Je, ni kweli huyu ndiye yule aliyengojewa kukomboa wana wale?

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,049
24,427
Nauliza katika mji ule uliokuwa chini ya himaya ya utawala ule, wengi waliishi kwa taabu na karaha huku wakingojea mkombozi!
Kweli hayawi hayawi akaja Bwana mfalme ambaye hakudhaniwa kabisa na wana wa mji ule na kusema atahakikisha anawakomboa wana wa mji ule hasa watoto wa maskini kwa kuhakikisha wanapata elimu na ya juu kabisa kwa kuwapa yale yawapasayo watoto wale wa maskini.
Ni takribani mwaka mmoja umeisha mfalme akiwa anafanya kazi yake katika mji ule, raia wake wengi wamekuwa wakijipa matumaini kwa yale anayoyafanya...
Wanajiuliza kweli kwamba huyu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kuwakomboa..
Matarajio yao yamekuwa na sintofahamu nyingi!
Ewe mtukufu mfalme ni wewe uokoae kwa kutumbua majipu?
Naam yupo ajae kuokoa kwa maji na moto...
 
Nani alikudanganya kuwa mkombozi wa binadamu ni binadamu mwingine?

Mkombozi wako ni fikra zako.

Mkombozi wa wanadamu ni fikra zao.

Acha kukabidhi akili zako kwa binadamu mwingine. Mbaya zaidi, usijaribu hata kufikiria kukabidhi akili zako kwa wanasiasa.

Kama binadamu angekuwa mkombozi basi hata Mungu angemtuma binadamu lakini hakufanya hivyo bali alimtuma Yesu.

Tunaambiwa Yesu alikuwa mkombozi lakini hakuwa binadamu bali alikuwa ni Mungu katika umbo la binadamu.
 
Hahaa, nani huyo atakayekuja kuokoa kwa maji na moto?
Kweli umevurugwa..
Anyway mfalme wetu amekuwa mtemi..
 
Alidhani kuomba ile mizimu ya babu yake wiki nzima kule chato ndyo angeweza kuongoza nchi. Mwambie nchi haiongozwi kwa mizimu ya babu yake.
 
Nani alikudanganya kuwa mkombozi wa binadamu ni binadamu mwingine?

Mkombozi wako ni fikra zako.

Mkombozi wa wanadamu ni fikra zao.

Acha kukabidhi akili zako kwa binadamu mwingine. Mbaya zaidi, usijaribu hata kufikiria kukabidhi akili zako kwa wanasiasa.

Kama binadamu angekuwa mkombozi basi hata Mungu angemtuma binadamu lakini hakufanya hivyo bali alimtuma Yesu.

Tunaambiwa Yesu alikuwa mkombozi lakini hakuwa binadamu bali alikuwa ni Mungu katika umbo la binadamu.
Sio kwel kijana hapo chin hukumalizia vizur
 
Duuuh hii nayo kichekesho cha karne Yesu hakuwa binaadamu ? Duuuh hatari hizi dini za watu ni balaa sana
 
Nani alikudanganya kuwa mkombozi wa binadamu ni binadamu mwingine?

Mkombozi wako ni fikra zako.

Mkombozi wa wanadamu ni fikra zao.

Acha kukabidhi akili zako kwa binadamu mwingine. Mbaya zaidi, usijaribu hata kufikiria kukabidhi akili zako kwa wanasiasa.

Kama binadamu angekuwa mkombozi basi hata Mungu angemtuma binadamu lakini hakufanya hivyo bali alimtuma Yesu.

Tunaambiwa Yesu alikuwa mkombozi lakini hakuwa binadamu bali alikuwa ni Mungu katika umbo la binadamu.
Fikra mbele ya mfalme mwenye mrengo mmoja yafaa nini?
Ni kweli fikra huzaa mapinduzi na dhana ya mapinduzi ni mabadiliko!
Zile fikra pevuka zimezikwa kaburini, mfalme hataki kuzisikia mbele ya kadamnasi..
 
Mtabiri maarufu aitwaye Yusuf Makamba alitabiri hivi, "Bwana huyu aliyepita aliwabatiza kwa maji, lakini Bwana huyu ajaye atawabatiza kwa moto!" Mwaonaje utabiri huu??
Naam yupo ajaye atakayebatiza kwa vyote, maji na moto.
 
Kawaambie:
Watoto wanasoma bure;
Watumishi hewa wameondolewa;
Wauza unga wakubwa wanakamatwa kama kuku;
Safari za viongozi kupishana angani kwenda nje zimekoma;
Vyanzo vya kodi vimeongezeka;
Mapato ya kila mwezi yameongezeka;
Viongozi wanaotaka kumentain status quo wanatumbuliwa;
Bei ya mazao ya wakulima imeongezeka mara nne;
Nk. Nk. Nk.
 
Nauliza katika mji ule uliokuwa chini ya himaya ya utawala ule, wengi waliishi kwa taabu na karaha huku wakingojea mkombozi!
Kweli hayawi hayawi akaja Bwana mfalme ambaye hakudhaniwa kabisa na wana wa mji ule na kusema atahakikisha anawakomboa wana wa mji ule hasa watoto wa maskini kwa kuhakikisha wanapata elimu na ya juu kabisa kwa kuwapa yale yawapasayo watoto wale wa maskini.
Ni takribani mwaka mmoja umeisha mfalme akiwa anafanya kazi yake katika mji ule, raia wake wengi wamekuwa wakijipa matumaini kwa yale anayoyafanya...
Wanajiuliza kweli kwamba huyu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kuwakomboa..
Matarajio yao yamekuwa na sintofahamu nyingi!
Ewe mtukufu mfalme ni wewe uokoae kwa kutumbua majipu?
Naam yupo ajae kuokoa kwa maji na moto...
UNAMUONGELEA HUYUU AU..
3c593d7c278e6ffc77d294b27660a0ca.jpg
 
Kawaambie:
Watoto wanasoma bure;
Watumishi hewa wameondolewa;
Wauza unga wakubwa wanakamatwa kama kuku;
Safari za viongozi kupishana angani kwenda nje zimekoma;
Vyanzo vya kodi vimeongezeka;
Mapato ya kila mwezi yameongezeka;
Viongozi wanaotaka kumentain status quo wanatumbuliwa;
Bei ya mazao ya wakulima imeongezeka mara nne;
Nk. Nk. Nk.
Usiandike kwa mihemko, toa uthibitisho wa bei ya mazao manne ambayo bei yake imeongezeka mara nne, usilete habari za korosho hapa.
Vipi kuhusu ajira, wapo vijana batch mbili mfano ni waalimu wa sanaa wapo mtaani hawajui hatma yao, hawa wa sayansi nao ni kama haieleweki tu, hao ni sample kuna vijana lukuki mtaani na shahada zao hawajui wafanye nini..
Elimu yenyewe ndio hii haimtune mtu kujiajiri, wanasiasa wanasema vijana wajiajiri, wakati wao hawajajiajiri!
Elimu bure bila kuwa na ubora ina umuhimu gani?
Vyanzo vya mapato vilivyoongezeka ni vipi, hebu viweke wazi tuvijue..
Weka pia data ni wauza unga wangapi waliokamatwa kama kuku, na ni akina nani hao!
Hao watumishi hewa walioondolewa, imekuaje maslahi ya watumishi waliobaki hayaboreshwi, na pia malipo ya mishahara yamezidi kile kiwango cha wakati ambao watumishi hewa walikwepo?
 
Mtabiri maarufu aitwaye Yusuf Makamba alitabiri hivi, "Bwana huyu aliyepita aliwabatiza kwa maji, lakini Bwana huyu ajaye atawabatiza kwa moto!" Mwaonaje utabiri huu??
Aisee umenikumbusha mbali sana...kweli bwana sasa waTz wanapata ubatizo kwa moto.
 
Nionavyo mimi mfalme yupo vizuri sana. Huyu mfalme kwa sasa yupo busy shambani. Ameamua kupanda mbegu karibu zote shambani kwake na ndiyo maana watoto wake wanalia lia njaa. Watoto hawa walizoea kupata milo 6 kwa siku na sasa imebaki milo 2 tu.
Lakini watoto hawa wanaolia sasa watakuja kufurahi baada ya mavuno. Kumbuka kuwa hawa watoto akili yao bado ni nyembamba sana, wanadhani mtu anaweza kulima shamba siku hiyo hiyo na kuvuna siku hiyo hiyo. Enyi watoto, mfalme siyo kwamba amewasahau, bado anawakumbuka.
Machozi mnayotoa sasa kwa uchungu, baada ya mavuno mtatoa machozi ya furaha. Pia kumbukeni kuwa, shamba hili lilikuwa limeharibiwa vibaya sana na mafuriko. Kwa hiyo mfalme anachokifanya ni kulirutubisha kwanza ndipo lianze kutoa mavuno. NAMKUBALI SANA MFALME, NAOMBA MUNGU AMLINDE KWA MKONO WAKE WENYE NGUVU DHIDI YA MAADUI ZAKE.
 
Kawaambie:
Watoto wanasoma bure;
Watumishi hewa wameondolewa;
Wauza unga wakubwa wanakamatwa kama kuku;
Safari za viongozi kupishana angani kwenda nje zimekoma;
Vyanzo vya kodi vimeongezeka;
Mapato ya kila mwezi yameongezeka;
Viongozi wanaotaka kumentain status quo wanatumbuliwa;
Bei ya mazao ya wakulima imeongezeka mara nne;
Nk. Nk. Nk.
wamakonde mnamatatizo hio bei ya korosho imewavua akili kabisa.
Ikija kupungua ndio mtajua forces of demand and supply ni kitu gani katika biashara.
bei ikipanda wanasiasa wanawadanganya wao wamepandisha na nyie mnavimba vichwa.
 
Back
Top Bottom