Je, ni kuna ulazima wa kuwatoza kodi wananchi wanyonge watumiapo mitandao ya Kijamii?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Tumepata kusikia ndugu Andrew Kisaka (Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Mawasiliano TCRA) akibainisha kuwa kuna haja ya watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania waanze kutozwa kiwango fulani cha pesa ili Mamlaka ya TCRA iweze kugharamia huduma ya kudhibiti Maudhui yanayojadiliwa mitandaoni.

Yaani (kwa mfano) kufika hatua ya watumiaji wa:-
Twitter (walipe 15,000Tsh kwa mwezi)
Instagram (walipe 10,000Tsh kwa mwezi)
Facebook (walipe 5,000Tsh kwa mwezi)

Ili tu waweze kuwa na pesa ya kutosha kusimamia maudhui mitandaoni. Kwani pesa za kodi hazikidhi kufanikisha shughuli yao ya kusimamia maudhui mpaka wananchi wa tanzania watozwe upya? Na itakuwaje kwa wale wasio na uwezo wa kulipa kiasi hiko cha pesa?

2472937_Capture.png
 
Hahahaa kila mmoja lazima aguswe kwa namna yake😄😄😄😄😄

First they came for the Socialists, and I did not speak out—
Because I was not a Socialist.

Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out—
Because I was not a Trade Unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.

— Martin Niemöller
 
Nchi zingine zinawezaje kusimamia? au wamekuja na hili ili kumfurahisha Rais wetu ilihali wananchi wengine wanaumia ? mbona kuna vijana wengi tu wanatafuta kazi na wanaweza kufiti nafasi yao. Wao waache kazi tutafute vijana ambao watakuja na mbinu mbadala ya kuthibiti hilo.
 
Kwahiyo yale makusanyo ya tril 1 kwa mwezi, na hata uchumi wa kati ni porojo!
 
Kwani hiyo mitandao watu wanaitumia bure? Si kuna malipo ya data"MB" ambazo wanatumia? Na hizo data si zinalipiwa kabisa?

Maoni yangu:
Wakae waelewane na makampuni ya mitandao ya simu ambayo tunanunua data huko, waelewane namna bora ya kugawana mapato

Pia wakiweza wawasiliane na watu wa hizo applications kama Facebook, Twitter na Instagram waone namna ya kugharamia process zao za kulinda maudhui yanayopakiwa katika applications zao hizo

Mnyonge mwisho atanyongwa sasa
 
Hakuna watu wajinga kama walioko tcra hawajui hata kwanini wako pale
Unajua kuna mengi wanafanya ya kijinga.sana, hawana ufatilialija service provideer jinsi wanajiamulia mambo kiholela.

Watu kuibiw fedha ,ktk hii mitandao, kuibiwa vifurushi wengi wanalalamik nmenunua kifurush ndan, ya dk mbili sijatumia naambiw kimeisha.

Ongezeko la bei la mawasiliani, unaamka unakuta tu,kifurush kimeongezwa ghalama.

Mbali na hayo, mawasilian yangu, wanakata fedha si bure, kwanini wanisumbue na matangazo yao kila muda,ukiwa unataka kuongea na mtu. Umelala usiku ,unasikia SMS inaingia,unajua jambo la msingi, uangalie ,Unataka matangazi ya miito, au ofa za ku bet, wakat hata hujui na hujawah ku bet.

Why, ninunue kifurush, unilazimsh nitumie ndan ya wiki, mwezi au siku, wakt nmetoa hela yangu, ilitakiw kifurush ,ni kama bidhaa ingine, nannua,nitumie Kikiisha ndiio kimekwisha, tuachane na expire time.

Naona TCRA wana mbana sana, mtumiaji mdogo,kuliko mambo ya ovyo wanayo fanyiwa. Hata leo,ukiw na shida,ukatak msaada wa TCRA utarushw chenga ushangae, hakuna msaada wanao toa, na bado wanataka wachukue fedha...mbayaaaaa
 
Wanataka kudhibiti wana CHADEMA kwani wanatumia sana social media kuliko tv ambazo zinakatazwa kuonesha habari za vyama vingine.
 
Wanao uwezo wa kutoza hizo kodi basi kama VAT tu inawapasua kichwa he hii kodi ya anonymous wataiweza
 
Wanao uwezo wa kutoza hizo kodi basi kama VAT tu inawapasua kichwa he hii kodi ya anonymous wataiweza
 
Back
Top Bottom