Je, ni kweli kila mwanamke huja na nyota yake ambayo humfanya mwanaume afanikiwe au amefeli katika maisha?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Maisha huwa yana Siri nzito linapokuja swala la mwanaume ktk kufanikiwa ktk maisha kila mtu huzungumza la kwake ila leo nataka tuzungumzie nyota za wanawake.

Je,ni kweli kuna mwanamke nyota yake akiingia katika mahusiano na mwanaume kama nyota yake itaendana au itapenda mwanaume basi mwanaume atafanikiwa

Lakini pia kuna wengine husema wapo wanawake nyota zao ambazo akikutana na mwanaume orvious atafeli katika maisha kufanikiwa kwake ni ngumu sana

Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili jambo?
 
binafsi sikupingi kuna toto moja kila likinitafuta basi nakuwa sina mkwanja hadi naonekana mzinguaji.

ila kuna dem mmoja niliwahi kuwa nae daa yaani haipiti siku tatu unaitwa tu kwenye mishe fulani na mkwanja wa maana unapata, ubaya nilimpoteza kijinga sana na now ni single maza ila alikuwa na nyota ya kuleta mambo mazuri tu kwangu.
 
Huu ni uongo.

Niamini mimi, utajikuta umekua malaya ili kujaribu kumpata utakayetembelea nyota yake.
 
binafsi sikupingi kuna toto moja kila likinitafuta basi nakuwa sina mkwanja hadi naonekana mzinguaji.

ila kuna dem mmoja niliwahi kuwa nae daa yaani haipiti siku tatu unaitwa tu kwenye mishe fulani na mkwanja wa maana unapata, ubaya nilimpoteza kijinga sana na now ni single maza ila alikuwa na nyota ya kuleta mambo mazuri tu kwangu.
Wewe umempoteza kijinga.

Ameenda kukutana na mtu mwingine mpaka wamezaa na wameachana.

So hamjali juu ya nyota zenu kung'arishwa? SMH
 
Nadhani kuna ukweli ambao wanaume hatuupi kipaombele saana na hili ni sehem ya mambo ambayo zamani wazee walikua wanapendekeza pindi ukitaka kuoa basi wanapendekeza wapi ukaoe
 
  • Thanks
Reactions: DVC
ni kwel kuna kuna wanawake, wanabahati sana kwenye maishaaa! yan ukiwa naye kwenye mahusiano basi lazima mambo yakae sawaa! pia kuna wadada wana mkosi, yan hata ukitiana tu kesho yake lazima upate bala!

pia vivyo hvyo kwa wanaumee, kuna wenye mikosi kama nin! yan ukiingia noa kwenye mahusiano ni bora Muowane tu mkiachana hutaolewaa kamwe!

ushahidi kaa hili zipo nying sanaa!
 
Nadhani kuna ukweli ambao wanaume hatuupi kipaombele saana na hili ni sehem ya mambo ambayo zamani wazee walikua wanapendekeza pindi ukitaka kuoa basi wanapendekeza wapi ukaoe
sure, na mara nyingi wanaangalia familia sana historical background
 
mambo ya riziki mungu alimaliza katika uumbaji hivo hizi imani zingine ni za kusadikika tu, unaweza kutana na ke A kumbe katika wakati ule riziko yako ni kiduchu bt ukakutana na ke B wakat ambao rizik yako ni kubwa nawe ukajenga iman juu ya mwanamke yule, mtoaji ni mungu ni si mwanamke hilo tambua.
 
Ni kweli kabisa, ingawa mwenye bahati kwako si lazima awe nayo kwa wote hali kadhalika mwenye mikosi kwako si lazima awe hivyo kwa mwingine.
 
Haya mambo ya nyota sijawahi kuyaelewa hata kidogo, niliwahi kusoma uzi wa mkuu mmoja humu niliishia kuchanganyikiwa tu.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Hamna cha nyota wala nini. We bana kama uko kwenye channel ya hela utafanikiwa tu, na kama haupo ndio ivyo tena haijalishi unatembea na nani. Kwanza kwa jinsi siku izi tunavyotembea na wanawake wengi si kila siku ingekua leo mkosi kesho bahati keshokutwa mkosi.
 
binafsi sikupingi kuna toto moja kila likinitafuta basi nakuwa sina mkwanja hadi naonekana mzinguaji.

ila kuna dem mmoja niliwahi kuwa nae daa yaani haipiti siku tatu unaitwa tu kwenye mishe fulani na mkwanja wa maana unapata, ubaya nilimpoteza kijinga sana na now ni single maza ila alikuwa na nyota ya kuleta mambo mazuri tu kwangu.
Hyo staili ilishawahi kunitokea sana mkuu kwa mademu kama 3 tofauti tofauti.
Unakuta napata demu ambaye nimemkubali sana na ana sifa zote za kuwa wife material ila nikianza kujipanga tu nikakitambulishe kwao aisee uchumi unayumba nakosa hata buku tu ya nauli ya kwenda kwao hadi mwisho wa siku penzi linavurugika automatically.
Sasa jiulize mtu hata buku ya nauli sipati nitalipaje mahari.
 
Wewe nenda kwenye maombi.
 
Back
Top Bottom