Je, ni kweli Freeman Mbowe yupo Kazini?

Atukuzwe Mungu wetu Aliye Mkuu na Mtakatifu Sana.

Usiku wa jana nilikua ndani ya viunga vya Kariakoo, sehemu muhimu kibiashara ndani ya jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla.. Nitaleta Mrejesho wa kile kilicho nipeleka pale

Kwa Sasa nataka kufahamishwa/kujuzwa Jambo hili ambalo nililinyaka/kulipata nikiwa pale Kariakoo.

Yalikua majira ya saa 0220 usiku nikiwa katika ile kazi iliyonipeleka pale mara baada ya kuusoma Uzi wa Mkuu Mshana Jr nikiwa mahali pale kulikuwa na kikundi fulani cha wazee na vijana wakipata kinywaji cha kahawa.. kundi lile lilikuwa limechangamka kwa stori za hapa na pale, wakati Mimi nasogea pale nilikuta mada inayomuhusu Mh. Mbowe.

Wanasema ukienda rumi fanya kama wafanyavyo warumi, basi kwa wepesi wa kanuni hii na Mimi nikaagiza kahawa (Japo si mtumiaji wa kinywaji hiki) na kisha nikatega sikio langu kwa umakini mkubwa.

Mzee mmoja ambaye bila shaka anaheshimika na kuogopeka miongoni wa wale wengine alikuwa akielezea sakata la Mh. Mbowe kuwa hii kesi yake na kufungwa kwake ni Danganya toto ili kuficha na kupoteza mambo mengine, akaulizwa kivipi kadiri ya maelezo ya yule Mzee ni kuwa Mh.Mbowe ni mmoja wa watu wa ile idara nyeti yenye jukumu la kuzingatis usalama wa nchi unakuwa katika ubora wake.

"Yule, yupo kazini pale na analipwa kama maafisa wengine wanavyolipwa posho zao za siku wakiwa katika misheni".. Haya yalikuwa maneno ya yule Mzee, kiukweli niliduwaa na kubaki na maulizo mengi, na ndio maana nikaleta bandiko hili ili wale wataalamu watusaidie kulichambua na kulinyumbua kinyumbufu.

Umakini wangu mahali pale ulipotezwa ghafla mara baada ya kundi lile kuhamia kwenye stori za timu za Kariakoo, nikaamua kuachana na lile kundi ili nitimize majukumu yangu ya msingi.

Katika yote, wananchi wenye mapenzi mema na nchi yetu kwa usalama na taswira nzuri ya nchi Tumuombe Mungu sakata hili limalizike kwa amani.

Ee Mungu Uturehemu.
Mkuu hii, inafanana na hadithi a Beans Mrema, ambaye uchaguzi wa mwaka 1995, Gari alilokua anafanyia kampeni kuzimwa na kusukumwa na wananchi. Wananchi walibeba Imani kubwa mioyoni mwao lakini Mrema mwishoni aliwaumiza na kupoteza imani kwa wananchi.
Unakisema kuhusu Mh. Mbowe inawezekana ikawa kweli au Ni uzushi. Ngoja tuwe na subira tunaweza kupata somo jipya
 
Chadema iliundwa kama TAKWA la nchi za Magharibi kutaka Multipartism, hivyo Mchonga akamuita rafiki yake Nzee Ntei aunde chama, so cdm ni ccm B, naye akamkabidhi Uhuru mboe aliyemwaminifu kwa sisiem,
Uhuru ni wakala mtiifu, aliyekazini
Unataka kudanganya watu kwamba successor wa Mzee Mtei ni Mbowe?

Jinga kabisa, na Bob Makani alikuwa ni nani?
 
Njia nyingine mnakuja nayo Ili jamii isimuamini but Moyo wake unaongea kwa sauti kuliko mdomo na mwili wake,kwani ukiwa mtu wa system unakuwa huna jema unaloweza kulifanya kwa nchi yako? Je madai ya Mbowe kwa nchi ya Tanzania ni ya ukweli au sio ya ukweli?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom