Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,434
- 113,444
Wanabodi,
Kwanza niungane na Watanzania wenzangu kumpongeza rais Magufuli na timu ya majadiliano kwa malipo ya Advance ya Dola $ milioni 100 ikiwa ni sehemu za yale malipo ya fedha zilizoitwa Kishika Uchumba cha Dola milioni 300 za Barrick.
Pongezi hizi nazitoa kwa dhati kwanza kwasababu ni mimi ni miongoni mwa Matomaso wa JF ambao tulikuwa na mashaka kuwa fedha hii haitalipwa, hivyo hadi jana ulipolipwa, ndipo tumeamini.
Barrick katika taarifa yao, wamesema balance watalipa ndani ya miaka mitano, kwa kulipa dola milioni 40 kila mwaka.
Lakini leo nimemsikia Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza live na Clouds Radio, kipindi cha 360, amesema balance italipwa katika Mikupuo miwili ya Dola milioni 100 kila mkupuo. Hii kama ni kweli, then ni habari njema kwetu.
Mfano tungeipata ile dola milioni 300 yote kwa mpigo, tungeweza kufanyia mambo makubwa zaidi kuliko kupata dola milioni 40 kila mwaka kwa miaka mitano!
Sasa ni hili la balance ya malipo, kama wenyewe wamesema watalipa dola milioni 40 kwa mwaka ndani ya miaka 5, halafu tukafanikiwa kuwahimiza waharakishe, hivyo hili tangazo la Waziri kuwa sasa tutalipwa dola milioni 100 in two installments, hili ni jambo kubwa jema na zuri kwa maslahi ya taifa. Issue inabaki ni moja tuu, nani mkweli kati ya Barrick na Waziri wetu?.
Nawatakia Jumatano Njema.
Paskali