Je, ni kweli kuhusu Amina Chifupa?

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,200
Kuna habaei za ajabu zinazunguka hapa Dar kuwa mzuka wa Amina unaonekana unafanya kazi shambani huko njombe.

I wonder kama hii kweli, kwa sababu Amina mwenyewe hata jembe alikuwa halijui, kuna aliyesikia?
 
Kuna habaei za ajabu zinazunguka hapa Dar kuwa mzuka wa Amina unaonekana unafanya kazi shambani huko njombe. I wonder kama hii kweli, kwa sababu Amina mwenyewe hata jembe alikuwa halijui, kuna aliyesikia?

Jamani,mtu akishakufa amekufa.Mtu akishafariki anatakiwa aachwe apumzike huko kwa Mungu.Haya mambo ya Kishirikina ni upuuzi mtupu.Nafikiri muda umefika sasa kuachana na fikra hizi potofu kwa sababu zinarudisha nyuma maendeleo ya Watanzania."Tazama mbele na jitahidi kuona mbali na si kutazama nyuma na kujaribu kufukua vilivyofukiwa."
 
Hapa advanced science and Technology kwa Mtanzania itabaki kuwa ndoto kama mambo yenyewe ni haya ya kufufua marehemu.

Achana na mambo ya kishirikina, "kama tumbo linanyonga kwa ndani dawa ni kwenda hospitali sio kupiga tumbo chale"

Amka watanzania!!!!!!
 
Yawezekana,hamna linaloshindikana.Mnakumbuka vie vimbwengo?
 
Hapa advanced science and Technology kwa Mtanzania itabaki kuwa ndoto kama mambo yenyewe ni haya ya kufufua marehemu.

Achana na mambo ya kishirikina, "kama tumbo linanyonga kwa ndani dawa ni kwenda hospitali sio kupiga tumbo chale"

Amka watanzania!!!!!!

heheeee, nimecheka kweli. kwa hiyo inawezekana watz tukawa primitive !
 
mwacheni Amina apumzike...alisakamwa sana enzi za uhai wake..na mkiendelea atawatembelea kweli, na akiwahoji sijui mtajibu nini!
 
Kutoka tovuti ya Majira

Familia ya Chifupa yaliumbua Kanisa

Habari Zinazoshabihiana
• Mrithi wa Chifupa aapishwa 18.08.2007 [Soma]
• Kifo cha Amina ni kurogwa, kisukari-Chifupa 13.07.2007 [Soma]
• Baba wa Amina Chifupa amtetea mwanaye 08.05.2007 [Soma]

*Ni kutokana na madai ya Amina kuchukuliwa msukule
*Mama asema kinachofanyika kanisani mazingaombwe
*Mtoto anayedaiwa kuishi msukule na Amina ni zezeta
*Mzee Chifupa naye aweka hadharani utafiti wake

Na Timu ya Majira Jumapili

SIKU chache tu baada kuibuka taarifa za kutatanisha kuwa aliyekuwa Mbunge wa CCM kupitia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV-CCM) marehemu Amina Chifupa kuwa hajafa na kwamba amechukuliwa msukule, familia yake imeibuka na kuithibitishia Majira Jumapili kuwa wameshafanya utafiti wa kina na sasa wanaijua siri kuu ya aliko Amina.

"Hivi ninavyozungumza na wewe, sisi familia tumefanya utafiti wa kina na sasa tumeamua kukaa kimya, hatupendi kujiingiza katika suala hilo, ila kama kuna mtu yeyote; mchawi, muumini wa Kanisa au mganga wa kienyeji anayedai Amina amechukuliwa msukule, sisi hatutaki kuamini hayo, ila anayeweza kumrejesha afanye hivyo kuliko watu kupiga kelele tu," amesema Mzee Gabriel Hamis Chifupa, baba mzazi wa Amina alipozungumza na Majira Jumapili juzi.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili kwa wiki kadhaa sasa, madai kuwa Amina hajafa na kwamba yuko kwenye mashamba ya miwa katika eneo moja wilayani Kibaha, yalianza kusambazwa na waumini wa Kanisa liitwalo Glory Christ lililopo Ubungo, Dar es Salaam.

Kanisa hilo limeelezwa kujipatia umaarufu mkubwa katika siku za karibuni kutokana na kile kinachoelezwa na waumini wake kutokana na kipawa na karama ya hali ya juu ya wachungaji wake kuwarejesha wanadamu waliokufa katika mazingira yenye utata.

Madai kuwa Amina yu hai na kwamba anaishi kama msukule kwenye mashamba ya miwa, ziliibuka baada ya kudaiwa kuwa mmoja wa watoto aliyerejeshwa kutoa ushuhuda wake kanisani hapo, kuwa huko alikokuwa alikuwa akicheza na kuishi na Amina.

Majira kanisani

Unapofika kwenye Kanisa hilo, pamoja na waumini wenyewe kujinasibu wanapokuwa nje ya Kanisa juu ya uwezo na kipawa cha wachungaji wao, lakini Majira Jumapili katika uchunguzi wake wa kina, lilibaini kuwa hali ni ya uoga, huku ikiaminika kuwa wachungaji wa Kanisa hilo si watu wa kuzungumza na wanahabari kirahisi.

Juhudi za awali za kuwapata wachungaji hao ziligonga mwamba kutokana na kila muumini aliyedodoswa kuonekana akisisitiza kuwa suala hilo ni gumu.

Lakini wakitumia mbinu za kisasa za uandishi wa habari, waandishi wetu walifika kanisani hapo na kujitambulisha kama waumini wapya waliokuwa wakitaka kujiunga na Kanisa hilo.

Kwa hali hiyo mmoja wa wachungaji ambaye alijitambulisha kuwa msaidizi wa Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo, alianza kuwahubiria 'Neno' na kabla ya kuulizwa, alianza kuzungumzia moja ya mikakati ya sasa ya Kanisa hilo ambayo ni kumrejesha Amina.

Alidai kuwa marehemu Amina yuko hai tofauti na watu wanavyodhani, na kwamba suala la wao kumrejesha ni dogo sana, iwapo tu wazazi wake watakubali.

Mchungaji huyo alikiri kuwa chanzo cha wao kupata fununu hizo ni mtoto mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina, ambaye walimrejesha baada ya kuwa msukule ambaye aliwathibitishia kuwa Amina naye yuko mahali alikotoka yeye, ambako alipataja kuwa ni katika mashamba ya miwa yanayodaiwa kuwa Kibaha, mkoani Pwani.

"Mtoto yule baada ya kuombewa hapa hapa kanisani, alisema pamoja na kuombewa lakini anasikitika kuwa amemwacha rafiki yake aliyekuwa akicheza naye na kufanya wote kazi Kibaha," alidai Mchungaji akimkariri mtoto huyo.

Alidai mtoto huyo alipoulizwa rafiki yake ni yupi aliyemwacha kwenye mashamba hayo, alimtaja Amina Chifupa, kitu ambacho kiliwashangaza waumini na kwamba baada ya kutoa ushuhuda huo, habari hizo zilienea sehemu mbalimbali za Jiji hadi zikamfikia mama yake Amina, Bibi Julieth Mbanga.

Mchungaji huyo alidai baada ya mama yake Amina kupata taarifa hizo, alifika kanisani hapo ili kupata taarifa zaidi.
"Alikuja hapa kanisani tukamwambia ikiwa ataamini na kukubali kuombewa mtoto wake atampata," alisema Mchungaji huyo.

Baada ya hapo inadaiwa Mama Amina alikubali kuombewa. "Alienda pale (akionesha eneo moja kwenye kanisa hilo) akafumba macho na kuombewa na kumwona mwanawe Amina," aliendelea kudai Mchungaji huyo.

Akieleza zaidi kilichotokea, Mchungaji huyo alisema Mama Amina alipomwona mwanawe alitimua mbio huku akimwomba Mchungaji asitishe maombi hayo.

"Hata walipofika nyumbani, siku nzima hakulala walikuwa wamejawa na hofu familia nzima," alidai Mchungaji huyo.

Aliongeza kuwa baada ya maombi yaliyomwezesha kumwona mwanawe, mama mzazi huyo wa Amina, alirejea nyumbani kwa ahadi kuwa angerejea baada ya kushauriana na familia yake, lakini hadi alipozungumza na gazeti hili, alithibitisha kuwa mama huyo hakurejea tena kanisani hapo.

"Kazi ya kumrejesha Amina ni ndogo kama wakija tunamrejesha kwa maombi hata leo hii," alidai.

Alipoulizwa alipo mtoto aliyemwona marehemu Amina, Mchungaji huyo alidai amefichwa ili asisumbuliwe na watu.

"Hili la Amina kuna siri nyingi na watu wanaweza kumsaka yule mtoto na kumdhuru, je, tungeamua kueleza mengine aliyoyasema kuhusiana na baadhi ya watu wake wa karibu wanavyohusika (na msukule huo) si ingekuwa balaa?" alihoji Mchungaji huyo na kuongeza kuwa ndiyo maana mtoto huyo wamemweka katika ulinzi mkali.

Wanavyofufua misukule

Mchungaji huyo alidai mtu anapoamini katika Kanisa hilo na akawa na ndugu yake aliyekufa kifo cha utata, anaweza kupelekwa katika maombi maalumu na ndani ya wiki moja akajua kama ndugu yake huyo alikufa kifo cha kawaida au la.

Akieleza utaratibu wa maombi kanisani hapo, alisema ili kumfufua mtu wao huanza Jumatatu ambapo pia huombea wagonjwa. Maombi hayo huendelea Jumatano kwa waumini kufunga na Ijumaa ndipo husomwa maombi maalumu ya kufufua waliochukuliwa misukule.

Kanisani hapo gazeti hili lilishuhudia waumini wengi wakiendelea na ibada mbalimbali za maombi huku ndani ya Kanisa kukiwa na bendera mbili; ya Tanzania na nyingine iliyoelezwa kuwa inawakilisha Taifa la wana wa Israeli.

'Naogopa mzimu'

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam, mama mzazi wa mwanasiasa huyo aliyekuwa machachari aliyetabiriwa angefika mbali katika safari yake ya kisiasa, alithibitisha kusikia taarifa hizo, lakini 'akaruka kimanga' kwenda kanisani hapo.

"Nilizipata taarifa za marehemu Amina kuonekana kwenye mashamba ya Kibaha kupitia kwa rafiki zangu wawili, ambao walinitaka pia niende kanisani hapo nikaombewe," alisema akionekana mwenye majonzi na kusisitiza kuwa hakwenda.

"Kama Kanisa hilo lilikuwa na uwezo wa kumfufua, lingefanya hivyo pale kifo kilipotokea," alisema.

Alipoulizwa kama yuko tayari kuwapa idhini wachungaji wa Kanisa hilo kumrejesha mtoto wake kutoka msukule, alisema akihoji:

"Mambo mengine ni kama mazingaombwe, wanaweza kutengeneza kitu chenye sura ya Amina kumbe ni jini, matokeo yake mambo haya yakatuletea matatizo sasa tutaonekanaje ndani ya jamii?"

Akionekana kutoyaamini madai ya Kanisa hilo, mama huyo alisema amesikia kuwa hata huyo mtoto anayedaiwa kumwona Amina hakuwa amechukuliwa msukule bali alikuwa na matatizo ya akili.

"Yule mtoto hakuwa amechukuliwa msukule kule kwenye mashamba ya Kibaha kama inavyodaiwa, bali alikuwa na matatizo ya akili," alisema akiongeza kuwa maneno hayo alielezwa na baadhi ya waumini wenyewe wa Kanisa hilo.

'Tunachokiamini'

Akitoboa siri ya kile familia yake inachokiamini kwa sasa, Mzee Chifupa katika mahojiano ya juzi, alisema Amina ameshawatokea ndugu zake ndotoni na kuwaeleza kuwa yuko kwa Mungu.

"Hatutaki ku-intertain (kuyakubali) haya maneno ya msukule, wala sisi kama familia hatutaki kujiingiza katika hilo. Msimamo wetu kwa sasa ni kwamba kama ambavyo mwenyewe alivyowatokea shangazi na mama zake wakubwa na kuwaeleza kuwa yuko kwa Mungu, sisi tunaamini hivyo," alisema.

Hata hivyo, Mzee Chifupa alilidokeza gazeti hili kuwa amefanya utafiti wa kina katika madai ya Kanisa hilo na kubaini kuwa hakuna usahihi.

"Nimefanya utafiti wangu na nilichokiona ni kwamba hakuna usahihi, tungeona ukweli tungekubali. Hatutaki matatizo lakini pia hatumzuii mtu, mwenye uwezo, afanye tuone," alisisitiza.

Mwezi huu Amina atatimiza miezi minne tangu alipofariki Julai 26 mwaka huu na familia yake imesisitiza kuwa bado wamebaki na kiza kinene;upweke umewatawala, wanajitahidi kuyazoea maisha bila yeye, ingawa mtu wa kwanza anayeonekana kuyazoea maisha hayo kwa haraka ni mtoto wa marehemu, Rahman ambaye Majira ilimkuta akicheza kwa furaha nyumbani hapo huku akimwita bibi yake kuwa ndiye mama yake.
 
Kutoka tovuti ya Majira

"Nilizipata taarifa za marehemu Amina kuonekana kwenye mashamba ya Kibaha kupitia kwa rafiki zangu wawili, ambao walinitaka pia niende kanisani hapo nikaombewe," alisema akionekana mwenye majonzi na kusisitiza kuwa hakwenda.

Duh, hii kali....au niseme ni kalikiti.
 
Back
Top Bottom