Je, ni kampuni ipi inaongoza kwa huduma bora za kuagiza magari ya nje hapa Tanzania

Autocom wapo vizuri,gari zao hazijatembea km nying na pia ni nafuu kulinganisha na makampuni mengine
 
MIMI HUWA NAAGIZA AUOREC JAPAN GARI ZAO ZIPO VIZURI INGAWA NAONA MEMBERS WENGINE WANALALAMIKA BEI YAO KUWA JUU KULIKO MAKAMPUNI MENGINE. JARIBU AUTOREC NAAMINI WAPO SAWA.
 
MIMI HUWA NAAGIZA AUOREC JAPAN GARI ZAO ZIPO VIZURI INGAWA NAONA MEMBERS WENGINE WANALALAMIKA BEI YAO KUWA JUU KULIKO MAKAMPUNI MENGINE. JARIBU AUTOREC NAAMINI WAPO SAWA.
Kampuni yenye magari bei juu lakini yenye quality ni japanesevehicles.com IST ya 2005 USD 3100 lakini inaquality nzuri mpaka unashangaa
 
Nimewahi kuagiza kupitia Beforward mara tatu mimi binafsi na mara mbili niliwasaidia jamaa zangu. Wako vizuri sana. Tatizo la watu wengi wanaangalia bei. ukiona gari lina bei rahisi ujue ni la zamani zaidi au limetembea Km. nyingi.

Pia unavyoangalia picha za gari chunguza zaidi na unaweza kuwaomba wakutumie picha kwa sehemu ambayo una mashaka nayo. Mara nyingine picha zao huonesha na sehemu yenye hitlafu hasa katika body. Kwa ujumla picha zao sio fake. Pia unaweza ku-negotiate bei.

Kuna jamaa yangu pia aliwahi kuchagua gari kwenye mtandao, na alipoliagiza baada ya ukaguzi akaambiwa gari hilo halifai. Maana yangu magari yao hukaguliwa kwa umakini zaidi ingawa hata makampuni mengine hukaguliwa ili gari linaloingia nchini liwe katika kiwango kinachokubalika.

Unaweza kupata gari lako ndani ya mwezi mmoja kulingana na ratiba ya meli. Movement zote unapata mtandaoni, tangu siku wanayofanya ukaguzi, linavyopakiliwa melini, siku ya kuondoka na siku ya kufika mara nyingi tangu meli iondoke bandarini ni siku 21.
Sijajaribu makampuni mengine kwani nimeridhika na hawa jamaa.
 
Kwa maelezo ya wadau mlio wengi nimeona makampuni yanayoongelewa sana ni kati ya SBT na Befoward..but nani ni bora zaidi kati yao
 
Nataka ni import gari mwenyewe mara ya kwanza nilipanda yard ila yard wengi wahuni wanaweza kukuuzia gari mtu katumia bongo anapeleka yard gari imenisumbua nimeuza nataka ni import mwenyew sahvi.

Ukicheki sbt na Beforward utaona hiz campun 2 zinautofauti Beforward naona gari zao zipo vzr milleage ndogo tofauti na sbt hta bei zao pia no rafiki ukija sbt hawa jamaa gari zao nying zmeenda milleage.

Siajua kwa realmotors na tcv mwenye utaalam na hawa jamaa aje atusaidie
 
Nataka ni import gari mwenyewe mara ya kwanza nilipanda yard ila yard wengi wahuni wanaweza kukuuzia gari mtu katumia bongo anapeleka yard gari imenisumbua nimeuza nataka ni import mwenyew sahvi...

Kama mfuko wako uko vizuri wachek Trust japan,hawa jamaa nilinunua gari last year january mpaka sasa sijawahi kubadili chochote zaidi ya Engine oil nani gari ya kazi.
 
Back
Top Bottom