Je, ni kwanini Waafrika hatuna undugu na Wazungu?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,563
2,042
Habari za muda huu wadau, nimekaa na kufikiria jambo fulani kuwa je ni sababu ipi kwanini Waafrika hatuna maelewano na Wazungu?

Mwaka wa 418 kulitokea mwanafilosofia wa kigiriki aliyeitwa Herodotus, huyu alidai kuwa "mtu ambaye hajui wala kuelewa chochote au tukio lolote lililotokea kabla ya kuzaliwa kwake basi atabaki kuwa mtoto milele". Dunia ya sasa ni rahisi sana kwa Mwafrika kuelewa maisha ya Diamond Platinumz kuliko hata jina au chimbuko la Baba wa babu yake.

Kipindi cha maisha ya Waafrika hakuna kitu Wazungu wamekifanya kwa nia njema. Katika pita pita zangu nimekutana na historia moja yenye kuumiza sana kwa Waafrika Ila darasani hatupewi!!! Kwanini? Ni kwa sababu hatuna tena mizuka ya kuelewa historia yetu.

Je, unajua kipindi cha utumwa, kipindi cha Trans Atlantic Slave Trade, Wazungu walitumia watoto wa Waafrika kama chambo ya kukamatia Mamba? Wengi watabisha lakini huo ndio ukweli na sababu ya watu kuukataa ni kwa kuwa mtaala wa elimu haujaweka historia hii.

images%20(87).jpeg

Sina undugu na Hawa jamaa

Ujinga wa Wazungu ndo ulikuwa huu

Kipindi cha mwaka 1800 mpaka katikati ya mwaka 1900 kulikotokea uhitaji mkubwa wa ngozi za mamba. Kwani ilitumika kutengeza mikoba, viatu, mikanda, makoti pamoja na bidhaa za ngozi. Lakini ajali ya wawindaji Hawa kupoteza mikono au hata kuliwa zilikuwa nyingi wakati wa kuwinda Hawa viumbe. Hivyo, waliamua kutumia mbinu zingine mbadala kama wanyama mfano: mbuzi na kuku au bata. Lakini wapuuzi Hawa waliona ni hasara kwao hivyo kuja na njia mbadala ya kumtumia mwafrika kama chambo. Mwanzoni watoto zaidi ya 100 waliibiwa huku wazazi wakipewa taarifa kuwa watoto wamekufa. Yaani mama abebe mimba kwa miezi tisa halafu punguwani mmoja anamchukua mtoto kwenda kufanya ujinga. Inauma sana.

images%20(81).jpeg

Kwanini nisiweke kinyongo na kizazi hiki?

Baada ya kuona kuiba ni soo wakaanza kukodisha watoto tena kwa dola 2 yaani wanamchukua mtoto kisha mzazi anapewa dollar 2.

Wazungu walifanya kitu kibaya sana kwa Waafrika wengi. Ijapokuwa Wazungu wengi walipinga tuhuma hizi kwa kudai kuwa wao (Wazungu) huwatendea vyema Waafrika kuliko hata nafsi zao.

images%20(77).jpeg
Mwaka wa 1923 kulitoka makala kwenye gazeti la Time lililoripoti ukatili huu kuwa "Watoto wadogo walikuwa wanawekwa ukingoni mwa mto ili kuwavutia mamba kuja nchi kavu. Wakati huo Wazungu hujificha na huwapiga risasi mamba wakitoka kwenye maji." Gazeti hili Ndio lilileta uelewa kwa watu juu ya Ujinga huu.

Ili kuanika zaidi utumbo huu kulipatikana picha, pamoja na michoro kwenye makumbusho ya Jim Crow ambalo ndo lilitoa mwanga zaidi. Pia kuna Jamaa mmoja huko Florida alikuwa na Picha 3 ukutani zikiwaonesha watoto wa kiafrika wakiwa uchi kando ya mto huku kwa chini kukiwa na maneno "Chambo ya Mamba."

Tarehe 3 June mwaka wa 1908 gazeti jingine liliwahi kuripoti kuwa katika Zoo ya New York kulitokea ujinga huu kwa watoto wawili kufungiwa ndani ya cage au uzio wenye bwawa la mamba ili kuwafanya mamba watoke Nje ya maji. Fikiria mamba walikuwa ni zaidi ya 25.

images%20(84).jpeg

Ni ngumu sana kumuelewa mzungu kwa matendo haya
We are are different races kabisa.




images%20(88).jpeg

Usisahau kuwa wengine walikuwa ndiyo msosi wa nguruwe.

images%20(64).jpeg

Hapo mtu kapewa dollar 2

Usiku Mwema Wadau. I stand to be corrected kokote.
 
Hata sisi ni wakatili sana miongoni mwetu. Kama mchavi anaweza tengeneza ajali aue wafrika wenzake ili apate kula nyama na damu zao. Tuna ukatili zaidi ya huo mkuu. Hata kwenye siasa zetu tunauana hadharani sababu ya madaraka na vyeo. Wzungu ni watu poa sana tukijilinganisha nao. Reference: Rwanda, Burundi, Congo, Sudan, Somalia,Tz watu wanatekwa, wanauawa, wanatupwa kwenye mifuko ya sandarus huko baharini. Waafrika sisi kwa sisi hatupendani iweje mtu baki (Mzungu/Mwarabu) atupende?
 
Ni kweli kuwa hata sisi ni wakatili lakini kwenye hoja niliyoweka hapo ni maalumu kuelezea ukatili wa Mzungu ila kama mtu ataona vyema alete Uzi wenye ukatili kati ya Waafrika na Waafrika itapendeza sana.
Hata sisi ni wakatili sana miongoni mwetu,Kama mchavi anaweza tengeneza ajali aue wafrika wenzake ili apate kula nyama na damu zao ,Luna ukatili zaidi ya huo mkuu,Hata kwenye siasa ztu tunauana hadharan sbb ya madaraka na vyeo.Wzungu ni watu poa sana tukijilinganisha nao. reference: Rwanda,Burundi,Congo,Sudan,Somalia,Tz watu wanatekwa,wanauawa,wanatupwa kwenye mifuko ya sandarus huko baharin....Wafrika sisi kwa sisi hatupendani iweje mtu baki(mzungu/mwarabu)atupende?
 
Unasema wazungu na wakati huo huo unataja jarida/gazeti la Times ndio lililoibua skendo hiyo, kwa hayo tu umeshindwa vipi kujua kwamba izo ni tabia tu za watu wachache wenye tamaa haijalishi rangi ndio maana hao Times ambao pia ni wazungu walichukizwa na icho kitendo ndio maana wakakilipoti

Je, unaweza kusema hivyo kwa Watanzania wote sababu ya mauaji ya Albino ? Tafakari kabla hujaweka hoja zako labda kama uwe una maanisha jambo lingine
 
kwenye historia tunayoma imefcha mambo mengi sana na mwingi tunaosoma ni uwongo
Mmenielewa tofauti sana na niq yangu..
Kila binadamu kazaliwa na ukatili ila kwa upande huu nimeleta hoja kuhusu ukatili wa Wazungu kipindi kile ijapokuwa kuna mambo mengi sisi Waafrika tumewafanyia Wazungu nadhani hata kutuzidi!!!
Sijaweka hoja hii kuwa ndo kutufanya Waafrika tuwe bora zaidi hapana nieleweni jamani wanajamii
 
Unasema wazungu na wakati huo huo unataja jarida/gazeti la Times ndio lililoibua skendo hiyo, kwa hayo tu umeshindwa vipi kujua kwamba izo ni tabia tu za watu wachache wenye tamaa haijalishi rangi ndio maana hao Times ambao pia ni wazungu walichukizwa na icho kitendo ndio maana wakakilipoti

Je, unaweza kusema hivyo kwa Watanzania wote sababu ya mauaji ya Albino ? Tafakari kabla hujaweka hoja zako labda kama uwe una maanisha jambo lingine
Ni kweli Times walitoa ripoti lakin unadhan kwa wakati huo ndani ya Times kulikuwa na Wazungu tupu!??? Na kingine umeona tofauti ya kimiaka ya kuanza unyama huu mpaka kuripotiwa???
Kuna ukatili ambao Mzungu anafanya na anaweza kupewa support na mwenzake lakini pia anaweza asipate support.
 
Sasa kama mzazi mwenyewe bila shuruti anakubali kupokea ujira wa dollar 2 kama sehemu ya malipo kwa kazi ya kumkodisha mtoto wake mwenyewe hapo lawama ziende kwa mzungu kweli?
Wakati huo walikuwa hawajui kuandika wala kusoma!!! Mkataba unasomeka kwa lugha ya kiingereza yaani hapo anakubali lakini haelewi mtoto anakwenda wapi kufanyiwa nini!!!
 
Back
Top Bottom