FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,059
- 40,723
Leo nilikuwa naelekea Kigamboni kupitia daraja la Nyerere, baada ya kuvuka nilipita ile njia ya kushoto inayopitia jeshini, kabla sijaingia kwenye kile kipande cha lami hapo katikati kulikuwa na malori ya mafuta (fuel tankers) takriban 350 yamepaki yakisubiri kupakia mafuta kwa ajili ya kusafirisha sehemu mbalimbali mikoani na hata nje ya nchi.
Sasa nikajiuliza, baada ya hii SGR itakayogharimu kiasi cha jasho la walipa kodi bilioni elfu saba (bilioni 7,000) za kitanzania, yaani bilioni ziwe 100, alafu ziwe mara 10 yake, alafu ziwe mara saba. (7,000,000,000,000/=) kukamilika si itabidi haya maelfu kwa maelfu ya malori yanayosafirisha mafuta kwenda mikoa mbalimbali nchini pamoja na nchi za nje yapaki au yatafute shughuli mbadala kama kubeba maji safi, au hata kupakua/kunyonya vyoo vilivyo jaa, au hata kukata screpa, au hata kuuza tu.
Sasa kwakua wamiliki wa hivi vituo vya mafuta (waarabu koko) ndani na nje ya nchicndio hawa hawa wanaomiliki haya malori, je, watakubali kupaki malori yao kwa hiari yao halafu waende kutumia SGR? Mfano labda lori lake linalopeleka mafuta Mwanza lisafiri tupu hadi Dodoma kusubiri treni ya SGR ikifika ndio wafaulishe halafu ndio apeleke hayo nafuta hadi Mwanza (double handling), je, atakubali kwa hiari yake kuacha kutumia malori yake na badala yake atumia SGR?
Kuna uzi ulikuwepo hapa na niliuliza swali hili bila kupewa majibu. JE, NI KWANINI MALORI YANAFURIKA ZAMBIA HIGHWAY ILIHALI TAZARA CAPE GAUGE RAILWAY IPO? JE, NI KWANINI WAFANYABIASHARA WANAIKWEPA? NA JE, NINI KITABADILIKA KIASI HAWA HAWA WAFANYABIASHARA WASIIKWEPE SGR?