Je, ni kweli kungekuwa na mgogoro wa Kikatiba kama Mahakama ingekubaliana na maombi ya Lissu?

Munjombe

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
1,937
2,632
Tuangaze macho yetu kwenye ibara ya 83 (1) a&b ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeweka wazi shauri linalo weza funguliwa Mahakama Kuu juu ya uamuzi wa kama mtu ni mbunge au la?Katiba imegawanya mashauri katika aina mbili ambazo ni kama ifuatavyo

1. Moja juu ya hoja kama uteuzi wa mtu kuwa mbunge ulikuwa halali au si halali 83(1)(a)
2. Kuhoji kama kiti cha mbunge ki wazi au la (83) (1)(b).

Sasa niende kwenye scenario na maoni yangu juu ya uamuzi wa jaji kuyakataa maombi kwa sababu alizo toa hususani kuamua kuwa kuyakubali maombi ya lissu ni kuleta mgogoro wa kikatiba.

SPIKA NDUGAI alitangaza kuwa kiti cha Mbunge(Tundu Lissu) kiwazi, na tume hapo hapo ikatisha uchuguzi ambao kimsingi chadema hawakushiriki na hivyo in my opinion hawangeweza kuwa na uhalali wa kupinga uchaguzi ambao uliitishwa na tume na wao kutoshiriki(locus standi).

Lakini hoja kuu hapa ni je ni kweli kiti cha Mbunge lissu kilikuwa wazi kama alivyosema spika,Je spika ana discrestion power ya kutangaza tu kiti cha mbunge ki waz au kuna utaratibu wa kisheria hadi kufikia huo uamuzi.

Ikiwa ni hoja ilikuwa ni katiba kama alivyosema NDUGAI JAJI alipaswa kujikitia kwenye Ibara 83(1)(b) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Jaji pia anapaswa kuanza na ibara ya 13 yote na husussani ibara ya 13(6) ya katiba ya Tanzania huku akijiuliza kama masharti yaliyowekwa kwenye ibara hiyo yalifuatwa maana kitafsiri katiba haiosomwi kwa kuangalia ibara moja ni lazima uisome kwa pamoja kupata uhalali wa maamuzi kikatiba.

Baada ya kujiuliza maswali kadha ya kiprocedure/hatua za uamuzi jaji pia alipaswa kuijielekeza pia kwenye substantive rights.

Kwa maoni yangu kwa kuwa msingi wa shauri ni katiba na ni juu ya maamuzi yalifanywa na spika kwa mujibu wa sheria kama alivyo dai hivyo Mahakama kuamua kuwa maamuzi kuwa spika alikosea kutangaza kiti cha mbunge kiwazi hayawezi sababisha mgogoro wa kikatiba.(interpretation is mine)
 
Kiukweli Nimemuangalia Jaji wa leo na Wa jumatatu iliyopita. ni watu wawili tofauti kabisa!

Yule wa jumatatu iliyopita, angetoa uamuzi siku hiyo, uamuzi wa Spika ulikuwa unabatilishwa na Lissu angeendelea kutambuliwa kama mbunge halali.

Huyu wa leo, kaja na kigugumizi, hofu na hoja hafifu sana!

Hata hivyo Mahakama ni Majaji, na Majaji ni binadamu kama alivyo Ndungai.
Uamuzi umetoka na ambaye hajaridhika akate rufaa.
 
Tuangaze macho yetu kwenye ibara ya 83 (1) a&b ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeweka wazi shauri linalo weza funguliwa Mahakama Kuu juu ya uamuzi wa kama mtu ni mbunge au la?Katiba imegawanya mashauri katika aina mbili ambazo ni kama ifuatavyo

1. Moja juu ya hoja kama uteuzi wa mtu kuwa mbunge ulikuwa halali au si halali 83(1)(a)
2. Kuhoji kama kiti cha mbunge ki wazi au la (83) (1)(b).

Sasa niende kwenye scenario na maoni yangu juu ya uamuzi wa jaji kuyakataa maombi kwa sababu alizo toa hususani kuamua kuwa kuyakubali maombi ya lissu ni kuleta mgogoro wa kikatiba.

SPIKA NDUGAI alitangaza kuwa kiti cha Mbunge(Tundu Lissu) kiwazi, na tume hapo hapo ikatisha uchuguzi ambao kimsingi chadema hawakushiriki na hivyo in my opinion hawangeweza kuwa na uhalali wa kupinga uchaguzi ambao uliitishwa na tume na wao kutoshiriki(locus standi).

Lakini hoja kuu hapa ni je ni kweli kiti cha Mbunge lissu kilikuwa wazi kama alivyosema spika,Je spika ana discrestion power ya kutangaza tu kiti cha mbunge ki waz au kuna utaratibu wa kisheria hadi kufikia huo uamuzi.

Ikiwa ni hoja ilikuwa ni katiba kama alivyosema NDUGAI JAJI alipaswa kujikitia kwenye Ibara 83(1)(b) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Jaji pia anapaswa kuanza na ibara ya 13 yote na husussani ibara ya 13(6) ya katiba ya Tanzania huku akijiuliza kama masharti yaliyowekwa kwenye ibara hiyo yalifuatwa maana kitafsiri katiba haiosomwi kwa kuangalia ibara moja ni lazima uisome kwa pamoja kupata uhalali wa maamuzi kikatiba.

Baada ya kujiuliza maswali kadha ya kiprocedure/hatua za uamuzi jaji pia alipaswa kuijielekeza pia kwenye substantive rights.

Kwa maoni yangu kwa kuwa msingi wa shauri ni katiba na ni juu ya maamuzi yalifanywa na spika kwa mujibu wa sheria kama alivyo dai hivyo Mahakama kuamua kuwa maamuzi kuwa spika alikosea kutangaza kiti cha mbunge kiwazi hayawezi sababisha mgogoro wa kikatiba.(interpretation is mine)

Mkuu hivyo vifungu vya sheria vina nguvu kuliko utashi wa rais?
 
Spika kwa sababu azijuavyo alimvua Ubunge Nassary na Mahakama ikabariki kwa kile kinachoweza kuitwa technicalities.

Akamvua Mbunge Lisu na leo mahakama imeajichezesha ijuavyo kwa kumruhusu Mtatiru kuapishwa na baadaye kuibuka na hoja kwamba wanaogopa mgongano wa mihimili.

Jambo hili ni jepesi ila ni gumu na zito kwa wanaokiangalia kiti Cha spika kwa jicho la karibu. Wabunge wengine ndani ya Bunge ampo salama kwa sababu wakati wowote na majira msiyodhani Mhe. Spika anaweza kutangaza kukuvua Ubunge uliopewa kwa kura za wananchi na utakapokwenda mahakamani utakutana na majaji ambao kwao haki siyo kipaumbele bali hofu ya mgongano wa mihimili ndiyo kipaumbele. Kwao wananchi siyo kipaumbele bali spika ndio kipaumbele.

Wabunge msishangilie kuchaguliwa na wananchi maana siyo kigezo cha wewe kuendelea kuwa mbunge, fadhila za spika ndizo zitakazokufanya kuwa mbunge.
 
Hoja kuu ni hiyo tu.

Kwa spika au mtu mwingine yeyote kuwa na madaraka ya kuwachagulia au kuondoa mwakilishi waliomchagua wananchi wenyewe.

Hili ni jipya kabisa na ndilo hasa linalotakiwa kujadiliwa kwa kina.

Haya madaraka waliyojitwisha hawa watawala bila ya kujali matakwa ya wananchi.
 
Jamani..,mwacheni Lissu amalizie tiba,mjue bado yupo kwenye uangalizi ma dokta.Hajaruhusiwa kusafiri
 
Wadau naomba kuelimishwa juu ya Mgogoro wa Kikatiba ambao Mh.Jaji Matupa amesema ungetokea.Je ni Mgogoro gani?Nani angekuwa kausababisha kati ya Bunge na Mahakama?
 
Sio kweli.

Kilichotokea ni uhuni wa yule hakimu kushindwa kusimamia vema majukumu yake. Na hii imetokana na hofu aliyonayo dhidi ya watawala.
 
Spika kwa sababu azijuavyo alimvua Ubunge Nassary na Mahakama ikabariki kwa kile kinachoweza kuitwa technicalities.

Akamvua Mbunge Lisu na leo mahakama imeajichezesha ijuavyo kwa kumruhusu Mtatiru kuapishwa na baadaye kuibuka na hoja kwamba wanaogopa mgongano wa mihimili.

Jambo hili ni jepesi ila ni gumu na zito kwa wanaokiangalia kiti Cha spika kwa jicho la karibu. Wabunge wengine ndani ya Bunge ampo salama kwa sababu wakati wowote na majira msiyodhani Mhe. Spika anaweza kutangaza kukuvua Ubunge uliopewa kwa kura za wananchi na utakapokwenda mahakamani utakutana na majaji ambao kwao haki siyo kipaumbele bali hofu ya mgongano wa mihimili ndiyo kipaumbele. Kwao wananchi siyo kipaumbele bali spika ndio kipaumbele.

Wabunge msishangilie kuchaguliwa na wananchi maana siyo kigezo cha wewe kuendelea kuwa mbunge, fadhila za spika ndizo zitakazokufanya kuwa mbunge.
Kama atachaguliwa na wanainchi lakini hakashindwa kutimiza vigezo kulingana na kanuni na sheria za bunge sisi wananchi atuna neno.
 
Tuangaze macho yetu kwenye ibara ya 83 (1) a&b ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeweka wazi shauri linalo weza funguliwa Mahakama Kuu juu ya uamuzi wa kama mtu ni mbunge au la?Katiba imegawanya mashauri katika aina mbili ambazo ni kama ifuatavyo

1. Moja juu ya hoja kama uteuzi wa mtu kuwa mbunge ulikuwa halali au si halali 83(1)(a)
2. Kuhoji kama kiti cha mbunge ki wazi au la (83) (1)(b).

Sasa niende kwenye scenario na maoni yangu juu ya uamuzi wa jaji kuyakataa maombi kwa sababu alizo toa hususani kuamua kuwa kuyakubali maombi ya lissu ni kuleta mgogoro wa kikatiba.

SPIKA NDUGAI alitangaza kuwa kiti cha Mbunge(Tundu Lissu) kiwazi, na tume hapo hapo ikatisha uchuguzi ambao kimsingi chadema hawakushiriki na hivyo in my opinion hawangeweza kuwa na uhalali wa kupinga uchaguzi ambao uliitishwa na tume na wao kutoshiriki(locus standi).

Lakini hoja kuu hapa ni je ni kweli kiti cha Mbunge lissu kilikuwa wazi kama alivyosema spika,Je spika ana discrestion power ya kutangaza tu kiti cha mbunge ki waz au kuna utaratibu wa kisheria hadi kufikia huo uamuzi.

Ikiwa ni hoja ilikuwa ni katiba kama alivyosema NDUGAI JAJI alipaswa kujikitia kwenye Ibara 83(1)(b) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Jaji pia anapaswa kuanza na ibara ya 13 yote na husussani ibara ya 13(6) ya katiba ya Tanzania huku akijiuliza kama masharti yaliyowekwa kwenye ibara hiyo yalifuatwa maana kitafsiri katiba haiosomwi kwa kuangalia ibara moja ni lazima uisome kwa pamoja kupata uhalali wa maamuzi kikatiba.

Baada ya kujiuliza maswali kadha ya kiprocedure/hatua za uamuzi jaji pia alipaswa kuijielekeza pia kwenye substantive rights.

Kwa maoni yangu kwa kuwa msingi wa shauri ni katiba na ni juu ya maamuzi yalifanywa na spika kwa mujibu wa sheria kama alivyo dai hivyo Mahakama kuamua kuwa maamuzi kuwa spika alikosea kutangaza kiti cha mbunge kiwazi hayawezi sababisha mgogoro wa kikatiba.(interpretation is mine)

Ngoja nitoke nje ya mada. Hivi mbunge ana kazi gani. Je ni haki mbunge mgonjwa wa more than 2 years kwa ubunge Wa 5years kushika tu madaraka wakati hawezi kutimiza wajibu wake. Wengi mnamtambua Lissu kama former president of TLS. Na mpiga domo. Lakini sio kama mpga kazi wa jimboni kwake.
 
Hata wakati wa mabishano ya korosho, Jiwe alitishia kuwafukuza wabunge 27 wa Lindi na Mtwara akiwamo PM pamoja na kuwapiga shangazi zao iwapo wangeendelea kumbishia. Wakanywea mpaka Leo.

Back
Top Bottom