Je ni kwanini tuzitumie posta, bandari na airport za tanzania?

Andy2000

New Member
May 19, 2009
3
0
JE NI KWANINI TUZITUMIE POSTA, BANDARI NA AIRPORT ZA TANZANIA? Siku chache zilizopita, kumekuwepo na malalamiko ya kutosha kuhusiana na Airport, Posta pamoja na Bandari ya Dar. Na kusema kweli, hali ya hizi idara zinatisha kiasi kwamba tunaonelea ni vyema tuukane uraia wa kitanzania na kubakia ughaibuni, au tutumie eapoti za Nairobi na Bandari ya Mombasa. Inasikitisha sana, baada ya kuangaika na kujinyima nchi za nje kutafuta riziki ili kuendeleza ujenzi wa nchi yetu kwa michango yetu midogo, mara tunapotua nchini kwetu, kuanzia kwenye kaunta za Immigration unakuta ni aibu tupu. Unaposogea kwenye customs, unakutana na watu wenye vitambi wenye macho ya tamaa, kwenye mizigo yetu ni wale manyang’au wanaoiiba bila kujali kana kwamba hawana akili nzuri. Nimekuwa nikiishi hapa Ujerumani kwa miaka 14 sasa. Kwa sabau ya kukosa makaratasi nilishindwa kurudi nyumbani hadi mwaka 2004. Lakini ingawa nilikuwa sirudi nyumbani, kila mara nilikuwa natuma mizigo midogo midogo pamoja na fedha kusaidia ndugu zangu nyumbani. Mwaka 2006 nilinunua gari lililotumika la mwaka 2001 kwa $3,800 pamoja na usafiri Ikafikia $4,800 nakutima nyumbani pamoja na nyaraka zote original. Gari ilipofika, ufisadi ulianzia TRA, TSCAN nk.. hadi kuitoa gari bandarini, nililipa kiasi cha $7,000 Inatia hasira sana, kuona kwamba kumnyima mtu rushwa inamfanya nakuhadhibu. Watu wa TRA waliponyimwa Rushwa walipandisha thamani ya gari, hapo hapo wakaanza kunifanyia mambo yawe magumu, inspection certificates wakadai ni feki, kwa hiyo TSCAN ikabidi wafanye inspection mpya na kunichaji zaidi ya $900. Niliporudi nyumbani mwaka 2007 February, kwenye msiba, hapo hapo kipawa, nilikuta mzigo wangu umefunguka, lakini sikufatilia sana kujua ni kipi hakipo ndani ya begi. Nikapitia kwa watu wa customs ambao walichomoa Camera wakasema nilipie ushuru, na thamni yake wakaiweka millioni mbili, kwa maana hiyo walitaka nilipe VAT, na 25% kwa hiyo ni kama 55% ya millioni mbili nilikataa, wakaniambia basi hawawezi kunisaidia. Ikabidi nihonge $50 ili nipewe Camera yangu ambayo nilinunua Euro 150. Kufika nyumbani, saa niliyoweka kwenye begi na viatu vipya sikuvikuta. Baada ya hapo niliamua kutokutumia Airport ya Dar es salaam tena. Natumia Nairobi na sijawahi kupata tatizo tena.. Vile vile nilipotuma gari aina ya Pick-up niliyonunua toka Japan, niliituma kupitia bandari ya Mombasa, na wala haikuchukua siku mbili kuitoa bandarini na gharama zilikuwa chini mno. Kuelekea Bukoba ilibidi nitumie mpaka wa Tarime ambako sikupata bugudha. Licha ya yote, nimetuma vifurishi vingi tu kupitia posta ya Tanzania, lakini mpaka leo havijafika, ingawa vilisajiliwa sehemu zinazotoka. Unapouliza nchi za watu wanakuthibitishia kwamba bidhaa ulizotuma zilifika Tanzania, matokeo yake unanyamaza kimya. Kwa nini hawa wezi wazidi kuachwa kufanya kazi shemu kama hizi ambapo wanawaibia na kuwanyanyasa hata wageni wanaoleta fedha za kigeni? Swali langu, je ni faida gani kuwa raia wa Tanzania, kuzitumia na kupata kero tunazozipata tukirudi nchini kwetu au tunapotuma kitu ambacho kina manufaa kwa nchi yetu. Kuna kosa gani tunapotumia Airport ya Nairobi ambayo haina bugdha au Bandari ya Mombasa isiyokuwa na Urasimu? Kwa nini watanzania wawe ni watu wa ajabu kiasi hiki, mengine vitambi vinazidi kuwa vikubwa kwa kuwaibia wanchi wakati ni shuguli zao kuwalinda? Mdau Benjamin M.. Ryayemamu Berlin, Germany Source: Michuzi
 
Huu ni umasikini wa kujitakia wenyewe, vitega uchumi tunavyo lakini vinakua mis-use kwa manufaa ya wachache. Bandari ya Dar na znz ziko katika sehemu nzuri ambazo zinaweza kuhudumia nchi nyingi za Africa ya Mashariki zisizo na bahari, ubaya wake ni wakubwa wanaoendesha uongozi wa hizi bandari. Ukiangalia bandari ya Zenj kuna (Mustafa) huyo mtoto wa mzee Jumbe utafiri ameandikiwa urithi na baba yake, jeuri na kujiona kama yeye hakuna. Ukija Dar wengine wanasamehe mizigo na magari yao bandarini hawawezi kulipia. Jee lini tutaweza kufanya biashara Halali bila kudhulumiwa wala kudhulumu serikali ? Hivi wateja wote wakikimbilia bandari za majirani si aibu hiyo. Aah lakini Ufisadi hauna Aibu Tz.
n.b na haya si bandari tu, ukienda airport, mipakani mwetu mwote mambo ni haya haya, sasa ukiwa utalipa chochote kwa wahusika utapitisha bila ya tabu tena mara nyengine bila hata wewe kupo Tz, ina maana security haipo hapo. Aassa Kheir tumeambiwa Naabi Issa AWS Atarejea kabla ya kiama huenda akaturekebishia mambo kwa umma ujao lakini kwa uongozi wetu huu, sina tamaa.
Asanteni
 
Back
Top Bottom