Je, ni kitabu gani kimekubadili mtazamo juu ya historia ya Afrika na mtu mweusi kwa ujumla?

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
518
901
Habari zenu wadau wa jukwaa hili. Leo ningependa kushea na nyinyi kuhusu hiki kitabu ambacho tangu nikisome takribani miaka kadhaa hivi wakati nipo chuo kiliweza kubadili mtazamo wangu kwa kiasi kikubwa sana kuhusiana na historia ya Africa na mtu mweusi kwa ujumla.
Kitabu hiki kinaitwa stolen legacy, mwandishi wa kitabu hiki ni George Jemes, G.M kutoka nchini Guiyana.

Mwandishi wa kitabu hiki anaelezea jinsi kwa miaka mingi nchi za magharibi zilivyoweza kuficha ukweli kuhusu mwanzo wa elimu ya sayansi na sanaa katika maendeleo na ustaharabu wa mwanadamu, mwandishi anaelezea kwa muda mrefu tumekua tukifundishwa kua wagiriki na waroma ndio chanzo cha elimu ya sayansi na sanaa kitu ambacho sio kweli.
Mwandishi anaelezea jinsi gani wanafilosofia wakigiriki walivyo copy na kupaste elimu ya wamisiri ambayo ilijulikana kama Egyptian mystries na kuigeuza kua Greece philosophy ambayo leo hii tunafundishwa mashuleni na credit wanapewa wanafilosofia kutoka Ugriki kama ndio waanzilishi wa elimu hii.

Mwandishi anaelezea kua wamisiri katika ulimwengu wa kale ndio waliokua wamepiga hatua katika mfumo wa kielimu na dini, Wamisiri walibobea sana katika nyanja za sayansi na sanaa, ambapo waliweza kujifuza elimu kuhsu mambo ya anga, Astronomy na cosmology, pia walibobea katika mahesabu, fizikia, kemia na mambo ya sanaa kwa ujumla.

Pia mwandishi anaendelea kuonyesha na kutujuza kua watu wa zamani kutoka mataifa mbali mbali waliweza kwenda Misri kwa ajili ya kuweza kujipatia elimu yao. Wanafilosofia wengi wa kipindi hicho wakiwemo wagriki walikwenda misri na walifundishwa na walimu kutoka misiri, wanafilosofia kama Thales, Pythogras, Democratius, plato wote walikanyaga misri kwa ajili ya kuchukua elimu yao.
Kwa mahana hiyo theory zote unazofundishwa darasani kuhusu hawa jamaa jua wao sio wahanzilishi bali walifanya kukopi na kupaste kutoka kwa wamisri.

Pia mwandishi akagusia kuhusu jinsi gani wagriki walivyoweza kuiba vitabu vya maarifa mbali mbali kutoka misri wakati Alekizanda the great alipovamia na kuiteka misiri, ambapapo alibadili jina mji wa Thebes na kuita jina lake Alexndria, pia walivunja makitaba kubwa iliyokua katika mji huo na kuchukua vitabu vyote ambapo walienda kufungua makitaba mpya mjini Athens Ugiriki na Aristoto ndio akapewa jukumu la kuisimamia makitaba hiyo.

Kw ufupi tu kwangu mimi hiki ndio kitabu kilicho weza kubadili mtazamo wangu kuhusu mambo yote niliofundishwa shuleni, karibuni na nyinyi mtuambie ni vitabu gani vimewza kubadlili mtazamo wako kuhusu historia ya Africa au kutilia mashaka historia tunayofundishwa darasani

Kwa wale wapenzi wa kusoma vitabu unaweza uka PM

PSX_20200409_104924.jpg
 
msomaji nimepita hapa nasubili comment za wadau🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Pia mwandishi anaendelea kuonyesha na kutujuza kua watu wa zamani kutoka mataifa mbali mbali waliweza kwenda Misri kwa ajili ya kuweza kujipatia elimu yao. Wanafilosofia wengi wa kipindi hicho wakiwemo wagriki walikwenda misri na walifundishwa na walimu kutoka misiri, wanafilosofia kama Thales, Pythogras, Democratius, plato wote walikanyaga misri kwa ajili ya kuchukua elimu yao.
Kwa mahana hiyo theory zote unazofundishwa darasani kuhusu hawa jamaa jua wao sio wahanzilishi bali walifanya kukopi na kupaste kutoka kwa wamisri.
msomaji nimesoma upya nikarudi tena kujibu lengo hasa la kudadavua yote haya ni nini sioni maana ya haya mambo yote basi ikia mtakubaliwa kua ninyi ndio waanzilishi mtapata faida gani au elimu waliyo nayo hadi sasa itahama kwao kama jibu ni hapana tuache kufanya hivyo papania nafasi uliyo nayo ili kujiongeza zaidi kielimu sio kusema sisi ndio waanzilishi ilihali huna kitu mtanisahe @sahanpas1
 
We unafikiri kwamba hakuna athari tunayoipata kutokana na kutokujua historia yetu, unyonge wote na dharau ambazo watu weusi tunafayiwa unatokana na kutokufahamu historia yetu, historia tunayofundishwa darasani imejaa propaganda na kuwatukuza wazungu kwamba ndiyo wamefanya mambo makubwa kumbe ni wazee wa copy na kupesti kutoka jamii nyingine alafu wanapewa crediti kama wahanzilishi. Ili kuweza kushinda vita vya utumwa wa kifikra hatuna budi kujua historia yetu kisha kujifunza historia ya jamii nyingine
 
Ngonjera zile zile, za sisi ndio wavumbuzi, tuna akili zaidi, wazungu wameturudisha nyuma, n.k. Swali la kujiuliza tu mtu mwenye akili ndio anakuwa na superior teknolog na anaenda kwenye ardhi za mbali kufanya conquest, badla yake Waafrika walibaki hapa hapa mwarabu akaja na kuwafanya watumwa kwa miaka karibu 1000, mzungu akaja akawafanya watumwa pia, kisha akawatawala
 
Dunia ina mengi kama wasemavo watu pori,ndo maana mi nkishika mpira kinachofata goli
 
Ngonjera zile zile, za sisi ndio wavumbuzi, tuna akili zaidi, wazungu wameturudisha nyuma, n.k. Swali la kujiuliza tu mtu mwenye akili ndio anakuwa na superior teknolog na anaenda kwenye ardhi za mbali kufanya conquest, badla yake Waafrika walibaki hapa hapa mwarabu akaja na kuwafanya watumwa kwa miaka karibu 1000, mzungu akaja akawafanya watumwa pia, kisha akawatawala
kabla ya waarabu na wazungu kuitawala Africa je unajua kwamba watu weusi pia walishaitawala ulaya na mashariki ya kati kwa takribani miaka 700 na wakapeleka elimu by that time wazungu walikua hawajui kusoma wala kuandika na walikua wakihishi mapangoni #johnny sack
 
Ha ha ha, halafu ikawaje?
 
Ha ha ha, halafu ikawaje?
unajua ya kua kila kutu kina wakati wake leo wazungu kua mbali kimaendeleo haina mahana kua jamii nyingine hazikuawai kupiga hatua katika suala zima la maendeleo
Na ukiangalia nchi nyingi za magharibi zimenza kua na mendeleo makubwa kuanzia karne ya 16 ukirudi nyuma autona historia ya mahana ya hawa watu weupe
 
Sawa, naamini story yako inatuambia kuwa baadae waafrika tutarudi juu.
 
bila kubadili fikra zetu itakua ni ndoto kwa sisi waafrika kua na maendeleo makubwa, ambayo yataletwa na sisi wenyewe pale tutakapojifunza kuanza kufikiri kama binadamu aliye huru na sio Kufikiri kama watumwa.
 
Ngonjera zile zile, za sisi ndio wavumbuzi, tuna akili zaidi, wazungu wameturudisha nyuma, n.k. Swali la kujiuliza tu mtu mwenye akili ndio anakuwa na superior teknolog na anaenda kwenye ardhi za mbali kufanya conquest, badla yake Waafrika walibaki hapa hapa mwarabu akaja na kuwafanya watumwa kwa miaka karibu 1000, mzungu akaja akawafanya watumwa pia, kisha akawatawala

Unacho paswa ni kutambua ukweli kama utakusaidia fuatilia vema rithisha kizazi Chako ile ilio asili yako.Pia jambo dogo tu hujui ni kwamba kuanzia mababu zako walitengenezwa katika kudumaza ufikiri wao na ndicho umerithi
 
we ndio hujui, fikra dumavu ndio hizi za kujidangabnya we ni superior wakati sivyo, kujirtambua ni kuelewa udhaifu wako na uimara wako kisha kutumia uiamara wako kufidia zile kasoro zinazoletwa na udhaifu wako, sio kujidanganya..
 
The African origine of civilization is it moth or reality by cheik anta diop
 
kabla ya waarabu na wazungu kuitawala Africa je unajua kwamba watu weusi pia walishaitawala ulaya na mashariki ya kati kwa takribani miaka 700 na wakapeleka elimu by that time wazungu walikua hawajui kusoma wala kuandika na walikua wakihishi mapangoni #johnny sack
Watu weusi wana nyodo hawo!
 
Habari zenu wadau wa jukwaa hili. Leo ningependa kushea na nyinyi kuhusu hiki kitabu ambacho tangu nikisome takribani miaka kadhaa hivi wakati nipo chuo kiliweza kubadili mtazamo wangu kwa kiasi kikubwa sana kuhusiana na historia ya Africa na mtu mweusi kwa ujumla.
Kitabu hiki kinaitwa stolen legacy, mwandishi wa kitabu hiki ni George Jemes, G.M kutoka nchini Guiyana.

Mwandishi wa kitabu hiki anaelezea jinsi kwa miaka mingi nchi za magharibi zilivyoweza kuficha ukweli kuhusu mwanzo wa elimu ya sayansi na sanaa katika maendeleo na ustaharabu wa mwanadamu, mwandishi anaelezea kwa muda mrefu tumekua tukifundishwa kua wagiriki na waroma ndio chanzo cha elimu ya sayansi na sanaa kitu ambacho sio kweli.
Mwandishi anaelezea jinsi gani wanafilosofia wakigiriki walivyo copy na kupaste elimu ya wamisiri ambayo ilijulikana kama Egyptian mystries na kuigeuza kua Greece philosophy ambayo leo hii tunafundishwa mashuleni na credit wanapewa wanafilosofia kutoka Ugriki kama ndio waanzilishi wa elimu hii.

Mwandishi anaelezea kua wamisiri katika ulimwengu wa kale ndio waliokua wamepiga hatua katika mfumo wa kielimu na dini, Wamisiri walibobea sana katika nyanja za sayansi na sanaa, ambapo waliweza kujifuza elimu kuhsu mambo ya anga, Astronomy na cosmology, pia walibobea katika mahesabu, fizikia, kemia na mambo ya sanaa kwa ujumla.

Pia mwandishi anaendelea kuonyesha na kutujuza kua watu wa zamani kutoka mataifa mbali mbali waliweza kwenda Misri kwa ajili ya kuweza kujipatia elimu yao. Wanafilosofia wengi wa kipindi hicho wakiwemo wagriki walikwenda misri na walifundishwa na walimu kutoka misiri, wanafilosofia kama Thales, Pythogras, Democratius, plato wote walikanyaga misri kwa ajili ya kuchukua elimu yao.
Kwa mahana hiyo theory zote unazofundishwa darasani kuhusu hawa jamaa jua wao sio wahanzilishi bali walifanya kukopi na kupaste kutoka kwa wamisri.

Pia mwandishi akagusia kuhusu jinsi gani wagriki walivyoweza kuiba vitabu vya maarifa mbali mbali kutoka misri wakati Alekizanda the great alipovamia na kuiteka misiri, ambapapo alibadili jina mji wa Thebes na kuita jina lake Alexndria, pia walivunja makitaba kubwa iliyokua katika mji huo na kuchukua vitabu vyote ambapo walienda kufungua makitaba mpya mjini Athens Ugiriki na Aristoto ndio akapewa jukumu la kuisimamia makitaba hiyo.

Kw ufupi tu kwangu mimi hiki ndio kitabu kilicho weza kubadili mtazamo wangu kuhusu mambo yote niliofundishwa shuleni, karibuni na nyinyi mtuambie ni vitabu gani vimewza kubadlili mtazamo wako kuhusu historia ya Africa au kutilia mashaka historia tunayofundishwa darasani

Kwa wale wapenzi wa kusoma vitabu unaweza uka PM

View attachment 1413676
Ni jambo jema kwamba ulisoma hicho kitabu ndio ukayajua hayo. Kwa mimi niliyesoma North African History nikiwa High School na baadae chuoni, hii sio habari ngeni kwangu.
 
Habari za Leo kiongozi ,samahani naomba unisaidie kupata kitabu cha STOLEN LEGACY ,nimependa jinsi ulivyokielezea kuhusu waafrica wa misri
 
Back
Top Bottom