Je, ni kwa namna gani majina tunayoitwa au tunayojiita mitaani na mitandaoni yana mchango katika ulimwengu wa roho?

Zoë

JF-Expert Member
May 20, 2019
19,521
2,000
Habari za usiku huu wadau, kwanza kabisa poleni na mapambano ya corona. Mlio kwenye quarantine hongereni na wale wenzangu na mimi tunaoendelea kupiga misele Mungu atunusuru, naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Mara nyingi huwa nasikia watu wakisema kuwa tukiachilia mbali majina tunayopewa na wazazi wetu pindi tunapozaliwa, majina tunayoitwa au tunayojiita mitaani na mitandaoni nayo kwa namna moja ama nyingine nayo yana mchango katika ulimwengu wa roho.

Sijui pengine labda na maana ya jina ambalo mtu huitwa au hujiita nayo inachangia, kwa mfano mimi nina jina moja tu ambalo nilipewa na wazazi wangu na si zaidi. Na hata mtaani kwetu sina jina jingine ninaloitwa tofauti na hili langu ila huku mitandaoni hususani Jamii Forums nimetumia majina kadha wa kadha yenye maana tofauti.

Edelyn - Kwa wale waliokuwa wanafuatilia animations za Barbie, hili jina nililitoa kwenye Barbie in the 12 dancing princesses kati ya wale watoto 12 wa mfalme mtoto wa tano alikuwa anaitwa Edeline. Nililipenda hilo sababu ndiyo linaendana na jina langu halisi ila nilibadili herufi kidogo tu ili liwe tofauti halafu ndiyo nikalifanya permanent nickname yangu na ndipo nikaja kugundua kuwa linamaanisha "Love of God" (Upendo wa Mungu), hili jina hata wazazi wangu na baadhi ya rafiki zangu wanalijua.

Marianah - Kwa wale wapenzi na wafuatiliaji wa mambo yanayohusiana na geography hususani physical geography hili neno sidhani kama ni geni machoni au masikioni mwao, hili ni jina la the deepest trench on earth Mariana trench inayopatikana chini ya bahari ya Pacific karibu na bara la Australia. Nilijiita hivyo sababu ya kupenda sana geography na mambo yake ila nalo niliamua kuongezea herufi ili liwe tofauti kidogo, hadi nilipokuja kugundua kuwa ni neno la kilatini likiwa na maana ya "Bitter" (Chungu).

Karma - Hili ni neno la kihindi lenye maana ya Destiny/Fate (Takdiri/Hatima), kwa kirefu linamaanisha "what goes around comes back around" (you get served what you deserve). Niliamua kujiita hivi sababu mie ni muumini mkubwa sana wa hii principle ya Karma, kwamba jambo lolote unalomtendea mtu hapa duniani liwe zuri au baya basi kwa namna yoyote ile nawe lazima utatendewa kama hivyo na kama siyo wewe basi hata wanao au wajukuu zako.

Sasa hilo jina ndiyo limenifanya nianzishe huu uzi, kutokana na baadhi ya watu kutaka kujua kwanini nilijiita hivyo. Kuna mtu aliwahi nishauri nibadili hilo jina naye akaniambia kuwa majina tunayoitwa au tunayojiita mitaani na mitandaoni nayo yana mchango mkubwa sana katika ulimwengu wa roho, nikamuambia lakini kumbuka kuwa kuna Bad Karma na Good Karma nami nilivyojiita hivyo sikukusudia Bad Karma tu bali na Good Karma pia.

Akaniambia mimi naweza kuona hivyo na ninaweza kuchukulia kawaida, lakini kwenye ulimwengu wa roho kuna mengi yanatendeka hatuyajui. Ukizingatia Shetani naye hayuko nyuma katika kutufanya wanadamu tutende maovu hivyo anaweza kuamua 'kusimamia kucha' hapo kwenye Bad Karma na kufanya mambo mengi sana yatakayoniathiri maisha yangu kupitia ulimwengu wa roho bila mimi kujua, hakunielezea kwa undani nami sikutaka kumuuliza maswali zaidi ila nilikaa nikajifikiria mwisho wa siku nikaona nibadili tu.

Moana - Hili nalo kwa wafuatiliaji wa animations najua wengi wenu mtakuwa mmeshaiona animation ya "Moana", hilo jina ni neno la watu wa jamii ya visiwa fulani vinaitwa visiwa vya Polynesia vinavyopatikana huko katika bahari ya Pacific likiwa na maana ya Ocean (Bahari). Hili nalo nilijiita kutokana na mimi kuona kuwa kuna baadhi ya tabia zangu zinaendana na za Moana, mfano being a thalassophile (having too much love for the ocean) and struggling to be a 'perfect daughter'. Hili la mimi kupenda bahari kupita kiasi nahisi ni tatizo, nitaja lianzishia uzi siku nyingine.

Zoë - Hili ni neno la kigiriki likiwa na maana ya Life (Maisha au Uhai), kama mpenzi wa movies na series nami nina my favorite actors and actresses. Na hili ni jina la two of my favorite American actresses, Zoë Saldana na Zoë Kravitz na nimejiita hivi kutokana na kupenda namna wanavyoigiza na kupendelea sana kuangalia movies zao.

Sasa hili suala nimelileta kwenu wadau, hasa kwa wale waliobobea katika haya mambo ya ulimwengu wa roho mnieleweshe ni namna gani majina tunayoitwa au tunayojiita mitaani na mitandaoni nayo yana mchango unaoweza kuathiri maisha yetu kupitia ulimwengu wa roho.
 

Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
17,458
2,000
Hehe nilijua tu, haya uliza baba.

Huku kwema sijui huko
Ulijua nini tena bibie?

Unapo ongelea "Ulimwengu wa Kiroho" una maanisha nini?

Achilia mbali huku mwisho yaani aya ya mwisho umetaka wajuzi wakujuze athari ya majina na huo uimwengu wa kiroho.
 

DIVIDEND

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
1,822
2,000
Kwahiyo wewe kazi yako kubwa hapa jamiiForum ni kubadilisha tu majina.
Ulimwengu wa kiroho majina yenye nguvu ni yale tunayopewa na sio yale tunayojipa wenyewe.
Rejea kwenye Bible utaona hii kauli "nawe utaitwa, au naye ataitwa"
 

iam_cipher

Senior Member
Feb 21, 2020
123
225
Duh!
Kama ni hivo bas shetani atatafuta upande fulan mbaya kwenye maana ya id yako mpya then asimamie apo.

Ninachoona dada angu,ishi tu ukifanya mema na majina yako yote hayapo kinyume na maadili mema(nahisi ndicho kinacho. matter hata uko kwenye ulimwengu wa roho).
 

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
3,825
2,000
this has been subscribed bbygirl, Nina usingizi mpaka sioni mbele nitakuja kusoma kesho Mungu akijalia uhai.!!

Ila I swear toka nimebadili jina langu kutoka 'SweetieLee' kuwa Carleen nimeona mabadiliko mno.!!

Na nilikuwa kanisani while napata wazo la kubadili, mpaka Leo sijui ni kwanini.! Nikaliombea jina hili ndiyo nikajiita, na kweli mambo mengi sana maishani mwangu yakabadilika..!! Sitamani mtu aniite SweetieLee hata kwa bahati mbaya.!

Bby C'ssy, kuna muunganiko mkubwa sana wa kiroho na haya majina tunayojiita.!!
 

Super Villain

JF-Expert Member
Jan 2, 2019
8,485
2,000
I'd za JF tunatumia tu kwa sababu tu yakuweka kamipaka tu lakini wengine tunamajina yetu mazuri tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom