Je ni kwanini mheshimiwa rais haandiki jina wala saini anapotoa salamu binafsi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kwanini mheshimiwa rais haandiki jina wala saini anapotoa salamu binafsi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Richard, Apr 11, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Wakulu heshima mbele.

  Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia salamu za raisi wetu mheshimiwa Jakaya Kikwete ambazo ni ama za kupongeza, au kutoa rambirambi au kutoa pole.

  Mara nyingi mheshimiwa rais wetu amekuwa anaitumia kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kuandika na kutoa salamu hizo kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

  Kwahio kinachotokea hapo ni uchapaji wa barua hizo na mwisho inasemwa alieandika ni kurugenzi ya mawasiliano.

  Mifano ipo mingi kwa kuangalia salamu nyingi tu ambazo mheshimiwa rais ametuma katika siku za hivi karibuni na akawaachia watu wengine wamalizie.

  Je ni kwa sababu zipi mheshimiwa rais amekuwa hatii saini mwisho wa salamu zake, je anahofia nini au haoni kwamba jambo hilo sio sahihi kiitifaki?

  Naomba kuwasilisha hoja.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ipo kwaajili hiyo, na wanaandika alichoagiza...Mkuu, unataka kuwanyang'anya jamaa ulaji nini?
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata barua tu ya "paragraph" moja?
   
Loading...