Je, ni kisasi kutoka Marekani au matukio tu?

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Baada ya CIA kutoa ripoti yao kuhusu ushiriki na ushawishi wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani, Rais Obama alisema ni lazima Marekani itachukua hatua dhidi ya Urusi katika namna wao watakavyoamua.

Je haya yanayotokea Urusi ni sehemu ya hatua hizo au ni matukio tu yametokea kukaribiana kwa pamoja.

Ndani ya masaa 24, yametokea matukio matatu ya kuihuzunisha Urusi.

1.Ndege ya Wizara ya mambo ya ndani ilindondoka na kuuwa watu takriban 27, japo ripoti baadae zilibadili idadi ya vifo huko Siberia

2. Raia takribani 50 wa wamefariki baada ya kilevi/pombe kuwekewa methanol ndani yake huko Siberia

3. Kuuawa kwa Balozi wa Urusi nchini uturuki, tena mda mchache kabla hawajakutana na kwa pamoja Uturuki, Iran na Urusi kuzungumza kuhusu Syria. Ukiangalia hawa wanamsapoti Assad kwa maslahi ya nchi yao hasa Urusi.

Ni Conspiracy au Coincidence?



Screenshot_2016-12-19-21-52-19.png
Screenshot_2016-12-19-21-53-09.png
Screenshot_2016-12-19-22-08-29.png

 
Labda hilo la tatu. Lakini huwa hawalipi wizi wa mitandao kwa mauaji. Wataiba au wamesha iba na wao kwenye mtandao
 
Haya sasa. Na hili roli lililoleta kasheshe berlin ni CIA au?

Vingine huwa ni ugaidi tu. Urusibwapo vitani hivyo kuuwawa kwa balozi ni sehemu ya vita.

Angalieni breaking news CNN
 
Haya sasa. Na hili roli lililoleta kasheshe berlin ni CIA au?

Vingine huwa ni ugaidi tu. Urusibwapo vitani hivyo kuuwawa kwa balozi ni sehemu ya vita.

Angalieni breaking news CNN
Kwani inashindikana ujasusi kutumia ugaidi? Uliwahi kujiuliza kwa nini Urusi alivyoanza kuipiga ISIS Marekani alikuja juu sana na figisu kibao.
 
Putin":" Huu ni mpango mahususi wa kudhoofisha amani nchini Syria

Putin:"tunataka kufahamu muuaji alitumwa na nani


**kijembe kakitoa hapa
 
Back
Top Bottom