wanao kuzunguka kama vile wadogo zako kaka zako usipende kuuza vitu unavyomiliki tabia hiyo sio nzuri.

Mi binafsi siamini kama kuna laana yoyote kwa mtu kuuza vitu vyako unavyomiliki kihalali. Hii nafikiri ni mila tu ya kiafrika ya kupenda kulimbikiza mavitu ndani hata kama huyatumii na huna mpango wa kuja kuyatumia tena.

Kuna watu majumbani kwao utakuta mtu ana makochi ya zamaniiiii kayaweka stoo, magodoro yamewekwa juu ya kabati, tv ya chogo ipo stoo, magari mabovu juu ya mawe.. nguo, viatu, mablangeti, mashuka, mapazia... sasa yote hayo ya nini? Uza nunua mapya au kula hiyo hela punguza makorokoro nyumbani kwako..!
 
Acha kabisaaaaa.
Niliokolewa na zawadi za kitchen party.
La sivyo sidhani kama ningenunua
Daa jamani, mimi sipendi kuuza kabisa vitu vya nyumbani, labda ni nunue kingine napo hupenda kumpa tu ndugu yangu lakini si kuuza
 
  • Thanks
Reactions: amu
Mi binafsi siamini kama kuna laana yoyote kwa mtu kuuza vitu vyako unavyomiliki kihalali. Hii nafikiri ni mila tu ya kiafrika ya kupenda kulimbikiza mavitu ndani hata kama huyatumii na huna mpango wa kuja kuyatumia tena.

Kuna watu majumbani kwao utakuta mtu ana makochi ya zamaniiiii kayaweka stoo, magodoro yamewekwa juu ya kabati, tv ya chogo ipo stoo, magari mabovu juu ya mawe.. nguo, viatu, mablangeti, mashuka, mapazia... sasa yote hayo ya nini? Uza nunua mapya au kula hiyo hela punguza makorokoro nyumbani kwako..!
Mimi nikipata kipya nagawa, TV chogo niligawa, sijui frig nimepata kubwa natoa, nguo nazo tena nawambia kama hamwezi kuvaa tuchome Moto mie nimechoka kuziona
 
Mkuu naomba niwe muwazi mfano umeenda kuweka kambi sehemu labda kwa muda wa mwaka mzima, bahati nzuri Mungu kakujalia ukapata labda ukanunua kitu Kama tv n.k ila ghafula ukiuza Ni laana?
Hamna kitu kama hicho laana ya wapi, wewe mfano unakitanda choka mbaya, umehamia mkoani ubebe cha nini wakati huko mbao original!
 
Mi binafsi siamini kama kuna laana yoyote kwa mtu kuuza vitu vyako unavyomiliki kihalali. Hii nafikiri ni mila tu ya kiafrika ya kupenda kulimbikiza mavitu ndani hata kama huyatumii na huna mpango wa kuja kuyatumia tena.

Kuna watu majumbani kwao utakuta mtu ana makochi ya zamaniiiii kayaweka stoo, magodoro yamewekwa juu ya kabati, tv ya chogo ipo stoo, magari mabovu juu ya mawe.. nguo, viatu, mablangeti, mashuka, mapazia... sasa yote hayo ya nini? Uza nunua mapya au kula hiyo hela punguza makorokoro nyumbani kwako..!
Heri kioze kuliko kumpa ndugu hiyo ni laana mbaya.

Umepata kingine kitoe cha zamani hata kwa bei poa, shukrani yake ni kubwa sana.

Kimfaacho mtu ni mali yake, hapo unajiichia hata aibu yako kuliko kuwa ombaomba, utasemwa hovyo.

Kibaya na cha laana ni kuuza vitu vidogovidogo vya urithi pasi na lazima.
 
Back
Top Bottom