Je ni kwa nini hisa za CRDB zimeporomoka ghafla? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni kwa nini hisa za CRDB zimeporomoka ghafla?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kimbori, Jun 16, 2012.

 1. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,732
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Hisa za benki ya CRDB zimeporoka kwa takribani 35%, kutoka 180 mpaka 118 ndani ya miezi sita. Je hii ni kwa nini? Pia, je imewahi kutokea?
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Moja ya sababu ya hisa kuporomoka bei ni pale watu wanapokuwa hawana imani na management!!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hisa za CRDB Toka mwanzo hazikuchangamkiwa kama za NMB
  moja ya sababu ni status ya mnunuaji
  kumbuka NMB Ilikuwa ndo firtst time wanauza hisa
  CRDB Tayari walishauza hisa nje ya soko...
  so kuna issue ya status ya wanahisa wa mwanzo
  na hawa wanahisa thru DSE..

  ngoja wataalamu waje watufafanulie zaidi..
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  huwa sina imani kabisa na ununuzi wa hisa za makampuni ya tz, unaweza kuona kampuni ina uelekeo mzuri lkn baada ya miaka michache inafilisika kutokana na uzembe/ufisadi.. niliiamini sana general tyre, twiga cement, precision air lkn leo hii nasikia vilio kila kona
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna vilio kona ya TWIGA cement kule kuna furaha kila mwaka!! CRDB ina management isiyoaminika na wanunua hisa ama sivyo bei ya hisa zake ingepanda!!Kumbuka kununua hisa ni kuwekeza na watu wanawekeza katika kampuni inayopata faida ili wapapte gawio; kampuni itapata faida pale tu uongozi wake unapokuwa adilifu.
   
 6. n

  ndagabwene Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu mzima kuna kila sababu ya kujua mambo yahusuyo uchumi.sheria ya uchumi inasema hivi "hakuna usahihi wa mizania"kutokana na kitu kinachoitwa "demand" na "supply".hivyo suala la kushuka kwa bei au thamani ya hisa kunategemea na soko limekaaje kulingana na bei na ndio maana unashauriwa kuwa makini sana kwenye ununuzi wa hisa si vizuri kununua hisa kwa bei ya juu sana kwani ipo siku bei itashuka kama hivyo.nafikiri nimejaribu kidogo kujibu japo mi sio mtaalamu sana wa haya mambo.
   
 7. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,732
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Ngoja tusubiri Mkutano Mkuu wa Wanahisa utatoa mapendekezo gani? Kama tatizo ni Kimei? Na watatoa mapendekezo gani. Ila uwekezaji katika hisa katika kampuni za ndani unatia mashaka makubwa
   
 8. w

  wanan Senior Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  kuna tatizo kwa wanhisa wote juu ya ufahamu wa hii biashara.wanatakiwa kufahamu kuwa kununua hisa nikufanya biashara,unapokuwa kwenye hii biashara utakiwa kufahamu mambo makuu mawili
  1-usisubiri gawio tu
  2-angalia muelekea wa kampuni ambayo umenunua hisa
  vitu vya kufanya ukiona biashara inakuwa uza hisa zako nunua zingine kampuni tofauti.pia unatakiwa kufahamu vitu ambayo vinasabisha thamani ya hisa kushuka
  1.thamani ya fedha(domestic currency)
  2.uongozi wa kampuni kuwa mbovu
  3.uwekezaji mbovu unaosababishwa na uongozi
  4.busines bank(tofauti na asili yake)
  kuna vitu vingi sana kwa wanahisa vya kuangalia mwisho na nasema watanzania wanatkiwa kupewa elimu ya kutosha juu ya hisa.
   
 9. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wote nyie mnakurupuka hamna elimu ya biashara ya uwekezaji wa hisa.CRDB inatengeneza faida kubwa sana 51bilion shs mwaka 2011 na miaka ya nyuma ni faida tupu.Tatizo watu wengi wananunua hisa kwa ajili ya kupata faida kama biashara ya kuuza karanga au mahindi kutoka soko moja na kuuza wakati mwingine badala ya kuwekeza(investments),Hivyo kujikuta share zote kumwaga sokoni kuuzwa kwa wakati mmoja bila kuzingatia demand.
  Pili tatizo linaonekana lilikuwa kwenye intial price.Shares za CRDB inaonekana zilikuwa over valued na kuuzwa sh.150 kwa IPO badala ya chini ya hapo kati ya 100-120sh/.Hivyo Kampuni zilizoidhinishwa na kuhakikiwa na cmsa na dse hayakufanya kazi vizuri either kwa bahati mbaya au intentionally.Tuchukue mfano wa DHL intial price offer yao ilikuwa shs.225 na sasa ni zaidi ya shs.600 hivyo ,nmb IPO ni sh.600 sasa ni sh.880, kampuni yenye kuleta faida kwa wawekazaji ni ile ambayo IPO yake inakuwa katika discount,price inakuwa below tha market value .
   
 10. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,732
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  Nimewahi kupata habari mbaya. Makampuni mengi (kupitia Brokers) yamekuwa yakihadaa wawekezaji wa ndani, kwa kuwaambia wanunue hata kama ni over value, wao wataziuza kwa wawekezaji wa nje, kitu ambacho hakifanyiki, hivyo kuwakatisha tamaa wawekezaji wa ndani waliopewa 30% ya hisa.
  Naomba wenye uelewa wasaidie kutoa elimu kwa njia ya makala, kwa kuwa kuna watu wanakuwa na hela lakini hawajui wawekeze wapi.
   
 11. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Zimeporomoka kwa kuwa Rostam ame withdraw hela zake!!!!!!!!
   
Loading...