Lugumgya
JF-Expert Member
- Dec 10, 2019
- 629
- 1,997
Ilikuwa juzi mida ya saa 2 usiku nikapokea simu kutoka kwa Mdogo wangu, akiniuuliza swali hilo! Yaani M 3 si kama nanunua? Why all that amount? Nahisi hawataki labda nimuoe! Au nimchukue bila kutoa chochote and the girl is ready! Kaka hivi kweli jamani? M.3? Anaendelea kulalamika! Baada ya malalamiko yake nikamwambia Mdogo wangu sikiliza!
Unampenda? Unamuelewa? Yuko tayari kwa ajili yako? Uko tayari ajili yake? Yote alinijibu ndiyo! Una uhakika na hisia zenu, au ni mihemko? Nina hakika brother! Huo uhakika umeupataje? Hujawahi kupendana na mtu Kama mlivyopendana na huyu afu Mwisho wa siku mkaachana? Iliwahi kutokea!
Alivyoondoka uliumia au hukuumia? Niliumia! Ulikuwa umeshamtolea Mahari kiasi gani? Nilikuwa sijamtolea! Kwanini uliumia? Nilikuwa nampenda!
Mdogo Wangu, kutoa mahari hata kama ni elfu 10 au 500 au Milioni 3 si kununua ni utaratibu tuliyoukuta! Hata mama alitolewa ng' ombe 12, miaka ya 80 ambayo ni thamani kubwa kuliko hiyo Milioni 3 yako! Milioni 3 is just fair for a wife! Siyo nyingi Mdogo wangu! Labda Kama hauna! Kama ndo waliyokubaliana na wajumbe uliyowatuma, haina shida.
Brother hapana, mtu mwenyew hana kazi atakuwa anategemea kila kitu kutoka kwangu! Nikacheka kidogo! Kazi anazo sema aliyemwajili atakuwa hamlipi Mshahara! Atafua, atapika, atanyoosha nguo zenu, atadeki, atasimamia malezi na makuzi ya Watoto, atatandika kitanda, atakuhudumia ukiugua, atawahudumia ndugu zako, atakupa sex ambayo wengine wanaitolea hadi magari ( japo zipo na za bure) nk. Ukiajili mtu akufanyie hayo yote miezi kadhaa tu, hiyo Milioni 3 itakuwa imeisha, na bado utakuwa huna mke! Yeye atafanya hizo kazi bure kabisa! Hutalazimika kumtumia nauli Pamoja na ya kutolea ili muonane! Hivyo, hiyo itakuwa ni Shukrani tu kwa wazazi, ni vibaya tu kwamba jamii iliweka utaratibu wa wazazi wa mke kujipangia Shukrani! Lakini kwangu M 3 kwa ajili ya mke is just okay!
Nikaendelea, Mdogo wangu, unakumbuka jinsi Mzee wetu alivyoamua kwenda kutafuta akatuacha Mimi Kaka yenu na mama? Unakumbuka jinsi mama alivyosimama imara kusimamia elimu yetu? Hakuwa na kazi ya ofisini lkn alikuwa na akili na Nguvu! Kama huyo mke wako mtarajiwa ana akili na Nguvu basi M.3 si kitu! Unakumbuka mama alivyofanya vibarua, mkawa mnaniletea unga na shilingi elfu 3 kila mwezi kule shule ya Sekondari kijijini Nyangalagata? Unakumbuka mama alivyowaongoza? Labda ndo maana baba alitoa Ng'ombe 12, aliiona thamani yake! Na wew Kama umeiona hiyo thamani, nitakuunga mkono! Lakini kama huioni thamani hiyo kwake, then M.3 unaporwa bila kupigwa ngeta! Ni Kama kibaka anachukua hiyo hela yako mbele ya Simon Nyankoro Sirro au Alphonce Mabeyo!
Akasema brother naona Kama yuko vizuri! Nikamwambia sawa Mdogo wangu! Kama yuko vizuri, haina shida!
Mdogo wangu mwanamke ni mtu muhimu Sana katika katika maisha yetu na Ustawi wa familia yoyote ile. Kwa hiyo kumlinganisha na kitu Kama M. 3 ni kumkosea heshima! Hiyo kazi inayokufanya uwe na uwezo wa kulipia M .3 imetokana na usimamizi wa mama, baba angeona Ng'ombe 12 ni wengi kwa ajili ya mama, mm na wew labda tusingekuwa na hali tuliyonayo leo! Lakini mama ndo alituombea, alitumia Nguvu zake kutosomesha, akasimamia maadali yetu, akawa mshauri wetu na mfariji wetu Mkuu! Hadi Leo tukienda kijijini kwetu napo panaonekena! Wew unaona M.3 zina thamani kubwa kuliko majukumu ya mwanamke katika familia!?
Japo si lazima utoe hela ndo afanye hayo, hata bure tu anaweza kufanya, washukuru wazazi wake kwa hicho walichoona wanastahili afu mjenge familia katika Imani na upendo! Niko Pamoja na wewe Mdogo wangu! Tarajia kheri!
Je, nimemshauri vibaya? Kama nyie ndo mngekuw kwenye nafasi yangu mngesemaje? M.3 ni nyingi kwa ajili ya mahari ya Mwanamke?
Lugumya!
Sent using Jamii Forums mobile app