Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
- Thread starter
- #21
Uswahilini tuna msemo usemao "Mkamatwa na Ngozi ndiye mwizi".
Hapa kwa ushahidi wa kimazingira unamwonesha moja kwa moja Kupaza kuwa ndie mhusika, lakini kuna kitu/vitu vyengine hapa vinanuka ambavyo vinaweza kumfanya Kupaza asiwe mhusika, lakini kutoka na haya mazingira yalivyosukwa, iwe ni kweli au la...Kupaza kanaswa.
Mnakumbuka kisa cha Ijumaa iliyopita ambapo Asha Mkwizu alimuua Mwanahamisi Happiness?
Tukio kama hili la Mkwizu vs Happiness ndilo linalozoeleka kutokea, na sio baina ya wananwake tu bali hata baina ya wanaume, kuwa yule "anayekuibia mpenzi wako" ndie mkosa na ndiye anayestahiki adhabu, na kumwacha upande mwizi wa kweli. Katika kesi ya Mkwizi na Happiness, mkosa alikuwa Dr Hauli lakini Mkwizu akamuua Happiness? Je hakuna uwezekano katika kesi hii kuwa Bi Shari alimwua Mwivano kama kulipiza kisasi kwa
a) Kunyang'anywa mume. b) Uchungu wa fadhila za punda za Kupaza na Mwivano.
Hakuna uwezekano pia mtu Mzungu aliyekuweko mtoni alikuwa msaidizi wa Bi Shari? Polisi wakati wowote walilifikiria hili? Tusisahau pia kuwa kuna mamia ya maelfu ya kesi Marekani ambapo mara nyingi "mtu mweusi ndiye "mbaya/adui" katika filamu?
Nilikuwa nasubiri mtu anisaidie kudadavua kama ulivyofanya..............Ahsante sana, kwani sikutaka kuwa na kiherehere cha kusherehesha mkasa huu mara tu baada ya kumaliza kuufasiri, nilitaka wasomaji wadadavue na kuweka mawazo yao humu kwa uhuru kabisa...............
Hebu tujiulize wote...........
1. Mama Shari Goss alikuja nchini kama mmishenari na kukutana na Peter Kupaza
2. Waliamua kuoana na kwenda kuishi wote Ughaibuni (Ikumbukwe kwamba kwa Mbongo hiyo ni bahati sana kupata mzungu na tiketi ya kuishi ughaibuni, lakini kwa Mzungu pia ni bahati maana sarakasi za mapenzi ya wao kwa wao zimewashinda na kupata Mbongo ni faraja na tulizo la moyo......Kumbukeni tunayo sifa ya ukarimu kwa wenzetu)
3. Kupaza kamwita dada yake binamu kwenda kuungana naye huko Majuu ili kujifunza kiingereza kabla ya kujiunga na chuo cha uuguzi
4. kashfa ya ujauzito wa kaka binamu unasambatisha ndoa ya Kupaza na mkewe Shari Goss......(Kumbukeni huyu Bwana alipata bahati hiyo ya kuishi na kufanya kazi ughaibuni kwa sababu ya ndoa yake na Shari Goss)
5. Kupaza akahamia kwenye eneo lingine na kuishi peke yake huku dada yake Mwivano akiishi Hostel na marafiki zake
aliokuwa akisoma nao.................
6. Si kwamba Kupaza aliona ni busara kumweka dada yake mbali na yeye ili kuepuka kuchomewa utambi kwa Polisi na Shari Goss baada ya Viza ya dada yake ya kuishi nchini humo kuisha muda wake?
7. Je Shari Goss anaweza kuishi kwa amani kweli, hasa baada ya ndoa yake kusambaratishwa na dada binamu wa mumewe?
8.Kwa nini Shari Goss awe wa Kwanza kuitambua sura ya Mwivano na kuripoti Polisi
9. Je ni visa vingapi vinavyofanana na hiki vinavyowapata Waafrika kutoka Afrika wanapotengana na wake zao au waume zao Wazungu?
10. Kisa cha mzungu kule mtoni nacho kinaacha maswali bila majibu.....................
Nimewaza kwa sauti tu..................................