Je, ni kweli ili mtu uendelee kibiashara ni lazima ufanye ushirikina?

Watu wengi ambao ni wafanyabiashara/wajasiriamali wamekua wakiusishwa/wakiamini kuwa ili kufanikiwa katika biashara itabidi ufanye ndumba kidogo ili mambo yaende sawa.

Leo naomba tupeane uzi juu ya ili kwamba ni je kuna ukweli wowote kwamba ili mtu afanikiwe yampasa kufanya ndumba au la...... Uwanja upo wazi tuwe wakweli ili tujue na wengine kama ndumba zinafaida tufanye...... MAWAZO YENU WAKUU.
Naona unatafuta excuse ya kujiingiza kwenye ushirikina
 
Watu wengi ambao ni wafanyabiashara/wajasiriamali wamekua wakiusishwa/wakiamini kuwa ili kufanikiwa katika biashara itabidi ufanye ndumba kidogo ili mambo yaende sawa.

Leo naomba tupeane uzi juu ya ili kwamba ni je kuna ukweli wowote kwamba ili mtu afanikiwe yampasa kufanya ndumba au la...... Uwanja upo wazi tuwe wakweli ili tujue na wengine kama ndumba zinafaida tufanye...... MAWAZO YENU WAKUU.
Swali"Je Ndumba au Ushirikina ni nini?" Ukiwa unafahamu maana yake weka hapa then utaelewa kwamba hata huu uzi wako nao ni ushirikina
 
ili uendelee kibiashara inabidi uchague upande wako kabla haujaanza.....kama ni kumtegemea Mungu basi kuwa na Mungu muda wote usichanganye mambo hasa uzinzi....na kama unafanya shirki basi egemea upande huo.....

wengi ambao hawafanikiwi katika biashara licha ya kumtegemea Mungu ni kutojua sheria za kufanikiwa kibiashara ukiwa upande wa Mungu, mambo kama kutoa zaka, sadaka ya shukrani, kuacha uzinzi....

ila uzinzi unaharibu sana biashara sana.....unaweza kuwa hausali wala nini ila uzinzi upo nao mbali utafanikiwa hata bila kuwa na imani kuuuubwa
Tofauti na kwenye biashara pia hata kwenye kazi za maofisini lazima uwe na upande, umenikumbusha kitu kikubwa sana kaka ndipo nilijua na kuelewa kuwa maisha ni fumbo kubwa sana.
 
Watu wengi ambao ni wafanyabiashara/wajasiriamali wamekua wakiusishwa/wakiamini kuwa ili kufanikiwa katika biashara itabidi ufanye ndumba kidogo ili mambo yaende sawa.

Leo naomba tupeane uzi juu ya ili kwamba ni je kuna ukweli wowote kwamba ili mtu afanikiwe yampasa kufanya ndumba au la...... Uwanja upo wazi tuwe wakweli ili tujue na wengine kama ndumba zinafaida tufanye...... MAWAZO YENU WAKUU.
Siyo kweli,bali ni kujiendekeza na tamaa za kijinga.

Mafanikio ya kweli yapo mbali na ushirikina na watu wanafanikiwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom