Je, ni kweli Halima Mdee ametatua migogoro ya ardhi kwenye jimbo la Kawe?

kudamademede

Member
Jan 1, 2020
62
241
JE, NI KWELI HALIMA MDEE AMETATUA MIGOGORO YA ARDHI KWENYE JIMBO LA KAWE?

Kwenye karatasi zake tano za utekelezaji wa Ilani jimbo la Kawe, kwenye ukurasa wa pili, Halima Mdee amesema ametatua migogoro ya Ardhi.

Kwenye ukurasa wake wa pili wa utekelezaji, Mdee anasema ametatua mgogoro wa ardhi Sala sala kwa baba Yaro Kata ya Wazo, lakini mwisho anasema atalisimamia jambo hili mpaka mwisho. Hii ina maana hili jambo halijaisha bado. Je ameshindwa kulimaliza ndani ya miaka 10? Kama ameshindwa ndani ya miaka 10, miaka 5 mingine ya nini? Si ya kupoteza muda tu? Tafakari.

Mdee anasema tatizo la ardhi kwa shule ya sekondari ya Benako kata ya Wazo mchakato unaendelea wizara ya Ardhi. Ni mchakato gani huu usioisha kwa miaka 10? Mchakato utaendelea hadi lini? Kwa utendaji huu, kama kwa bahati mbaya akichaguliwa, anaweza kurudi tena baada ya miaka 15 na kusema mchakato bado unaendelea. Huyu mtu ambaye kwa miaka 10 hajaweza kutatua mgogoro wa ardhi kwenye kata, anaishia tu kusema mchakato unaendelea, si wa kumuamini tena. Nina uhakika ukimuuliza mchakato upo kwa nani? Na tatizo ni nini hasa, hana majibu. Mdee ameshindwa kutatua migogoro ya ardhi jimbo la Kawe, haina haja ya kumuamini tena, tumemuamini kwa miaka 10 inatosha.

Hajaishia hapo. Ameendelea kusema eti “ _sehemu kubwa ya mgogoro wa ardhi wa Mabwepande umekwisha. Yapo maeneo machache ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi._” Huu ni ubabaishaji. Haya maeneo yanafanyiwa kazi mpaka lini? Tatizo liko wapi? Wahusika ni akina nani? Kwa jinsi Mdee anavyotoa taarifa ya utekelezaji inaonyesha wazi hata hajui kinachoendela. Ni bla bla tu, wala hajafuatilia. Mtu wa aina hii haaminiki. Kama ameshindwa kumaliza migogoro kwa miaka 10, atawezaje ndani ya miaka 5? Lakini pia kama ameshindwa ndani ya miaka 10, watu wa Kawe mnahitaji kumpima tena ili aonekane hawezi? Ebu tafakari.

Bado anaendea kusema mgogoro wa pale Boko kwa Somji eti hatua za urasimishaji zinaendelea? Kwa nini hazifikii mwisho? Kama hazijaisha ndani ya miaka 10, anahitaji muda mwingine wa kupoteza?

Kwa uhalisia, migogoro yote ya ardhi anayosema ametatua katika jimbo la Kawe hakuna hata mmoja ulioisha, mara aseme urasimishaji unaendea, mara mazungumzo yanaendelea, mara mchakato unaendelea, visingizio kibao, longo longo zisizo isha. Kawe tunahitaji mtu wa namna hii tena? Kwa viashria hivi, Mdee hana uthubutu wa kutatua matatizo ya ardhi katika jimbo la Kawe. Hana uthubutu kabisa. Kama angekuwa na uthubutu na nia thabiti ya kutatua migogoro hii, ndani ya miaka 10 ya uongozi wake ingekuwa imeisha.

Unaweza kuwaza mtu ambaye kwa miaka 10 ameshindwa kutoa suluhu za changamoto za wananchi, anahitaji miaka mingapi kufanya hivyo? Kama ameshindwa kwa miaka 10, miaka 5 aongezewe ya nini? Watu wa Kawe tutadanganywa mpaka lini?

Kwa upande mwingine, mgombea ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, askofu Dr Josephat Gwajima hata kabla ya kuchaguliwa ameanza kutoa suluhu kwa baadhi ya kero za ardhi katika jimbo la Kawe.

• Kule Bunju katika eneo la Chasimba, wananchi walikuwa wanalipa 8000 kwa kila meta ya mraba katika ardhi yao wenyewe. Mdee hii kero hakuiona. Gwajima ameiona na amepita katika mamlaka husika na wananchi watakuwa wanalipa 4000 kwa kila meta ya mraba sawa sawa na kipato chao.

• Mdee hajabaini tatizo la wananchi wa Mbweni ambao wanaitwa wavamizi. Gwajima amebaini tatizo lililopo na kuahidi kulimaliza.

• Haitoshi, Gwajima kabla ya kuwa Mbunge amewasaidia wananchi kupata maji, nyumba 252 kule Salasala. Je itakuwaje akiwa mbunge?

Waswahili wanasema, nyota njema huonekana asubuhi. Gwajima anaonekana kuwa na kasi katika kutatua changamoto za wananchi. Itakuwa busara kumpa nafasi Gwajima walau kwa miaka mitano kuliko kumuongezea Mdee ambaye ameishatumia miaka 10, miaka mingine mitano, na bado kuna changamoto kibao.

Wananchi wa Kawe ni wakati wa kuamua sasa. Mojawapo ya kazi ya mbunge ni kuishawishi serikali kuleta maendeleo katika jimbo lake. Kwa migogoro hii ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 katika jimbo la Kawe, Mdee anaonyesha wazi kabisa ameshindwa kuzitatua, ameshindwa kuishawishi serikali kutatua hizi kero, hana uthubutu wa kuzitatua, na kumpa nafasi tena ya kuwa mbunge itakuwa ni kupoteza muda na kupoteza nafasi ya kupata maendeleo katika jimbo la Kawe. Wanakawe tufanye maamuzi sahihi.

Selemani Hamidu
Kawe mikoroshini
23/09/2020
 
Kaka nimekubaliana na wewe asilimia zote Gwajima ni mtu sahihi kwa sasa kuwa Mbunge wa Kawe Halima tumpumzishe kwanza.
Tuna uhakika Gwajima ataivusha Kawe
 
Hivi mfuko wa Jimbo kwa Mwaka Ni kiasi gani kinatengwa maana Halima Mdee kunatetesi ametumia kwa manufaa take binafsi
 
Halima ameshapigwa kawe mapema sana maana hakuna alichofanya kwa wananchi huku kila sehemu shida tupu hawataki kumuona
 
Toa kwanza boriti kwenye jicho ndio umsaidie mwingine kutoa kibanzi kwenye jicho lake.

Ikiwa wananchi wote tungewapima wapunge wote kwa huu mwendo bila kujali vyama, ingekua jambo la heri na manufaa.

1. Mgombea urais mwenyewe anatuambia kuna mambo bado yapo kwenye mchakato, hayajakamilika, na yeye asipewe mingine mitano?

2. Wabunge wote nao wanasema bado mambo yapo kwenye mchakato, hicho kikitumika kama kigezo unachotaka kukitumia Kawe, iwe hivyo kwa wabunge wote bila kujali vyama.

3. Mimi kama mdau wa Kawe nimepata hati kwa utaratibu wa serikali kwa gharama isiyozidi 1M, hauoni huo ni moja ya maeneo yaliyofanyiwa kazi? Bado maeneo ya Nyakadangwe utoaji wa hati na kurasimisha unaendelea. Hayo haujayaona?

Kwa sie wananchi imefika majali hatuangalii sana chama gani kipo madarakani, tunachotaka ni maendeleo, hayo mengine ni ajira za watu binafsi.

CCM sawa, najua itachochea maendeleo japo haitakiwi kuwa hivyo, lakini Gwajima hapana.
 
Halima huku kabaki kujisifia ana sauti ya kukoroma kama spika iliyopasuka base anaomba kura kwa sababu ana sauti ya kukwaruza akiuliza kwa nini ujafanya chochote anakuwa mkali safari hii anapigwa spana.
 
lakini mwisho anasema atalisimamia jambo hili mpaka mwisho. Hii ina maana hili jambo halijaisha bado. Je ameshindwa kulimaliza ndani ya miaka 10?
Unazungumzia miaka 10 ? Mbona wengine wa ccm wamebaki na migogoro ya ardhi inafukuta kwa zaidi ya miaka 20 sasa ?
 
Halima huku kabaki kujisifia ana sauti ya kukoroma kama spika iliyopasuka base anaomba kura kwa sababu ana sauti ya kukwaruza akiuliza kwa nini ujafanya chochote anakuwa mkali safari hii anapigwa spana.
Spana za MATAGA bwana . . . yaani ujinga ujinga tu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom