Je, ni kweli 99% ya watanzania ni waoga?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Nimepitia maeneo na kusikia tunasemwa kuwa sisi watanzania huwa ni waoga sana, mkusanyiko huu ulikuwa unajumuisha watanzania na wengine wa mataifa jirani na kwetu, walichosema ni kwamba ikitokea swala la:

Mahakamani: mtanzania anapopewa kesi ya uongo au madai ya uongo au kudhalilishwa na ikitokea ameshinda kesi dhidi ya tuhuma juu yake huwa ni muoga kuomba kulipwa fidia kwa muda alio upoteza, kwa ajili ya gharama za kesi na mengineyo hivyo huishia kukaa kimya bila ya kujali amepoteza sana kwenye kesi hiyo. Wakaongeza haijalishi ni taasisi ipi lakini kwenye ofisi binafsi mtanzania anweza akawa na ujasiri wa kudai fidia ila taasisi zingine na watu wengine kama viongozi na wakuu flan huwa ni waoga kudai fidia je hili ni kweli? Walichosema ni kwamba endapo hawatakuwa waoga na kuamua kuwa wanadai fidia basi matatizo madogo ya kushtakiana na kupewa kesi yatakuwa ni historia. Sasa mtanzania afanyeje ili awe na ujasiri.

Kuomba kazi za kufundisha nje ya nchi: mtanzania hata akiwa professor amehitimu ulaya au marekani au hapa nchini mfano amepata PhD huishia kuomba nafasi za kisiasa badala ya kutafuta vibaruwa vya kufundisha nje ya nchi na nchini kwake maana anaweza akawa anafundisha nchini kwake na nchi za nje anaenda kama consultant, sasa haieleweki ni uoga na kukosa self confidence ya kuwa ma consuntants nje ya nchi hata nchi jirani achilia mbali ubaguzi na ukabila wakaenda mbali kuanza na takwimu ya watanzania ma professor kwenye vyuo vya nchi jirani na kwetu Kenya, Uganda, Burundi, nchi za afrika magharibi… takwimu haikuwepo ila waliosoma huko walisema wengine hawajawahi sikia na wengine walisema yuko mmoja tu, sasa wanao fundisha hapa nchini na kufundisha nje ni wa kuhesabu yani wachache sana ukilinganisha na wenzetu maana wao ni waabunifu na wanasikika sana kwa michango yao katika ngazi za kimataifa ndio maana wanachukuliwa kufundisha vyuo vya nje, sasa hapa tatizo ni nini. Wanasema ma professor wengi baada ya kufundisha vyuoni jioni utawaona wako na redio zao wanasikilza taarifa ya habari na likizo ikifika wanaenda vijijini kwao na si kutafuta sehem za kuchakarika nje ya nchi ili kuongeza wigo wa maslahi na posho na hakuna mwenye ujasiri wa kukataa nafasi za kisiasa maana wanajua ndio hapo wanapoona pana wafaa, swala sio maslahi swala ni exposure na michango ya kitafiti na elimu kupeleka nje na kuleta ndani ya nchi. Je swala hili ni kweli na linaendelea tu au.

Kuomba na kufanya kazi nyinginezo kwenye mashirika ya nje ya nchi: kushindwa kujieleza kwenye interview za mashirika makubwa ya kimataifa, kukosa confidence ya kuingia kwenye mashirika na kufanya kazi bila ya mazoea. Tunao wengi walio hitumu toka mwaka 2014 na kuendelea au nyuma ya hapo na wana Masters au postgraduate wanakosa ujasiri wa kuwa buzy kuomba kazi nje ya nchi badala yake wanasubiri serikali ndio iajiri waombe au mashirika yasiyo ya kiserikali yafungue matawi ndio waombe kazi, wachache sana wanaomba na ni wa kuhesabu. Je ni kweli sasa tufanyeje au nini kifanyike ili tuwe na ujasiri huo.
 
Hiyo 1% iliyobaki ni mimi.
 
Haikuwa nia ya Baba wa Taifa kujenga Taifa lenye watu waoga kama ambavyo amewahi kusema kwenye hotuba zake, lkn matokeo yake ndiyo hayo. Inawezekana hatukumuelewa vizuri wakati wake, au alitumia njia isiyo sahihi kujenga Taifa aliloliota. Taifa lenye watu waoga si Taifa la kujivunia. Unaweza lielewa hili kama tu wew si mwoga, na unajuwa mjisikio wanaoupata watu wasio waoga juu ya walio waoga. Mtu muoga ni mpofu wa kuonewa, kukandamizwa, kunyimwa haki za msingi, kutawaliwa kimabavu wala hawezi ona kama utawala wa sheria unakiukwa.

Mtu muoga pia anaweza kuziba macho na kujipa upofu kwa makusudi kabisa ili lengo lake binafsi, pengine na la familia yake, liweze timia. Huwezi ukalisaidia Taifa lako kwa kuangalia maslahi binafsi au na ya familia yako. Watu hawa ndio huwa wanamaswali kerefu kama "ili iweje?", "ninakosa nini? " "nitafaidika nini?" na mengine mengi, ambayo kimsingi, kama wew si kipofu, lazima ukasirike sana juu ya huu upofu wa watu hawa.

Hawa watu wanaojipa upofu huwa wako tayari, tena kwa kushupaa sana, kutetea maovu yafanywayo na watawala kwa kuwa kufanya ivo, mkono huenda kinywani - maslahi binafsi. Watu hawa ni adui kwa Taifa linalotaka kujenga misingi ya demokrasia na maendeleo kwa kuwa hurudisha nyuma mara mbili hatua moja iliyopigwa katika kujenga misingi imara ya Taifa.

Baba wa Taifa alikuja kugundua kuwa Taifa letu ni Taifa la watu waoga, na alikuwa anakerwa sana kuliona Taifa likiwa ivo. Alijuwa fika kuwa Taifa likiwa na watu waoga lazima litazalisha viongozi dikteta kwa kuwa hakutakuwa na sauti ya umma ya kusema HAPANA, bali ya wachache ambao hawatasikika sana. Inawezekana aligundua hili kwa kuchelewa sana, na bahati mbaya Mungu akamchukua mapema. Huenda angekuwepo mpaka leo hii, angeweza kusaidia ujenzi wa taifa lisilo na watu waoga kwa kuwa tayari alikuwa kishaliona tatizo.

Sasa Baba wa Taifa hayupo, nguvu yake ambayo ingeweza kusikilizwa na viongozi wa wakati huu haipo, na aliyoyaona ndiyo yanatokea. Swali la kujiuliza ni moja tu: NANI ATAWEZA KUBADILISHA TAIFA HILI LIWE TAIFA LA WATU WASIO WAOGA? Lazima wawepo wa kutuongoza.

Huwezi ukajiita MZALENDO kama wew ni muoga, hukemei kwa namna yeyote ile mambo na mienendo inayoharibu misingi ya demokrasia na utawala bora - vitu vinanyoleta ustawi wa taifa lolote. Huwezi kujiita MZALENDO kama wew ni kiongozi halafu unakiuka misingi ya demokrasia na utawala bora!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu komboa fikra za Watanzania, amina!
 
Huyo Baba ndie aliyesababisha watu wawe waoga mpaka sasa, ilikuwa hata kumuongelea unaogopa "Eti atakusikia". Watu hata kwenye mitandao wanogopa kusema kweli wakati id anayotumia ni fake ip address fake lkn mtu mwoga. Ukitaka kuishi kwa amani Tz ukubali unyonge la sivyo utakunyia debe.
 
Unamwili wakuleta hapa
IMG_20180426_163809_849.jpg
IMG_20180426_163942_347.jpg
 
Back
Top Bottom