Je!? Ni kweli kakobe alitaka kuvunja ndoa ya mtu singida? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je!? Ni kweli kakobe alitaka kuvunja ndoa ya mtu singida?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by analysti, Jul 16, 2010.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Kuna habari imerushwa na TBC1 Jana ikimuonyesha mama mmoja aliyetambulishwa kuwa ni mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship tawi la Singida linaloongozwa na Askf. Z.Kakobe, akilalamika kuwa askofu huyo amekuwa akitaka kuvunja ndoa yake kwa kumlazimisha Mume wake Amuache na aandike barua ya kuachana nae kwa kile alichodai kuwa ni ukiukwaji taratibu za kanisa uliofanywa na mama huyo!!.

  Mama huyo aliendelea kulalamika kuwa, askofu huyo amekuwa akiwaongoza kwa vitisho kedekede vinavyo wafanya wengi wao kutothubutu kuzungumza maovu wanayofanyiwa na askofu huyu ambae kanisa lake kuu lipo pale Mwenge.

  Swali linakuja kwetu wanaJamii kuwa kama shutuma hizi ni za kweli, ni kweli viongozi hawa wanaendesha makanisa kwa kuongozwa na roho wa mungu??.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  No comments
   
 3. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  kwa nini?
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndio raha ya kuwa mkoloni.
  Na ndio raha ya kukubali kutawaliwa.
   
 5. b

  bob giza JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi kakobe nilishamfutaga kitambo..(am sorry kwa nitakaowakwaza!!)
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,995
  Trophy Points: 280
  Je kakobe ni mtuymishi wa mungu yupi?
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ninavyomjua kakobe, hasa kwenye hilo suala la ndoa, anaamini kuwa, ukishaolewa basi hautakiwi kuachana na mumeo, ukiachana naye ukaolewa na mwengine, unatenda dhambi. pia, anaamini kuwa, kama ulikuwa nyumba ndogo hata kama umezaa na mwanaume huyo watoto wengi, ni dhambi na unatakiwa kuachana naye. ukiwa kwenye mitara pia ni hivyohivyo. NA HII NI BIBLICAL, anasema ukweli kufanya hivyo. Tatizo ni kwamba,ukiwaita watu waje kuokoka, anakuja kila mtu ni sawa na umetupa nyavu baharini kukusana samaki changu, unakusana kamba, unakusanya kila aina ya samaki. wengi huwa wanaokoka lakini kumbe walikuwa wanaishi na wanaume za watu, walikuwa kwenye mitara etc. sasa baada ya kuokoka, kakobe huwa anawaambia waachane na vitu kama hivyo ili watafute waume zao halali kibiblia.

  ukitaka kumhukumu mtu, msikilize kwanza, nyie mnaosema kuwa mlishamfuta, mnaonyesha upeo mdogo wa utu uzima na uelewa...you can't judge somebody without giving him a chance to be heard and defend himself..na usikikilize upande mmoja wa shilingi, weka zote mbili ndo utapata jibu kamili.

  zaidi ya yote, kakobe ni mwanadamu, anaweza kuwa na mapungufu yake, hakuna malaika duniani. na hiyo haimpunguzii kutukuwa mtumishi wa Mungu. watu wengi huwa wanachanganya hii kitu, mtumishi wa Mungu akikosea, wanaruka juu, wanauliza kwanini...hawajui kama yeye naye ni mwanadamu kama wao. hata watumishi wote na manabii walikosea sana lakini Bado walikuwa watumishi wa Mungu..Yesu peke yake hakutenda dhambi, wengine wooote walitenda dhambi nyingi tu na bado Mungu aliendelea kuwaregard kuwa watumishi wa Mungu. KAMA MUNGU AKIHESEBU MAOVU, NANI ATASIMAMA JAMANI.....

  watu wanasema kakobe anawakandamiza, lakini hajawalazimisha kuendelea kusali pale, si wahame kanisa...mbona huwa habembelezi na huwa anafukuza hata kufukuza mtu akifanya upuuzi? Tz ina uhuru wa kuabudu. Mimi siwezi kujaji jamaa bila kumsilikiliza yeye kwanza....
   
 8. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Je!? Inawezekana ikawa alimpa uchungaji mtu ambae hayuko kwenye ndoa halali?, na huyo mume wa huyo mama anayeshawishiwa kumuacha mke wake kakobe anakutana nae wapi kama si hukohuko kanisani!. Na kama huyo mama anamatatizo kwa nini asimvue uchungaji badala yake anamtenganisha na mume wake?

  Mpendwa binafsi natambua kuwa kakobe ni binadamu kama wengine na anastahili kufanya makosa akiwa kama binadamu, lakini kuna makosa ambayo akiyafanya mtu kama yeye yanafanya uhalali wake kama kiongozi wa dini utiliwe mashaka.Na pengine hata mungu kumuondolea upako!!! kama anao anyway!
   
 9. minda

  minda JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  jibu lipo hapo kwenye rubrics; ni kweli viongozi hawa wanaendesha makanisa kwa kuongozwa na roho wa mungu na wala siyo Roho wa Mungu, kitu ambacho ni kondoo wachache sana wanalitambua. [​IMG]
   
 10. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #10
  Jul 16, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari nilisikia asubuhi pia. ipo kwenye gazeti la mwananch. ngoja tuicheki vizuri then tutacome back
   
 11. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ndiyo inawesekana kuwa alimpa uchungaji mtu ambaye hayuko kwenye ndoa halali. this depends on whether huyo mama alidisclose laifu lake lote au la...haowever, this was just my speculation, sitakuwa na jibu lote kwasababu sijui issue yenyewe itakuwaje. ila ninachowahakikshia ni kwamba, issue itakavyokuwa inaendelea, itakuwa wazi na nyie mnaojaji mtu bila kuangalia upande mwengine wa shilingi, mtapata aibu tu. cha kufahamu ni kwamba, kakobe ana maadui wengi ajabu, hata selikali yenyewe, waandishi wa habari wengi ni maadui zake na hawampendi. Tanesco ndo usiseme....kuna mwandishi mmoja hivi wa Tbc1 alishawahi kuongelea suala la ugomvi wake kakobe na tanesco, hauwezi kuamini kama kweli ni mwandishi wa television ya taifa, alikuwa mweupe yaani kama hajasomea..nadhani waandishi wetu wanahitaji kwenda shule vizuri...wasiendeshwe na chuki, wasiendeshwe na upepo wowote ule, kama hawatakuwa wanafanya hivyo, wataaibika tu.

  nakumbuka kuna kipindi fulani Jerry Muro alishawahi kumhoji injinia mmoja pale mnazimmoja jengo lilipobomoka, alimshambulia kiasi kwamba yule jamaa ndo alikuwa mhusika, kumbe aliyekuwa anahusika alikuwa mtu mwengine. mwishoni, akasema "aisee, unajua wananchi wanaposikia unavyoongea wanaweza kuchukua sheria mkononi"...akimaanisha matamshi ya yule injinia yangemfanya apigwe na wananchi kama alikuwa anahamasisha wananchi wafanye ivyo vile...nilikaa na mai waifu wangu, nikamwambia, JERI MURO HATAFIKA MBALI na uandishi wake wa habari..

  amekaa kidogo tu, akawa kama amelewa umaarufu, kuongozwa na speculation, alienda kumshambulia yule pastor kule bagamoyo na kuliaibisha Jina la Mungu na mambo chungu mzima...mwisho wake, he has been reduced to the gound...HUO NDO UANDISHI WA HABARI AMBAO HAUNA STRATEGY, hauna usomi, mtu anatafuta tu umaarufu, mtu anaendeshwa tu na chuki ,mtu anaendeshwa tu na vile anavyofikiri yeye na si vile hali halisi ilivyo na inavyotakiwa kuwa kwake yeye kama mwandishi wa habari...
   
 12. s

  sha Senior Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante sana mtumishi wa Mungu "mpeni sifa Yesu" watu wengi wamepotoka na wanapenda injili laini idanganyayo (Isaya 30:10 ) Na hawawezi hata kuthubutu kumsikiliza Askofu Kakobe,WANAMHUKUMU KWA KILE WASIKIACHO TUKWA WALIOSHINDWA VIWANGO, Mtumishi wa Bwana ambaye binafsi amedhamiria kwa dhati yote kuiona pepo, Watu wanakimbilia miujiza na uponyaji badala ya uzima wa milele na wakifika pale wanashindwa viwango, NAKUOMBA WEWE MWENYE SHAKA FIKA UJIFUNZE PALE VIWANGO VYA MBINGUNI, "duniani mnao manabii na mitume wawasikie hao vinginevyo hukumu ya jehanamu ya moto ni LAZIMA" je hivyo ni vitisho?????????????!!!!!
   
 13. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  waandishi wa habari wanatumika kama silaha ya kumshambulia mtu, na si kama watu wanaotakiwa kutupatia habari kwa kuangalia pande zote mbili. angalia kama hata hao hao tbc1 watakuwa walipanda daladala tu kwenda pale mwenge, wakamhoji kakobe kuhusiana na hilo...na kama angekataa kuhojiwa si wangesema kuwa "mwanamke huyu anasema hivi,lakini kakobe tulivyomhoji amekataa kuhojiwa"....etc, si wangeeleweka, sasa angalia uandishi wa habari wa kitz, mtu anachukua habari, hajui kama ni kweli, kwasababu anataka kumwadhibu mtu fulani kutokana na chuki zake, anairusha...bila hata kwenda kwa huyo mtu kumwuliza anasemaje kuhusu tuhuma hizo...angalieni mjifunze hata uandishi wa habari wa nchi za wenzetu tu..WAANDISHI WA HABARI MSIKUBALI KUCHUKULIWA KAMA SILAHA YA WATU KUWASHAMBULIWA WALE WASIOWAPENDA, fanyeni kazi yenu professionally jamani...jamii itawahukumu kutokana na matendo yenu...kwasababu tunaona,
   
 14. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  majibu yote haya utayapata ukipanda daladala ukaenda pale mwenge ukamwuliza kakobe. hauna hata haki ya kuongea hivi wakatu hatujamsikia kakobe akidefend himself. unaongea kwa chuki yako dhidi ya makanisa ya kipentecost, na post hii ndo msingi wake huo....kama mtu ni mungu mtu wa kwanza angekuwa papa kule vatican, na si kakobe....tusiende huko, turudi kwenye mada. unatakiwa kuokoka...!
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakuunga mkono kwa 40% japo hoja yako inaweza kuzua maswali mengi . Jiulize

  1 - huyu mama alikuwa na wadhifa gani ndani ya kanisa la kakobe?
  2- wakati anapewa wadhifa huo hakuwa na mume mbaye leo anaambiwa amwache?
  3 - What went wrong?
  Tatizo kuu lililopo ktk jumuiya ya wapentekoste hapa nchini ni kuwa wachungaji na watumishi wa Mungu wengi wamegeuka na kujifanya ni miungu watu badala ya kuwa watumishi wa Mungu wamegeuka kuwa watumishi wa makanisa(masinagogi yao tu).

  Kumbuka mtumishi (mtunzaji wa shamba) alimwambia bwana wake kuwa asiukate mti ataupalilia, kuupa mbolea na kuunyweshea maji ili uzae matunda mwaka unaofuata.

  Tatizo hawa wanaojiita watumishi wa Mungu theory hii hawaielewi. wanachofanya ni kuendekeza udikteta na kugeuza makanisa kuwa mali wao binafsi.
  Baba - mtume na nabii
  Mama - senior pastor!!!!!!!!
  Huoni kuwa hii ni issue inayoweza kuvua matatizo kama haya??????!!!!
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Inaonekana humfahamu kakobe hasa katika masuala ya uongozi wewe. Na kwa taarifa yako sina chuki yo yote na upentekoste kwani nami ni mpentekoste. tatizo ni kuwa watumishi wengi wapentekoste masuala ya uongozi na utawala ni sifuri.

  Sina haja ya kudiscuss kuhusu papa as I dont believe in it. I am highly opposite them.
   
 17. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Walikwenda kwa kakobe, wakaambiwa yuko bize na maombi!!, hapa busara ndogo tu ilimtuma asiseme sitaki kuhojiwa, nafikiri unaelewa!!. Ni kwa nini kakobe tu awe na maadui kila kona, Serikali, waandishi wa habari n.k?
  Ni kitu gani unachotaka kutuaminisha?. Kiweke wazi tafadhali!!
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  usiwashambulie waandishi wa habari bure. tatizo ni sisi wapentekoste wenyewe ambao hatujajenga misingi thabiti ya kushughulikia conflicts ndani ya makanisa.
  Kakobe mwenyewe ni expert wa kukimbilia waandishi wa habari, inawezekana ndiyo sababu huyo mama amekimbilia huko. angejenga msingi imara wa conflict resolution ndani kwa ndani hali hii ya kukimbilia kwa waandishi isingetokea.
   
 19. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hata mimi nashangaa, KOKOBE IS A PROBLEM TO HIS OWN ESTABLISHMENT. huwa ni mwepesi sana kuita waandishi wa hapari ikiwa anakuwa kinyume na wengine. Inapokuwa issue inamhusu yeye huwa anadai niko kwenye maombi.
   
 20. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Mada tuliyonayo ni kuokoka????
   
Loading...