Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,127
- 3,480
Nimekuwa mteja wa kubadili pesa mara kwa mara hasa wakati nataka kwenda nje kikazi au hata kutembele jamaa na marafiki.
Awali sikuwa najua kwamba hizi Bureau de Change ni mahsusi kwa ajili ya kutorosha pesa zetu kwenda nje. Lakini kuna siku baada ya kupata fununu hizi nilikuwa makini kidogo kutaka kujua kama ni kweli kuna mchezo mchafu unao fanyika wakati mteja anapofika mahali hapo kwa lengo la kubadilisha pesa. Kinachofanyika ni kutoa receipt ambayo si halisi kwa ajili ya wakaguzi wa TRA.
Nilikuja kubaini hili baada ya kuona jamaa wananipatia receipt ambayo ni tofauti na receipt aliyopewa mteja aliyetangulia kwa lengo hilo hilo. Kilichofanyika ni kwamba wale wahindi walitazamana usoni kisha wakakubaliana jambo fulani kisha wakaleta kijitabu kingine cha receipt na kile cha awali kikawekwa chini ya counter na nikahudumiwa na kutoka wakati wote hao jamaa wakikonyezana mimi nilikuwa najifanya kusoma prices za kubadilisha fedha.
Kwa hiyo nikaona nitoe haya machache kwa wana JF ili mwenye mchango zaidi wa haya niliyoyachokonoa atupatie mwanga zaidi kwani naamini mchango wa wana JF ni suluhisho tosha katika harakati za kukabiliana na ubadhirifu wa uchumi.
Nawasilisha.