Mpeni sifa Yesu
JF-Expert Member
- May 23, 2010
- 646
- 129
Maneno yapi? kubali ukweli na ujirekebishe? usiwe kama Yuda isikari yote aliyekuwa miongoni mwa wale 12 waliokiri kuwa hakuna hata mmoja wa kumsaliti mwishoni akamsaliti.
ndani ya upentecoste kuna tatizo na wenye macho ya kiroho na kimwili wanajua hilo na ndiyo maana hata wachungaji wenyewe kwa wenyewe wanashambuliana, hata kushambuliana kuwa wengine wanajihusisha na ushirikina. Kakobe humshambulia rwakatare mara kwa mara, na wengine kama akina Katunzi kupitia wapo radio ndiyo usiseme ni matusi ya kejeli kwa watumishi wengine wapentekoste mbele kwa mbele.
Vipofu wa kiroho kama wewe ni vigumu kuliona na wanajivunia haya, ilimradi tu wanadai ni wapentekoste. Unaishia kuhukumu na kutukana watu! wewe una hadhi gani ya upentekoste? kwa sababu tu unasali kwa kakobe? Kumbuka Yesu alisema Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo mbinguni hamwingii. Hawa watumishi wapentecoste wanaojimbana kila siku, huo ndio wito wao?
ikiwa watumishi wanashambuliana hizi muda wa kujenga systems za uongozi na utawala ndani ya makanisa yao kushughulikia migogoro midogo mpaka wanakimbilia kwa waandishi watakuwa nao?
Wengi pengine hata wewe mmegeuza upentecoste kichaka kama si fimbo ya kuchapia wengine kwa kigezo cha repent na uokoke.Ni lazima kutoa boriti ndani ya jicho lako kabla ya kupiga kelele kuhusu kibanzi cha mwenzako.
Kumbuka Yesu alisema wengi watakuja watasema "Bwana Bwana...., naye atawajibu siwajui, ondokeni." Upentekoste wako isiwe fimbo ya kuhukumu na kutukana wengine na kujiona wewe ni bora zaidi ya wengine mbele za Mungu.
ndugu yangu, mimi wala sisali kwa kakobe, wala usihangaike kugesi vitu. pia, tusifike mbali. nimesema wewe si mpendecost kwasababu niliona umejiunga na wapinga kristo kushambulia ukristo, na hivyo utapata thawabu ya wapinga kristo. upentecost haumfikishi mtu mbinguni hata hivyo, na kwenye upentecost kuna madhehebu mengi..yote hayo ni taratibu tu za kuwafikisha watu kwenye njia sahihi wamwone Mungu wao wenyewe ibinafsi...si ticket toka kwenye dhehebu kuwa ndio ufike mbingini, pamoja na kwamba, si madhehebu yote yana system nzuri ya kumlisha mtu Neno la Mungu akamwona Mungu.
watu waliookoka wana hofu ya Mungu, watu waliookoka huwa hawakurupuki tu kumshambulia mtu hasa anayejihusisha na mambo ya Mungu, kwasababu kufanya hivyo ni kitu hatari kwao, ndio maana nikasema wewe sio mpentecost kwasababu niliona hauna hata hofu ya Mungu, siku maanisha kuwa wewe nim wenye dhambi sana la hasha, bali hauna tabia za kipentecost....ukimgusa mtumishi wa Mungu, unagusa mboni ya jicho la Mungu. hata tz kuna watumishi wa Mungu wengi sana, pamoja na kwamba unaona kama wanashambuliana wao kwa wao, haiwatoi kwenye fact kwamba bado ni watumishi wa Mungu. kukemeana katika wokovu ni kitu cha kawaida, na wachungaji si malaika. Paulo alimkemea Petro mbele za watu kabisa kwasababu petro aliteleza kidogo, na bado tu wote waliendelea kutumika mbele za Mungu. NI NANI ATAWAHUKUMU WATEULE WA MUNGU? MUNGU NDIYE MWENYE KUWAHUKUMU, na si mwanadamu...ukifanya hivyo utakula jeuri yako.
Miriam dada yake Musa pamoja na wengine, walijiunga kwenye kikundi wakamshambulia Musa kuwa kwanini amemuoa mwanamke methiopia/kushi/seba,....kilichotokea, haijalishi kama walikuwa sahihi au la, Mungu alishuka kwa hasira, AKAMPIGA MIRIAMU KWA UKOMA, ilibidi Musa aanze kumwomba mungu upya ili amponye tena.
Ndugu yangu, watumishi wote wa Mungu huwa wanatukanwa na kusinginziwa mambo mengi, Yesu mwenyewe alitukanwa na kusingiziwa, ni vita tu vya shetani, ila mwishoni huwa inakuja kugundulika kuwa walikuwa wanaonewa tu pamoja na kwamba wamesharushiwa matope hadi wamechoka....usikurupuke tu kuanza kushambulia, huwezi kujua kakobe au mtumishi yeyote wa Mungu yuko kwenye vita ipi katika ulimwengu wa roho wa hapo tz...in order for you to be safe, tulia kimya, mwombe Mungu awasaidie watumishi wa Mungu kwenye vita, au pale walipovunjika moyo au kuteleza, ili wasimame na kazi ya Mungu iendelee...HAUNA HATA SAUTI YA KUWAHUKUMU WATUMISHI WA MUNGU. ushauri wangu ndio huo..unaweza kuendelea kurusha mawe yako...lakini nakuhakikishia, utaona matunda yake siku moja na utakuwa wa kwanza kwenda kuwambia watu waache ulichokuwa unakifanya. Mungu akusaidie, na wote.
by the way, watu wawili tu wameshikilia bango jambo hili....na mko biased sana!