Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,630
- 106,614
SALUTE COMRADES
Miaka mingi kumekua na nadharia inayosema kua binaadamu tunatumia asilimia 10% tu ya ubongo wetu katika mambo yote tunayofanya, gunduzi zote za kiteknolojia na kisayansi, kufikiria na kufanya maamuzi kwenye vitu vigumu na mambo kadhalika ni asilimia 10% tu ndio metumika!wengine wanasema Albert Enstein alitumia 13% ya ubongo wake. Kama kwa maendeleo yote haya tumetumia asilimia kumi imagine tukiweza tumia 100% ya akili zetu
Muvi mbalimbali kama LUCY aliyocheza mwigizaji scarlet Johnson ilizidi kupigilia msumali nadharia hii kwa kuonyesha jinsi ambavyo huyo bnti Lucy alivyokula madawa ambayo yalimfanya kuweza kua na uwezo wa kutumia akili yake kwa asilimia 100% ambapo alianza kuweza kusafiri katika muda kwa akili (Mind Time Travelling), aliweza kukontroo magari kwa akili,aliweza kutumia kioo cha gari kama computer, aliweza kujifunza kichina ndani ya sekundi na mengine meengiii. Pia muvi mbalimbali kama Limitless ya Bradley Cooper, Define your life, flight of the navigator na kadharika zimeelezea nadhalia hii ya 10% of Brain.
Inasemekana kua nadharia hii ilisambazwa na mwandishi wa habari aitwae Lowell Thomas kwa kutumia kitabu chake kiichoitwa How to win friends and influence peoples ambapo alimnukuu vibaya mwanasaikolojia William James ambapo aliwahi kusema “average person specifically develops only 10% percent of his/her latent ability” ambapo kiuhalisia James alikua amezungumzia “our latent mental energy” lakini pia inaonekana kua nadharia hii pia ilichagizwa pia kuenea na mtalamu wa ubongo (Neurosurgeon) Wilder Penfield ambapo aligundua silent cotex mnamo mwaka 1930’s ambapo alisema kua silent cotex haina kazi kwenye ubongo mpaka ishituliwe na na umeme lakini kiuhalisia hiyo sehemu siku hizi imegundulika kua inafanya kazi.
Wanasayansi wengi wanasema kua nadharia hii ni uongo! Bnaadamu wote tunatumi 100% ya ubongo wetu, vifaa vya kisasa kama brain scanning vinaonyesha ubongo wetu unafanya kazimuda wote kwa kupitia viungo vyote hata tukiwa tumepumzika zipo tafiti nyingi zimefanywa zinaonyesha kua binaadamu tunatumia 100% ya ubongo wetu.
Kwenu GreatThinker je mna maoni gani juu ya hili? Ni kweli tunatumia 10% kwa mnavyodhani na kama tunatumia 10% ya uwezo wa ubongo wetu nini kitatokea kama tutaweza kutumia 100% ya uwezo wa ubongo wetu??
Tchao..
~Da’Vinci..