Je, ni kweli Bush kanunua kiwanja Kigamboni?.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ni kweli Bush kanunua kiwanja Kigamboni?..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkandara, Mar 12, 2009.

 1. M

  Mkandara Verified User

  #1
  Mar 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana Jamii,
  Kuna habari huku majuu zinasambaa sana kwamba Bush (Kichaka) amenunua sehemu kubwa sana Kigambioni na anataka kuwekesha (uwekezaji) sijui kitu gani..Ndio maana ziara yake Bongo ilichukua muda mrefu sana na inasemekana kisha kuja tena Bongo baada ya kukabidhi madaraka kwa Obama ktk kumalizia malizia taratibu za umiliki..
  Je, maneno haya kweli?!? au ndio yale ya kambi ya kijeshi ya Marekani baada ya Kenya kuwatolea nje!
  Kale ka - nzi kako wapi?..
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Aliyekulitea hizi tetesi ulitakiwa umuulize iwapo anajua kuwa ardhi ya Tanzania ni mali ya serikali.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Aliyekulitea hizi tetesi ulitakiwa umuulize iwapo anajua kuwa ardhi ya Tanzania ni mali ya serikali

  kama unalijua hili kawaulize BARRICK imepewa miaka mingapi!!!???tema mate chini
  just for info;kweli amenuunua bush na fmailia yake sehemu kubwa tu na watanzania wengi tumeathirika;mi ni mmoja wapo;nilikuwa na kiwanja viwili huko kigamboni kimoja nikaambiwa ntafidiwa kuna ujenzi wa nyumba za wananchi na majengo mengi tu;tukauliza wakati mkigawa hamkujua wakatumbia hii ni georgr bush foundation
  wacha hilo nilikuwa nimeanza kalinta wamesimamisha ujenzi wote kuna watu walikuwa wanamalizia kujenga mahoteli;wanaambiwa ati wasimamishe;;;;;
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Pointi yako ssielewi hapa.

  Kama sheria imebadilika ningekuwa na la kuongelea, for far sioni hoja ya kujadili.

  BTW,pole kwa kupoteza ardhi (ambayo hata hivyo ni mali ya waTZ wote, serikali ikiwa guarantor wake).

  Shukran.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mkandara,

  Kweli Bush ataenda Tanzania bila ya media yoyote ya Tanzania kujua?

  Inawezekana amenunua ardhi lakini sidhani kama ameenda TZ kimya kimya.

  Pia kama ni kweli amenunua ardhi TZ ni jambo zuri. Hata kama simpendi Bush lakini jambo lolote ambalo linaweza kuwaongezea mlo Watanzania wenzangu hata kama ni wachache mimi nitaliunga mkono.

  Kitendo cha mtu kama Bush kukaaa TZ hata kwa wiki moja tayari kuna Watanzania kibao wanaweza kufaidika.
   
 6. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimepata kusoma sehemu wanasema ana hisa au ni mtu muhimu katka likampuni la barrick.

  tunalitambua likampuni hilo kama limekuja kuwekeza katka sekta ya madini. kama kweli atakuja nunua eneo huko kigamboni kwa shughuli zake basi anakuja kuwekeza kama alivyowekeza awali hapa tz kupitia barrick.

  lakin kuna taarifa kuwa hatupati chochote cha maana kwenye uwekezaj wa kampun la barrick. ni kama wanajichimbia madin na kuondoka nayo bure. udhibit mdogo, udanganyifu mwingi na hatuwez kuacha kuwalaumu barrick kwa hilo pia (na wamiliki wake). na mengine mengi ya ovyo yanaripotiwa kuhusu hilo li barrick.

  sasa shareholder wa hilo likampun lisilo taka tufaidike na mawe yetu anakuja tena 'kuwekeza'. unafikiri amebadilika? unafikir tutafaidika na uwekezaj huo safar hii? kwanin haikuwezekana kule kwenye madin iwezekane kigambon?
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Matatizo ya Barrick wa kuwalaumu ni viongozi wetu ambao wameingia mikataba mibovu kwa faida zao binafsi.

  Pia mtu kuwa na share kwenye kampuni fulani haina maana anakubaliana na maamuzi yote ya kampuni hiyo. Shareholders walio wengi hawana sauti kabisa kwenye managements za kampuni hizo zaidi ya kusubiri malipo ya investment zao.

  Watanzania inabidi ifike mahali tuache kuwa against uwekezaji na badala yake tuwe wajanja wa kutumia hizo opportunities kwa faida ya nchi na wananchi wetu.

  Tanzania itaendelea pale ambapo sehemu kubwa ya raia wetu watakuwa na kazi, hili haliwezi kufanyika kama hakutakuwa na investments mbalimbali zinazofanywa na wenyeji pamoja na wageni. Muhimu tu ni kuhakikisha Tanzania kama nchi inafaidika kutokana na hizi investments na sio sasa ambapo faida kwa wananchi ni ndogo sana.
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Wewe Sweetbaby,
  Taratibu....we hebu ongea vizuri hapa mana nami nina ka-sehemu pale. Mbona nilisikia kwenye press conf waziri akitangaza hamna kitu kama hicho?????
  Unasema kweli umesimamishiwa ujenzi? Halafu ni maeneo gani hayo?? Pse chonde chonde si unajua maisha yenyewe mpaka ununu ka plot ni kudunduliza wasije wajanja wakaninyanyanya mimi nibaki patupu maana hata title sina. msiniulize kwa nini sija!
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli Bush kanunua ardhi Kigamboni basi ni baraka kwa wenye ardhi na TZ kwani kipato kitaongezeka ilimradi kusiwe na ubabaishaji na udanganyifu.
   
 10. s

  skasuku Senior Member

  #10
  Mar 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mbona hizi habari ni kama za redio mbao.

  Leteni habari zenye uhakika. Wewe Mkandara, hizo data umezipata wapi. Lete source.
   
 11. C

  Chuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Eneo la Kigamboni limewekwa ready kwa wawekezaji..ni mipango Mipya ya Miji. Even GOT imechukua viwanja vingi kwajili ya kutengeneza nyumba kama za Osterbay/Msasani style...

  So Kama unae muwekezaji basi mlete nyumbani...wanatakiwa serious investors kama anavyosema JK, sio mtu akae na viwanja akisubiri kuja kuwalangua watz.

  Mradi huu hautahusu viwanja 20,000 vilivyopimwa...so zoezi nafikiri litaanza upya la Tathmini, sasa wadau wa GOT wapo busy kutengeneza PLAN, then hao wawekezaji waje...so inawezekana Bush Foundation wameonesha interest ya kuwekeza...na Wengine wapo tayari kuwekeza...wanakaribishwa..!!!

  Ila Angalizo..watu wa TIC wamekuwa moja wapo wa vikwazwo vya uwekezaji...wawekezaji wakija wao wanataka kitu kidogo..Huwezi tegemea nchi za nje kama zitakuja kuwekeza, otherwise tutawapata akina Richmond kuja kuwekeza...

  Kwa watu waliotembelea Dubai au wanampango wa kutembelea Dubai wafike Dragon Mall...Hilo Mall la wachina watupu...na hio Serikali ya China ime-invest sio watu binafsi....then Gov ya China imewapa wananchi wake waendeshe...sie badala kuwakaribisha serious investor tunawakaribisha machinga kuja kuuza maua k/koo...AKILI zetu zimejaa Makohozi...(samahani wadau inakasirisha)
   
 12. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shida ni kama sisi ni wajanja na tumestaarabika kufikia hapo
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Mar 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mtanzania,
  Mkuu kwanza heshima mbele..
  Hizi ni habari za tetesi nilizozipata toka kijiweni hapa na ndio maana nimetaka kuuliza wana JF kama wana taarifa hizi..
  Kuhusuiana na kuja kwa Bush kimya kimya mkuu wangu hilo linawezekana kwani hata Jimmy Carter alipomaliza urais wake alikuja TZ kimya kimya na ardhi ambayo alijishughulisha na kilimo cha ngano.. hadi leo hii navyozungumza sijui eneo alochukua wala huo mradi umemsaidia nini Tanzania!..Mbali na tetesi nyingine kuwa Carter alikuwa na foundation iliyohusiana na Utalii wa kupanda milima..
  Miaka imekwenda, Tanzania kubwa na siwezi kufuatilia habari kama hizi kama vile ndio maisha yangu..kuhusiana na Barricks mkuu wangu mbali na viongozi wetu hawa jamaa wanafahamika dunia nzima kwa Unyonyaji...Makosa yameanza pale tu tulipowakaribisha wao tukifikiria kwamba ni Wawekezaji..Hili neno wawekezaji, linatumika vibaya sana kwani tunaishi kama dangulo ambalo fedha ndio inapewa thamani kuliko utu wetu..
  Sasa nachotaka mimi kuelewa hapo Kigamboni kuna kitu gani ambacho Bush anaweza kuwekeza kiasi kwamba wananchi waporwe ardhi na kumpa Bush ambaye kiutaalam hana expertise nje ya Urais wake... hana elimu zaidi ya kushinda mtihani akiwa mwanachama wa Skull..Hata kusimamia visima vya mafuta vya baba yake vilimshinda..Nakuomba tazama sinema inayoitwa W...Utamfahamu vizuri Bush.. ni Kabuntas!..
   
 14. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kwa akili za viongozi wetu linawezekana hilo kwani mnajuwa Mabalozi wangapi wamegemewa Ardhi hapa TANZANIA kama ni bahashishi yao wakiwa tz au wakimaliza muda wao serekali inategemea mabalozi hao watakuwa wakipigia debe viongozi hao kwa mfano balozi yule mweusi wa kimarekani aliyemaliza muda wake kabla ya huyu mweupe inasadikiwa amemiliki Ardhi sehemu moja ya hapa TZ pia inasemekana amekuwa na uhusiana wa kimapenzi na mtoto wakike miongoni mwa Marais walikuwa Madarakani hivi sasa kwa hayo basi inawezekana Bushi kuwa ameshamegewa sehemu yake
   
 15. L

  Lugaon Member

  #15
  Mar 12, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii hi story tu mbona hamna ushahidi?
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ..nakubaliana na kupingana na wewe!!Ni kweli kwamba unaweza kuwa na share kwenye kampuni na usiwe na sauti kwenye maamuzi, lakini ukweli unabaki kuwa uendeshaji wa kampuni ni lazima uwe unaendana na misingi ambayo unaisimamia, labda kama lengo lako ni dividend peke yake! Hata hivyo nadhani kuna organization ilipull out of Barick kwa kupinga jinsi hao jamaa walivyohandle mambo ya Bulyanhulu! Kama Bush ni mmoja wa shareholders ni wazi anakubaliana nao otherwise angeweza kuinvest elsewhere ambako anadhani biashara inafanywa in a fair way. Bush ni mtu mwenye personal agenda siku zote, na kama kawaida yetu huwa hatutafakari mambo tunajitumbukiza tu kwenye makubaliano hata kama si ya faida kwa watu wetu, bali ya faida kwa urafiki wa JK na Bush! Ukweli kwamba wananchi wengi wanaweza kufaidika kwa investment hauwezi kupingwa, bado hatujui ni investment ya aina gani ni repulcation yake kwa jamii, kama haiwezi kutuweka kwenye win-win situation hatuna haja ya kuruhusu ujio wake in the first place!!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Mar 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lugaon,
  Mkuu hata ushahidi wa kwamba wewe una kiwanja TZ sina, lakini haina maana huna ama unacho..hizi ni tetesi! kama wewe unajua lolote kwa uhakika tumwagie mkuu.
   
 18. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi nia kiwanja kigamboni lakini sijaambiwa kitu na last time went there watu wanaendelea na ujenzi kama kawaida, mimi nipo tuangoma perhaps ni somewhere else lakini nafikiri si habari za uhakika
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Pointi yako ssielewi hapa.

  Kama sheria imebadilika ningekuwa na la kuongelea, for far sioni hoja ya kujadili.

  BTW,pole kwa kupoteza ardhi (ambayo hata hivyo ni mali ya waTZ wote, serikali ikiwa guarantor wake).

  Shukran

  Itakuwa ngumu kuielewa kama umeshindwa kuelewa na kujibu mada halisi#
  ciao
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Shapu
  Shapu is a Citizen of the World
  Senior Member Join Date: Thu Jan 2008
  Location: Citizen of the World
  Posts: 117
  Rep Power: 22

  Thanks: 217
  Thanked 38 Times in 30 Posts
  Credits: 4,150

  re: Je, ni kweli Bush kanunua kiwanja Kigamboni?..

  --------------------------------------------------------------------------------

  Quote: sweetbaby
  Aliyekulitea hizi tetesi ulitakiwa umuulize iwapo anajua kuwa ardhi ya Tanzania ni mali ya serikali

  kama unalijua hili kawaulize BARRICK imepewa miaka mingapi!!!???tema mate chini
  just for info;kweli amenuunua bush na fmailia yake sehemu kubwa tu na watanzania wengi tumeathirika;mi ni mmoja wapo;nilikuwa na kiwanja viwili huko kigamboni kimoja nikaambiwa ntafidiwa kuna ujenzi wa nyumba za wananchi na majengo mengi tu;tukauliza wakati mkigawa hamkujua wakatumbia hii ni georgr bush foundation
  wacha hilo nilikuwa nimeanza kalinta wamesimamisha ujenzi wote kuna watu walikuwa wanamalizia kujenga mahoteli;wanaambiwa ati wasimamishe;;;;;

  Wewe Sweetbaby,
  Taratibu....we hebu ongea vizuri hapa mana nami nina ka-sehemu pale. Mbona nilisikia kwenye press conf waziri akitangaza hamna kitu kama hicho?????
  Unasema kweli umesimamishiwa ujenzi? Halafu ni maeneo gani hayo?? Pse chonde chonde si unajua maisha yenyewe mpaka ununu ka plot ni kudunduliza wasije wajanja wakaninyanyanya mimi nibaki patupu maana hata title sina. msiniulize kwa nini sija!

  Sharp;
  Mkuu hii ni kweli na halisi;tuko wengi tumeambiwa tusiendele na ujenzi ndugu yangu
  huyu waziri anapiga siasa nenda wizarani upate ukweli halisi
   
Loading...