Je, ni kweli binadamu tunatumia asilimia 10 ya uwezo wa ubongo, na nini kitatokea kama tutatumia asilimia 100 ya uwezo huo?


Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
is-2-jpg.1018243

SALUTE COMRADES
Miaka mingi kumekua na nadharia inayosema kua binaadamu tunatumia asilimia 10% tu ya ubongo wetu katika mambo yote tunayofanya, gunduzi zote za kiteknolojia na kisayansi, kufikiria na kufanya maamuzi kwenye vitu vigumu na mambo kadhalika ni asilimia 10% tu ndio metumika!wengine wanasema Albert Enstein alitumia 13% ya ubongo wake. Kama kwa maendeleo yote haya tumetumia asilimia kumi imagine tukiweza tumia 100% ya akili zetu

Muvi mbalimbali kama LUCY aliyocheza mwigizaji scarlet Johnson ilizidi kupigilia msumali nadharia hii kwa kuonyesha jinsi ambavyo huyo bnti Lucy alivyokula madawa ambayo yalimfanya kuweza kua na uwezo wa kutumia akili yake kwa asilimia 100% ambapo alianza kuweza kusafiri katika muda kwa akili (Mind Time Travelling), aliweza kukontroo magari kwa akili,aliweza kutumia kioo cha gari kama computer, aliweza kujifunza kichina ndani ya sekundi na mengine meengiii. Pia muvi mbalimbali kama Limitless ya Bradley Cooper, Define your life, flight of the navigator na kadharika zimeelezea nadhalia hii ya 10% of Brain.

Inasemekana kua nadharia hii ilisambazwa na mwandishi wa habari aitwae Lowell Thomas kwa kutumia kitabu chake kiichoitwa How to win friends and influence peoples ambapo alimnukuu vibaya mwanasaikolojia William James ambapo aliwahi kusema “average person specifically develops only 10% percent of his/her latent ability” ambapo kiuhalisia James alikua amezungumzia “our latent mental energy” lakini pia inaonekana kua nadharia hii pia ilichagizwa pia kuenea na mtalamu wa ubongo (Neurosurgeon) Wilder Penfield ambapo aligundua silent cotex mnamo mwaka 1930’s ambapo alisema kua silent cotex haina kazi kwenye ubongo mpaka ishituliwe na na umeme lakini kiuhalisia hiyo sehemu siku hizi imegundulika kua inafanya kazi.

Wanasayansi wengi wanasema kua nadharia hii ni uongo! Bnaadamu wote tunatumi 100% ya ubongo wetu, vifaa vya kisasa kama brain scanning vinaonyesha ubongo wetu unafanya kazimuda wote kwa kupitia viungo vyote hata tukiwa tumepumzika zipo tafiti nyingi zimefanywa zinaonyesha kua binaadamu tunatumia 100% ya ubongo wetu.

Kwenu GreatThinker je mna maoni gani juu ya hili? Ni kweli tunatumia 10% kwa mnavyodhani na kama tunatumia 10% ya uwezo wa ubongo wetu nini kitatokea kama tutaweza kutumia 100% ya uwezo wa ubongo wetu??

Tchao..

~Da’Vinci..
 
gigabyte

gigabyte

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Messages
884
Likes
770
Points
180
Age
35
gigabyte

gigabyte

JF-Expert Member
Joined May 27, 2015
884 770 180
Bado sijaelewa.Je kinachoangaliwa ni 10% ya matumizi ya ubongo au 10% ya kufikiria kwetu.Kama ni matumizi ya ubongo katika utendaji kazi katika shughuli mbali mbali naweza kusema ubongo unafanya kazi kwa 100% ila kama ni kwenye kufikiria waliosema tunafikiria chini ya 10% wako sahihi kwasababu bado naamini yako mambo mengi sana ambayo binadamu bado hajayafikiria.Tena kama uku kwetu ndo kabisa hatutaki kusumbua bongo zetu kwenye tafakuri.Kwaiyo zile zama zilizosemwa kwenye Bible kua maarifa yataongezeka mimi naamini bado hazijafika kwasababu mambo mengi tunayoyaona sasa ni tafakari ya wazee wetu wa zamani.Kizazi cha sasa labda kwasababu tulikuta tayari vitu vimeshafikiriwa hatutaki kusumbuka sana kutafakari vya kwetu zaidi ya pale walipoishia wazee tunapambana kumodify mawazo ya wazee.
 
7 mchana

7 mchana

Senior Member
Joined
Dec 30, 2018
Messages
101
Likes
36
Points
45
7 mchana

7 mchana

Senior Member
Joined Dec 30, 2018
101 36 45
Ndio hapo utata unapokuja sasa. Era tuliyonayo imerelax sana. Tupo ktk comfort zone ambayo mwisho wake sio mzuri.

Mzungu na race kadhaa za dunia hii ndio pekee waliobaki wanaishi ktk reality kwa kias kikubwa. Wanashughulisha bongo zao kuzidi kugundua vitu vipya kila siku. They are producers.

Waafrika kwa asilimia kubwa tupo vifungoni. We are living just for surviving. Na hata mm na ww ambao tuna think out of the box tukisema tutoke out of this zone itahitajika nguvu ya ziada sabab tupo kifungoni.

IQ ni kweli tumetofautiana. Ndio mana hata darasani huwa hatupati maksi sawa wote.
suala LA IQ Naona ni imani tu hakuna ktu kama hchi. Wanafunzi kutofautiana max class hawez measure chochote about someone's mental ability
 
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
477
Likes
879
Points
180
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
477 879 180
suala LA IQ Naona ni imani tu hakuna ktu kama hchi. Wanafunzi kutofautiana max class hawez measure chochote about someone's mental ability
Sasa kipimo kipi ndio bora zaid kweny kumeasure mental ability?
 
7 mchana

7 mchana

Senior Member
Joined
Dec 30, 2018
Messages
101
Likes
36
Points
45
7 mchana

7 mchana

Senior Member
Joined Dec 30, 2018
101 36 45
Sasa kipimo kipi ndio bora zaid kweny kumeasure mental ability?
hakuna kipimo kunachoweza kutofautisha... ila pale inapokua abnormal sana ndo twajakuwatambua watu waliochanganyikiwa na kadhalika... perfomance darasa iko influenced na vtu vngi sana.

Student anaweza perform low in class kwa sababu mbali mbali eidha hayuko interested na lessons husika ama pengine kuna vtu anavfikilia nje ya masoma yale ambayo yana weza kuwa positive ama negative Katina maisha yake au anamattzo huko hatokako

Vyote hv vnawezamfanya a loose concentration Mara kwa mara awapo katika lessons zake


Na haina maana kuwa ana low IQ
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
Nawasubiri wadau mtiririke..
 
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined
Jan 14, 2019
Messages
48
Likes
122
Points
40
Wordsworth

Wordsworth

Member
Joined Jan 14, 2019
48 122 40
Imesemwa hivi kwa muda mrefu, ila sio kweli kwamba tunatumia 10% tu ya ubongo wetu.
 
Ziroseventytwo

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
4,824
Likes
3,657
Points
280
Ziroseventytwo

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
4,824 3,657 280
Dr Norman Vincent Peal outher wa kitabu kiitwacho The power of positive think anasema kuwa ikitokea binadamu akatumia akili yake kwa kufikia 50% angeweza kuujenga mji wa New York kwa siku 1.

Hii inaonyesha kwamba binadamu wengi bongo zetu ni new brand yaani hazijatumika kabisa. Watu wa aina ya Eistern, Newton, Kina Da Vinci ndio watu wanaoonekana kutumia akili nyingi sababu mambo waliyofanya yanaonekana. Na hii imewasaidia maana wao waliyaweka kwenye maandishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
Basi waafrika huwa tunatumia percentage chache sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwalimu wangu wa E science aliwahi tuambia kitu kama hicho.. ati asilimia 90 ubongo wetu waafrika tunauzika ila wazungu wanatumia karibia 60% ya ubongo. Sikuwahi kumwelewa wala kumuamini

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
Dr Norman Vincent Peal outher wa kitabu kiitwacho The power of positive think anasema kuwa ikitokea binadamu akatumia akili yake kwa kufikia 50% angeweza kuujenga mji wa New York kwa siku 1.

Hii inaonyesha kwamba binadamu wengi bongo zetu ni new brand yaani hazijatumika kabisa. Watu wa aina ya Eistern, Newton, Kina Da Vinci ndio watu wanaoonekana kutumia akili nyingi sababu mambo waliyofanya yanaonekana. Na hii imewasaidia maana wao waliyaweka kwenye maandishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli sometimes hili linafikirisha mno mkuu!! Sidhani kama nina fikra hata nusu theruthi ya da vinci...

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
@Educational mentor tupe maoni yako kama mtaalamu wa mambo ya akili

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Blaki Womani

Blaki Womani

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
10,408
Likes
7,722
Points
280
Blaki Womani

Blaki Womani

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
10,408 7,722 280
Hii imenikumbusha kichekesho kimoja kama sio ukweli.

Kwamba kulikuwa na vichwa 3 vimewekwa chumba cha maonyesho kimoja cha mzungu kingine kutoka Asia na kingine kutoka Africa. Kichwa cha mzungu hakikuwa na ubongo kabisa kile cha Masia ubongo ulikuwa robo na kile cha Mwafrika ubongo ulikuwa kama alivyozaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,644
Likes
43,620
Points
280
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,644 43,620 280
Hii imenikumbusha kichekesho kimoja kama sio ukweli.

Kwamba kulikuwa na vichwa 3 vimewekwa chumba cha maonyesho kimoja cha mzungu kingine kutoka Asia na kingine kutoka Africa. Kichwa cha mzungu hakikuwa na ubongo kabisa kile cha Masia ubongo ulikuwa robo na kile cha Mwafrika ubongo ulikuwa kama alivyozaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio story zenu wazee mnawadanganya watoto...
Eti Mungu wakati anagawa akili mwafrika alichagua ngoma wazungu wajachagua akili ya Maendeleo eti ndio maana tunadumisha ngoma za asili na mila kuliko kudumisha mambo ya Maendeleo

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 

Forum statistics

Threads 1,262,487
Members 485,588
Posts 30,123,570