Je ni kwa kiasi gani Watanzania wanahamasishwa kuisoma Rasimu ya Katiba?

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
252
Toka Rasimu ya katiba itolewe kuna swali nimekuwa najiuliza sana.....''' Je ni kwa kiasi gani watanzania wamekuwa wakihamasihwa kuisoma ili waweze kuchangia vizuri matahalani kuikosoa au kushauri mambo ya kuongezaaa? Ukitazama au kusikiliza vyombo vya habari utashangaa kuna mambo huwa yana hamasishwa kwa namna ya pekee tofaauti na swala muhimu kama hili la katiba!!! Mathalani kampeni ya ''maleria haikubaliki'' hiii karibu kila chombo kiliitangaza ,viongozi wakashadidia n.k, afu kuna haya mambo ya mipira utasikia sijui saidia serengeti boys mara taifa stars hoyee......shangilia stars n.k yani kila siku ni hayo lakini sisi tusio wapenzi wa mipira tunashangaa kunani? maana yanakuwa ni matangazo mengisana....Kiasi tunahamasika na sisi hebu tukaone haya yanayotangazwa saaana.....Hii ni tofauti na Rasimu ilivyotangazwa....! hakuna uhamasishaji kabisa...yamebaki mabishano tu....JE NI KWAMBA hakuna nia ya DHATI kwa viongozi wetu juu ya Rasimu hii au ni nini kinasababisha hili? Naombeni mchango wenu.
 
Back
Top Bottom