Je, ni kweli kuna sehemu takatifu duniani au ngonjera na ukoloni wa kijamii?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,709
Kwanza salamuni wana jamvi.

Huwa siachi kujiuliza tena kwa kusononeka nisikiapo maeneo kama Jerusalem na Makka na mengine yakiitwa matakatifu kana kwamba dunia iliyobaki ni chafu. Huwa sipati jibu. Ajabu ya maajabu, sehemu tuambwazo ni takatifu ni majangwa yasiyo na uzuri wowote kuishi viumbe! Sehemu zenyewe ni vumbi na vurugu tupu. Hebu tuelimishaneni na kujielimisha.

Hivi kuna sehemu takatifu kuliko Afrika hapa duniani ambapo hata maadui zetu ambao walituletea huu ujinga wanakiri kuwa ndiko chimbuko la watu wote? Je si kweli kuwa watu wote ni waafrika hasa ikizingatiwa kuwa asili yao ni Afrika?

Kwangu binafsi, nadhani–––kama ni utakatifu–––basi dunia yote ni takatifu hasa ikizingatiwa kuwa takriban sayari zote zilizomo angani hazina maisha wala uzuri kama wa dunia.

Naomba kutoa hoja wanangu.
 
Yani unaambiwa kwako Mmakonde si patakatifu, kwangu Muarabu, Myahudi au Muhindi ndiko patakatifu.

Na wewe unakubali?

Hapo hakuna utakatifu, ila ujinga wako unaweza kufanya kile kitu kinaitwa "self fulfilling prophecy" ukapafanya hapo pahali kukubalika kuwa ni patakatifu.

Umenikumbusha habari moja ya Elijah Muhammad, kiongozi wa "The Nation of Islam", kikundi cha Waislamu wa Marekani kikichovuma sana kuanzia miaka ya 1950s.

Elijah Muhammad aliendesha Uislamu tofauti sana na Uislamu wa Shia au Sunni, wake ulikuwa wa kisiasa zaidi kwa watu weusi dhidi ya weupe. Aliita watu weupe mashetani. Huku ndiko alikopatia umaarufu Malcolm X.

Sasa kuna kipindi Waislamu wa kweli huko ma Sunni wakawa wanamshtukia, wakamuona anafanya utapeli, wakataka kumuadabisha.

Elijah Muhammad naye akawajia juu, akawaambia mkinibana sana mambo yangu, nitawaambia wafuasi wangu waache kuelekea Kibra ya Mecca kqtika salat, waelekee Kibra yetu mpya ya Chicago.

Elijah Muhammad alielewa kwamba hizi sehemu takatifu hazijawekwa na Mungu, ni sehemu zimetungwa na watu tu.

Mwishowe wakamuachia afanye anavyotaka, na Waislamu wa Marekani chini yake wakaendelea kuelekea Kibra ya Mecca.

Watu wana uwezo wa kutengeneza kitu kinaitwa "manufactured reality".

Leo hii tunajivunia nchi inaitwa Tanzania.Tunaadhimisha Muungano. Kabla ya 1964 hili jina Tanzania wala nchi ya Tanzania haikuwapo. Imetungwa tu na kina Nyerere na Karume. Lakini ndiyo nchi yetu.

Na kabla yake mzungu alikuja akafanya mpaka wa koloni lake. Mpaka umemtenganisha Mmasai wa Longido na wa Kenya, hawa ndugu jirani kabisa, wamekuwa katika nchi mbili tofati.

Tunaambiwa huyu Mmasai yuko nchi moja na Mmakonde wa Mtwara, na Mmakomde wa Mtwara naye katenganishwa na ndugu yake aliye upande wa pili wa mto Ruvuma aliye Msumbiji. Huyu Mmasai na Mmakonde wamekuwa ndani ya nchi moja Tanzania licha ya kuwa mbali sana, na ndugu zao kabila moja majirani kabisa wanakuwa wako nchi nyingine kwa sababu ya mipaka ya kuwekwa na watu.

Yani watu wanajiundia ukweli wao, wanafanya kitu kisicho kweli kikawa kweli.

Mifano ni hela za makaratasi, hazina thamani, ni watu tu wamezipa thamani.

Na hizo sehemu takatifu ni hivyo hivyo.

Watu tu wameamua kuzipa utakatifu.
 
Yani unaambiwa kwako Mmakonde si patakatifu, kwangu Muarabu, Myahudi au Muhindi ndiko patakatifu...
Mwanangu Kiranga kwanza big up. Ni wachache wenye taamuli na utambuzi kama wako. Tungekuwapo kama milioni moja Afrika, sina shaka tungeweza kuwavusha wenzetu wanaotapeliwa hadi kujifunza kujichukia na kuchukiana kwa upuuzi huu unaoitwa imani ambapo matapeli kama Gwajima wameutumia na kuwa matajiri. Wangejua waarabu na wayahudi, wahindi na wazungu wanavyotubagua wasingepwakia huu upumbavu wa dini.

Hata hii dhana ya Mungu mmoja waliiba Afrika wakaitumia dhidi ya waanzilishi wake sawa na dhana nyingi kama vile demokrasia na nyingine. Ukifanya uchunguzi wa kina utakuta hata haya majitu yanayotukuzwa kama vile yesu na muhamad saa nyingine hata hayakuwapo. Yametengenezwa ili kutumika kuwapumbaza waswahili wajinga na kuwanyonya.

Nimependa approach yako kwenye dhana ya utakatifu na mambo mengine kama hayo ambayo kimsingi siyo realistic bali ritualistic.

Asante sana mwanangu Kiranga umenifanya nijisikie fahari.
 
Afirika au wafirika pana utakatifu hapo? Jerusalama na Makka ni sehemu takatifu kuliko unavyofikiria,na huwezi kuamini enzi hizo kabla ukoo wenu haujafikirika kuwepo, hizo sehemu takatifu zilikuwa jangwa kama huku kwa Mwafirika kulikuwa msitu na sehemu nyingi za vichaka vya hapa na pale ndio pengine mkaonekana au kukaonekana wanaokaa huku wote ni Wafirika, nakutaka uondoe zana kuwa bara hili linaishi weusi peke yao hata wa rangi azipendayo Magufuli wapo.
 
Afirika au wafirika pana utakatifu hapo ? Jerusalama na Makka ni sehemu takatifu kuliko unavyofikiria,na huwezi kuamini enzi hizo kabla ukoo wenu haujafikirika kuwepo ,hizo sehemu takatifu zilikuwa jangwa kama huku kwa Mwafirika kulikuwa msitu na sehemu nyingi za vichaka vya hapa na pale ndio pengine mkaonekana au kukaonekana wanaokaa huku wote ni wafirika,nakutaka uondoe zana kuwa bara hili linaishi weusi peke yao hata wa rangi azipendayo Magufuli wapo..
Phew! Japo una haki ya kujieleza, huu ushuxxxzi uliotoa umeniacha hoi kiasi cha kukosa la kuongeza hasa nikiangalia ulichotapanya hapa. Haya endelea na ukoloni wako kichwani ukisifia vya wenzio na kuponda vyako.

Ama kweli mental slavery bado iko hai barani kwetu. Du! Sina hamu wala sikutegemea kuwa enzi hizi tungekuwa na watu wenye fikra za zama za mawe kama wewe!
 
Kazi kubwa ya mkoloni anayoifanya kwa mtu anayemtawala iwe kijamii au kisiasa ni kumuondolea KUJITAMBUA, KUJITHAMINI na KUJIAMINI. Ukiyatazama yote haya unayoyauliza yanazunguka hapo. Masuala ya dini ni matengenezo ya wanadamu.

Nini watu wanaamini kuhusu Mungu, kimekuqa kikibadilika kila nyakati toka zama za kale hadi sasa. So, hata wewe unaweza ukatengeneza mahala pako patakatifu. Ukisoma historia ya Uislam, Muhamad alikuwa akienda milimani kuomba kabla hata Quran haijawepo. So haya mambo ni man's creation tu.

Ukitaka ujue haya, jiulize Adam na Hawa walikuwa dini gani. Unaambiwa walikuwa waislam, wengine wanasema walikuwa wafuasi wa Judaism. Ni uumbaji wa mwanadamu tu.
 
Hiyo strategic tourism plan, ukiangalia sehemu zote zinazoitwa takatifu watu huenda kwa wingi hivo nchi husika uingiza pato la kutosha kupitia hao watalii wanaoenda kuutafuta utakatifu ili hali huku wanakotoka wamedhulum maskini, wameua nk nk.

Mfano Mecca ni wanyama wangapi wanauzwa wakati wa kumaliza hiyo ibada? Hotel rooms ngapi zinakuwa booked.
 
Kwanza salamuni wana jamvi.

Huwa siachi kujiuliza tena kwa kusononeka nisikiapo maeneo kama Jerusalem na Makka na mengine yakiitwa matakatifu kana kwamba dunia iliyobaki ni chafu. Huwa sipati jibu. Ajabu ya maajabu, sehemu tuambwazo ni takatifu ni majangwa yasiyo na uzuri wowote kuishi viumbe! Sehemu zenyewe ni vumbi na vurugu tupu. Hebu tuelimishaneni na kujielimisha.

Hivi kuna sehemu takatifu kuliko Afrika hapa duniani ambapo hata maadui zetu ambao walituletea huu ujinga wanakiri kuwa ndiko chimbuko la watu wote? Je si kweli kuwa watu wote ni waafrika hasa ikizingatiwa kuwa asili yao ni Afrika?

Kwangu binafsi, nadhani–––kama ni utakatifu–––basi dunia yote ni takatifu hasa ikizingatiwa kuwa takriban sayari zote zilizomo angani hazina maisha wala uzuri kama wa dunia.

Naomba kutoa hoja wanangu.
Father of All nakumbuka tulipokuwa tunafundishwa tafsiri ya Quran sura ya Tembo (105), tuliambiwa mfalme Abraha alikuwa akichukizwa sana na jinsi watu wakienda kufanya ibada (Hija) kwa kuzuru mji wa Makka, basi akaamua kwenda kuvunja ile Kaaba, na matokeo yake ndiyo yale yanayosimuliwa kwenye hiyo sura.

Kwa kuwa tunapashana habari si vibaya tukipitia kwenye link ya Wikipedia na kuangalia mfalme aliyetaka kutengeneza sehemu yake takatifu na kutaka kuharibu sehemu takatifu ya wenzi wake.

Yani unaambiwa kwako Mmakonde si patakatifu, kwangu Muarabu, Myahudi au Muhindi ndiko patakatifu.

Na wewe unakubali?

Hapo hakuna utakatifu, ila ujinga wako unaweza kufanya kile kitu kinaitwa "self fulfilling prophecy" ukapafanya hapo pahali kukubalika kuwa ni patakatifu.

Umenikumbusha habari moja ya Elijah Muhammad, kiongozi wa "The Nation of Islam", kikundi cha Waislamu wa Marekani kikichovuma sana kuanzia miaka ya 1950s.

Elijah Muhammad aliendesha Uislamu tofauti sana na Uislamu wa Shia au Sunni, wake ulikuwa wa kisiasa zaidi kwa watu weusi dhidi ya weupe. Aliita watu weupe mashetani. Huku ndiko alikopatia umaarufu Malcolm X.

Sasa kuna kipindi Waislamu wa kweli huko ma Sunni wakawa wanamshtukia, wakamuona anafanya utapeli, wakataka kumuadabisha.

Elijah Muhammad naye akawajia juu, akawaambia mkinibana sana mambo yangu, nitawaambia wafuasi wangu waache kuelekea Kibra ya Mecca kqtika salat, waelekee Kibra yetu mpya ya Chicago.

Elijah Muhammad alielewa kwamba hizi sehemu takatifu hazijawekwa na Mungu, ni sehemu zimetungwa na watu tu.

Mwishowe wakamuachia afanye anavyotaka, na Waislamu wa Marekani chini yake wakaendelea kuelekea Kibra ya Mecca.

Watu wana uwezo wa kutengeneza kitu kinaitwa "manufactured reality".

Leo hii tunajivunia nchi inaitwa Tanzania.Tunaadhimisha Muungano. Kabla ya 1964 hili jina Tanzania wala nchi ya Tanzania haikuwapo. Imetungwa tu na kina Nyerere na Karume. Lakini ndiyo nchi yetu.

Na kabla yake mzungu alikuja akafanya mpaka wa koloni lake. Mpaka umemtenganisha Mmasai wa Longido na wa Kenya, hawa ndugu jirani kabisa, wamekuwa katika nchi mbili tofati.

Tunaambiwa huyu Mmasai yuko nchi moja na Mmakonde wa Mtwara, na Mmakomde wa Mtwara naye katenganishwa na ndugu yake aliye upande wa pili wa mto Ruvuma aliye Msumbiji. Huyu Mmasai na Mmakonde wamekuwa ndani ya nchi moja Tanzania licha ya kuwa mbali sana, na ndugu zao kabila moja majirani kabisa wanakuwa wako nchi nyingine kwa sababu ya mipaka ya kuwekwa na watu.

Yani watu wanajiundia ukweli wao, wanafanya kitu kisicho kweli kikawa kweli.

Mifano ni hela za makaratasi, hazina thamani, ni watu tu wamezipa thamani.

Na hizo sehemu takatifu ni hivyo hivyo.

Watu tu wameamua kuzipa utakatifu.
Umenikumbusha movie ya 'Malcom X' aliyocheza Denzel. Mwishoni alizunguana na huyo Elijah Mohammed.
 
Hiyo strategic tourism plan, ukiangalia sehemu zote zinazoitwa takatifu watu huenda kwa wingi hivo nchi husika uingiza pato la kutosha kupitia hao watalii wanaoenda kuutafuta utakatifu ili hali huku wanakotoka wamedhulum maskini, wameua nk nk.

Mfano Mecca ni wanyama wangapi wanauzwa wakati wa kumaliza hiyo ibada? Hotel rooms ngapi zinakuwa booked.
Ni kutokuwa na maarifa,na fikira zilizopanuka.Makka kuwa patakatifu,kumeleta faida dunia nzima,kwa kuongeza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja:

1: Kipindi chote cha kwenda hija,kunatumika usafiri wa nchi kavu,baharini,na angani,kwa mfano watu kutoka mikoani, wanapanda mabasi kwenda viwanja vya ndege, vya kimataifa, hapa wenye mabasi ya kwenda kwenye miji mikuu, tayari wanaogeza ajira kuanzia mafuta, vipuli, maderevya, makodakta, na serekali kupata pato kupitia kodi mbali mbali.

2. Ajira kwa mawakala wa kukata tiketi za ndege za kimataifa,makampuni ya wakala wa ndege,wanaongeza wafanyakazi,ofisi za wakala zinaongezeka mikoani,serekali inapata kuongeza mapato kupitia,kodi za ofisi,kodi za tiketi za ndege, nk

3. Viwanja vya ndege,vinapata kodi,kupitia ndege zinazotua na kuondoka,na pia kuna tozo mbali mbali kwa abiria, hapa mapato ya nchi mbali mbali yanaongezeka.

4. Ukija kwenye bahari, pia abiria wanaongezeka, kwenda kwenye miji mikubwa yenye viwanja vya ndege vya kimataifa.

5. Ukija kwenye uuzaji,wa bidhaa,kama wanyama,nafaka ,samaki, vyakula, matunda,nguo nk,kupelekwa katika mji wa Makka na Madina, kibiashara kuna mapato,kwa serekali na wananchi,wakichangamkia fursa,hizi ni mzunguko mzuri wa mapato.

6. Nchi zetu za kiaAfrika zikichangamkia fursa hizi,ni nafasi nzuri kibiashara,ni soko kubwa hili tulichangamkie.Kama tukisema ni utalii,basi huu ndio utalii wa kimataifa,kwa sababu nchi nyingi duniani, zikichangamkia ni faida kwa nchi zote duniani.

7. Ziko fursa nyingi sana,wenye mahoteli, Guest, wenye Taxi,wenye mabasi,magari ya kukodisha, kwenye miji yenye viwanja vya ndenge za kimataifa,wanafaidika,na ni kwenda kuhiji na siku za kurudi Hija.

8. Mabenki yanaobadilisha pesa za kigeni pia wanafaidika na mzunguko huu wa kibiashara.

Apewe pongezi sana aliyeanzisha,ibada hii ya Hija kwa waislamu.Inaonyesha aliona mbali, kwa kuleta uchumi kwa dunia nzima,kwa kufaidika waislamu,wasio waislamu, wasio na dini,bila kumbaguwa yoyote. Na ni faida ya mapato kwenda na wakati wa kurudi.
 
Nadhani ungejikita kwenye kujibu hoja ya mleta mada, badala ya kueleza faida zinapatikana kutokana na Hija. Mada ni je kuna mahali patakatifu Duniani?
 
Back
Top Bottom