Je, ni kweli Bureau de Change zinahamisha pesa ya Tanzania kwenda nje?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Nimekuwa mteja wa kubadili pesa mara kwa mara hasa wakati nataka kwenda nje kikazi au hata kutembele jamaa na marafiki.

Awali sikuwa najua kwamba hizi Bureau de Change ni mahsusi kwa ajili ya kutorosha pesa zetu kwenda nje. Lakini kuna siku baada ya kupata fununu hizi nilikuwa makini kidogo kutaka kujua kama ni kweli kuna mchezo mchafu unao fanyika wakati mteja anapofika mahali hapo kwa lengo la kubadilisha pesa. Kinachofanyika ni kutoa receipt ambayo si halisi kwa ajili ya wakaguzi wa TRA.

Nilikuja kubaini hili baada ya kuona jamaa wananipatia receipt ambayo ni tofauti na receipt aliyopewa mteja aliyetangulia kwa lengo hilo hilo. Kilichofanyika ni kwamba wale wahindi walitazamana usoni kisha wakakubaliana jambo fulani kisha wakaleta kijitabu kingine cha receipt na kile cha awali kikawekwa chini ya counter na nikahudumiwa na kutoka wakati wote hao jamaa wakikonyezana mimi nilikuwa najifanya kusoma prices za kubadilisha fedha.

Kwa hiyo nikaona nitoe haya machache kwa wana JF ili mwenye mchango zaidi wa haya niliyoyachokonoa atupatie mwanga zaidi kwani naamini mchango wa wana JF ni suluhisho tosha katika harakati za kukabiliana na ubadhirifu wa uchumi.

Nawasilisha.
 
Kwani wakati wa kupanda ndege unakaguliwa kujua unaondoka na kiasi gani, huyo uliyemuona labda alikuwa anakwenda kuomba viza, labda walimsaidia hiyo risiti iliakaonyeshe ubalozini.

Nakumbuka kima cha juu ambacho kisheria mtu anaruhusiwa kununua na kuondoka nazo ni us dola 10,000. au sawa na hicho kwa currency nyingine
 
Wana JF, kukumbatia soko huria kumekuwa na madhira makubwa sana kwa uchumi na maisha ya Watanzania. tangu awamu ya pili kukubali soko huria na kuondoa udhibiti wa fedha za kigeni kumeibuka maduka mengi ya kubadilishia fedha aka Burea de change. Ukitaka kuuza pesa ya kigeni kama vile USD au Pound ya Uingereza nk ni rahisi sana na wala hutaulizwa swali lolote. Ajabu ni pale ukitaka kununua USD au Pound; utaulizwa passport!

Kuuza na kununua pesa za kigeni katika maduka haya hakuna udhibiti wowote kutoka serikalini, hawa wamiliki wanajifanyia tu biashara wapendavyo; hatuna uhakika kama serikali inafaidika na biashara hii au ni kwa manufaa ya wamiliki ambao wengine wao ni wakubwa wa Serikalini.

Ukweli ni kuwa hakuna nchi yoyote ile makini ambayo haina udhibiti wa fedha za kigeni zinazoingia na kutoka kupitaia Berau de Change isipokuwa Tanzania tu.

Nilitembelea Uganda hivi karibuni nikiwa na vidola vyangu vya Kimarekani nikadhani mimi ni mfalme. Nilipoenda kubadilisha ili nipate shilingi za uganda ndipo nikagundua jinsi serikali ya Uganda ilivyo makini na biashara hii. Ilikuwa ni duka la kawiaida tu mtaani. Nilipoingia kubadilisha ili nipate Ushs nilulizwa passport kwanza (yaani kuwauzia USD naulizwa passport wakati TZ ni kinyume chake). Nlipowapa pasport wakaniomba USD na nilipowapa ndipo wakaanza kujaza makaratasi (fomu) kibao! Yaani jina langu na namba yangu ya passport na kiasi nilichouza vyote viliandikwa! Hapo ndipo nilipooona jinsi Serikali yaUganda ilivyo makini na uchumi wake na jinsi wanavyo-monitor pesa za kigeni zinazoingia na kutaka nchini mwao kitu ambacho ni muhimu kwa uchumi na katika kudhibiti pesa chafu.

Hii ilinipa mawazo kuwa kama hizi Bereau de Change za kwetu ni mfereji wa kupeleka fedha ng'ambo na ni njia nzuri kwa wamiliki wake kuhodhi fedha za kigeni kitu ambacho huchangia kwa kiasi kikubwa mfumuka wa Bei (shilingi kushuka thamani na kupandisha thamanai ya USD).

Nadhani serikali yetu na wataalamu wetu wa Uchumi na BoT ni vema wakadhibiti uuzaji wa fedha za kigeni katika Burea de Change vinginevyo thamani ya pesa yetu itakuwa chini kila siku.
 
Ibrah kuna kingine hukukinote huko Uganda nacho ni receipt. Receipts za bureau zote kwenye kubadili foreign currency ni za Bank Kuu ya Uganda. Hii inaashiria udhibiti wa wazi wazi kwenye foreign currency. So bank kuu yao wanajuwa kiasi gani kimeingia na kiasi gani kimetoka. Hapa kwetu kila bureau na receipt yake infact receipt hapa ni optional unaulizwa kama unahitaji au lah.

Nimepata bahati ya kutembea nchi kadhaa za Africa, my very honest opinion ni kwamba sisi maeneo mengi ni wachovu kuliko tunavyofikiri. Hata wale tunawaona ni hopless kama Nigeria mambo yao mengi wanayafanya vizuri tu. Huwanajiuliza hawa viongozi wetu ambao ni wataalamu wazuri wa kusafiri hivi wakienda huko huwa wanaishia kufanya shopping tu halafu basi?!?!? Mungu tusaidie Tanzania.
 
Naona tunasahau ngama ya miaka ya 80/early 90's.. Yale yale ya wana wa Israeli jangwani Sinai
 
Ibrah kuna kingine hukukinote huko Uganda nacho ni receipt. Receipts za bureau zote kwenye kubadili foreign currency ni za Bank Kuu ya Uganda. Hii inaashiria udhibiti wa wazi wazi kwenye foreign currency. So bank kuu yao wanajuwa kiasi gani kimeingia na kiasi gani kimetoka. Hapa kwetu kila bureau na receipt yake infact receipt hapa ni optional unaulizwa kama unahitaji au lah.

Nimepata bahati ya kutembea nchi kadhaa za Africa, my very honest opinion ni kwamba sisi maeneo mengi ni wachovu kuliko tunavyofikiri. Hata wale tunawaona ni hopless kama Nigeria mambo yao mengi wanayafanya vizuri tu. Huwanajiuliza hawa viongozi wetu ambao ni wataalamu wazuri wa kusafiri hivi wakienda huko huwa wanaishia kufanya shopping tu halafu basi?!?!? Mungu tusaidie Tanzania.
 
Kwa sasa kunakuja sheria kutoka BoT kwamba wale wote wenye Bureau wanatakiwa kuwa na computer based system of tracking transactions.
 
Kweli Ibrah hata huku China kubadi pesa mpaka passport na ujaze form,sio mambo ya Bongo kwetu.
 
Huu ni ufisadi mwingine maana kuna wageni ambao si Watanzania wanaruhusiwa kufungua biashara ya Bureau De Change, nchi nyingine kuna biashara ambazo waheni hawaruhusiwi kabisa kuzifanya, lakini siyo kwetu. Nasikia wanataka kupiga marufuku wageni wote wasiruhusiwe kuwa na bureau de change, lakini nchi yetu maneno marefu lakini vitendo ni ZERO.

Walisema kwamba wafanyabiashara wote wanaotaka malipo kwa dollar wanavunja sheria na wataanza kuchukuliwa sheria, lakini hadi hii leo hakuna yeyote yule aliyekamatwa maana wavunjaji sheria wengi wamo serikalini na kwenye chama wanafumbia macho tu wakati sheria zetu zinaendelea kupindwa na kudharauliwa kila kukicha
 
Acheni ubwege...haya mambo hayapo!!!mtaongeza ukiritimba wadau....si kuwa yapo Uganda na China basi na hapa ziwepo...

Haya Mambo DUBAI hayapo, sehem ambayo karibu kila mwananchi anayo passport.

Inakuwaje mzazi katumiwa pesa na ndugu yake kutoka UK, anatakiwa atumie anaambiwa awe na passport wakati yeye Hana....

ACHENI UZEMBE KUZIBHITI VITU VYA KILA KITU...INFLATION INASABABISHWA NA VITU VINGINE KABISA....

SO FAR SHERIA YA PASSPORT IPO....HASA UNAPOTAKA UPEWE DOLA HAPA TZ...Huwa inatupa tabu wengine hadi tutafute wengine wenye passport kutuchukulia pesa, matokeo yake nao huhitaji kitu kidogo....
 
Msitake turudi kule kwenye miaka ya themanini ambapo kulikuwa kuna sheria kali kuhusu fedha za kigeni lakini fedha zenyewe hazikuwepo. Tulipolegeza hizo sheria, basi fedha zillianza kuonekana.

Tatizo letu ni kushamiri kwa ukiukwaji wa sheria. Sio tatizo la upungufu wa sheria za forex. Kila mwisho wa mwaka nawasili Dar na kubadilisha dola kiasi. Mara nyingi lazima nidai risiti ndio nipewe. Na hiyo kawaida ya kutoa risiti feki au kutotoa risiti kabisa naiona kwenye biashara nyingi Dar, sio kwenye maduka ya forex tu. Maduka ya vifaa vya ujenzi na maduka ya spea za magari yameshamiri vitendo hivyo.

Hali tuliyonayo ya kuweza kubadili fedha kwa urahisi ni nzuri. TRA na Polisi wangeweza kabisa kuwakamata wale wanaotoa vyeti feki kama wangependa. Ni kiasi cha wao kwenda madukani na kubadilisha fedha.

Ukitaka kununua dola bila shaka unaangaliwa zaidi. Lakini kama dola tayari unazo, kwanini usumbuliwe kuzibadilisha? Mnataka tuanze tena kubadilisha kwa magendo? Maana lazima tubadilishe, na mfumo wa zamani wa kwenda kuketi NBC masaa 6 ndio umalize shida yako hatutaukubali tena.
 
Pesa zinatorooshwa sana kupitia airports zetu (sina uhakika kama kuna sharia ya kudhibiti utoroshaji pesa nje ya nchi) kama UK na Australia nakumbuka wakati Fulani niliingia na kiasi zaid ya 10,000 USD Australia wakazizuia zile pesa mpaka nitakapotoa maelezo ya SOURCE ya zile PESA
 
Ibrah kuna kingine hukukinote huko Uganda nacho ni receipt. Receipts za bureau zote kwenye kubadili foreign currency ni za Bank Kuu ya Uganda. Hii inaashiria udhibiti wa wazi wazi kwenye foreign currency. So bank kuu yao wanajuwa kiasi gani kimeingia na kiasi gani kimetoka. Hapa kwetu kila bureau na receipt yake infact receipt hapa ni optional unaulizwa kama unahitaji au lah.

Nimepata bahati ya kutembea nchi kadhaa za Africa, my very honest opinion ni kwamba sisi maeneo mengi ni wachovu kuliko tunavyofikiri. Hata wale tunawaona ni hopless kama Nigeria mambo yao mengi wanayafanya vizuri tu. Huwanajiuliza hawa viongozi wetu ambao ni wataalamu wazuri wa kusafiri hivi wakienda huko huwa wanaishia kufanya shopping tu halafu basi?!?!? Mungu tusaidie Tanzania.
Maswahiba tunakumbushana tu
 
Nimekuwa mteja wa kubadili pesa mara kwa mara hasa wakati nataka kwenda nje kikazi au hata kutembele jamaa na marafiki.

Awali sikuwa najua kwamba hizi Bureau de Change ni mahsusi kwa ajili ya kutorosha pesa zetu kwenda nje. Lakini kuna siku baada ya kupata fununu hizi nilikuwa makini kidogo kutaka kujua kama ni kweli kuna mchezo mchafu unao fanyika wakati mteja anapofika mahali hapo kwa lengo la kubadilisha pesa. Kinachofanyika ni kutoa receipt ambayo si halisi kwa ajili ya wakaguzi wa TRA.

Nilikuja kubaini hili baada ya kuona jamaa wananipatia receipt ambayo ni tofauti na receipt aliyopewa mteja aliyetangulia kwa lengo hilo hilo. Kilichofanyika ni kwamba wale wahindi walitazamana usoni kisha wakakubaliana jambo fulani kisha wakaleta kijitabu kingine cha receipt na kile cha awali kikawekwa chini ya counter na nikahudumiwa na kutoka wakati wote hao jamaa wakikonyezana mimi nilikuwa najifanya kusoma prices za kubadilisha fedha.

Kwa hiyo nikaona nitoe haya machache kwa wana JF ili mwenye mchango zaidi wa haya niliyoyachokonoa atupatie mwanga zaidi kwani naamini mchango wa wana JF ni suluhisho tosha katika harakati za kukabiliana na ubadhirifu wa uchumi.

Nawasilisha.
Kuna risiti za system ambazo zinasoma na BOT kabisa ambazozinahitaji ID na kila kitu.Then kuna risiti ya mfanyakazi wa Bureau ambaye anampiga bosi wake.Anakuja na hela zake anazizungusha hapo hapo.Na kuna risiti ya boss kwa ajili ya kulegeza vyuma
 
Kuna vitu mnachanganya sana.. Ikiwa UG wako vizuri kuthibiti fedha hizo za kigeni tungeona UGX ikiwa imara sana zaidi ya TZS.. Mambo mengine haya muwaachie tu wachumi sio kubwabwaja msiyokuwa na uelewa nayo. Thamani ya hela kupanda au kushuka haijawahi kuongozwa na maduka ya kubadilishia fedha. Hakuna nchi duniani ambayo hela zake nyingi zimezagaa nchi zote ulimwenguni kama USA ila bado dola inabaki na thamani yake suala la kusema hela zinatoroshwa ni kichekesho tu.
 
Nimekuwa mteja wa kubadili pesa mara kwa mara hasa wakati nataka kwenda nje kikazi au hata kutembele jamaa na marafiki.

Awali sikuwa najua kwamba hizi Bureau de Change ni mahsusi kwa ajili ya kutorosha pesa zetu kwenda nje. Lakini kuna siku baada ya kupata fununu hizi nilikuwa makini kidogo kutaka kujua kama ni kweli kuna mchezo mchafu unao fanyika wakati mteja anapofika mahali hapo kwa lengo la kubadilisha pesa. Kinachofanyika ni kutoa receipt ambayo si halisi kwa ajili ya wakaguzi wa TRA.

Nilikuja kubaini hili baada ya kuona jamaa wananipatia receipt ambayo ni tofauti na receipt aliyopewa mteja aliyetangulia kwa lengo hilo hilo. Kilichofanyika ni kwamba wale wahindi walitazamana usoni kisha wakakubaliana jambo fulani kisha wakaleta kijitabu kingine cha receipt na kile cha awali kikawekwa chini ya counter na nikahudumiwa na kutoka wakati wote hao jamaa wakikonyezana mimi nilikuwa najifanya kusoma prices za kubadilisha fedha.

Kwa hiyo nikaona nitoe haya machache kwa wana JF ili mwenye mchango zaidi wa haya niliyoyachokonoa atupatie mwanga zaidi kwani naamini mchango wa wana JF ni suluhisho tosha katika harakati za kukabiliana na ubadhirifu wa uchumi.

Nawasilisha.
Uongo huo.
 
Kwa maelezo hayo hujaeleweka, rejea kichwa cha habari ulichokiandika mwenyewe. Napata shaka na uwezo wako kidogo kwakuwa habari ulioiandika na kichwa cha habari ni vitu viwili tofauti. Kama huu ndio uwezo wako ni ngumu sana kugundua mbinu za wahindi wenye uzoefu na kazi zao kwa muda mrefu.
Muda wote uliwaona wahindi wakikonyezana, hao wahindi ni mazuzu hata wakonyezane muda wote mbele ya mtu ambae wameshamhisi ni hatari kwa biashara yao?
Tofauti ya risiti ndio kilichokusababisha uhisi wanatorosha pesa? Kivipi?
 
Au walikuwa wanakonyezana kwa sababu nyingine kabisa.

Labda Muhusika kama ni Mdada alikuwa ameajaaliwa n.k.
 
Back
Top Bottom