Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,568
Kwa sasa Serikali na mashirika yake haipaswi kuwa ndio mwajiri mkuu, badala yake serikali wajibu wake ni kujenga na kukuza sekta binafsi ili itoe ajira. Ni bahati mbaya sana wahitimu wengi wana ndoto za miaka ya 80 kwamba ajiri ziko serikalini au mashirika ya umma kama Tanesco, BoT, NSSF, PPF, Mamlaka za maji nk. hivyo wanapopata kazi makampuni binafsi huwa hawajitumi kwani wanachukulia kama vile mtu aliyepunzika barazani kwa mtu kusubiri mvua iishe aendelee na safari yake. Wengine hukaa tuu nyumbani wanangojea ajira za serikali na mashirika yake wakati kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu wapya. Bila kuondoa mawazo mgando kwa jamii kuwa ili uhesabike una kazi nzuri ni mpaka uajiriwe kwenye serikali na mashirika yake, malalamiko juu ya ajira za upendeo hayataisha. Baadhi ya waajiri binafsi nao wanaelekea kukata tamaa ya kutoa ajira kwa wahitimu wapya kwani hawakai, hujifunza kazi na kukimbilia serikalini na wakati mwingine kwenda kulipwa mshahara mdogo zaidi kwa mategemeo ya kusomeshwa zaidi kuko mbeleni