Je ni Jinsi Gani serikali inaweza kuzibiti Mapato yake ya ndani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni Jinsi Gani serikali inaweza kuzibiti Mapato yake ya ndani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Serendipity, Dec 20, 2009.

 1. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wana JF, Huwa najiuliza kila siku jinsi serekali inavyo poteze mapato yake ya kila siku lakini, Lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti hili. Kilicho nisukuma kuandika hapa,ni wito uliotolewa na Raisi JK wa JMT akiwasihi watumishi waache udokozi sehemu zao za kazi! Unaweza kusoma zaidi kwenye link hii: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16747
  Mimi nadhani, kama serikali ipo siriazi na inataka kweli kuzibiti mapato yake basi ingeiga mifanao ya serikali nyingine katika nchi zilizoendelea jinsi wanavyo dhibiti cash collection katika idara za serikali.
  Mfano, Tanzania,mathalani pale wizara ya ardhi, utakuta cashier anakusanya zaidi ya milioni 30 kwa siku, mshahara wake si zaidi ya laki 4 kwa mwezi, na utakuta huyu cashier hajafanya kazi zaidi ya miaka 3 lakini ameweza kujenga nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 200!(Ushaidi ninao)
  Pili, pale TRA, Kuna vijana wadogo lakini wana hela ya kufa mtu! zote wanazipata kwa njia zisizo halali!
  Tatu, Pale Kigamboni ferry, wale wanaokusanya hela madirishani pamoja na ma- supervisor wao(sio wale wanaochana ticket), wote mishahara yao haizidi laki 3 kwa mwezi lakini wana majumba ya kifahari na mali nyingine kibao, zinazozidi kipato chao halisi hata zaid ya mara 3000(Ushaidi ninao, nawe waweza kuchunguza hili!)
  Nne,Ubungo Bus terminal;Hili lilisha semwa sana na kudhibitishwa na CAG.
  Tano, Kmpuni ya NPS inayojihusisha na parking fees mjini DSM,(Hili halijajadiliwa sana, ila nilisha toa hoja hii, ila wna JF hawakuchangia, Lakini ushahidi ninao!)
  Hayo ni maeneo machache tu ambayo nimeweza kuya point kutokana na uzoefu wangu!
  Naomba ieleweke kwamba sina chuki binafsi na wahusika wanaofaidi(ambao wengine ni marafiki zangu, lakini nina uchungu zaidi na maendeleo ya taifa kuliko personal developments!)

  sugessted SOLUTION
  Katika maeneo yote nyeti, yanayohusisha ukusanyaji wa hela, serekali itafute njia mbadala, baada ya kukusanya CASH money basi watumie Bank draft au Postal Money order au kutumia Laser cards(Kama TEMBO CARD ya CRDB) ili kudhibiti hawa ma-cashier kucheza na makaratasi!
  Kwanjia hii serekali itadhibiti mapato yake kwa asilimia 100%
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...basi mimi nilidhani anazungumzia waajiriwa 'vibaka' tu kwenye mahoteli nchini... Majuzi tu 'vibaka' hao walinikomba mali zangu kadhaa pale Lamada Apartments na hoteli mojawapo maarufu mjini Zanzibar!.
  ...Mabingwa wa lugha wanasema samaki huozea kuanzia kichwani, kama wizi serikalini unaanzia kwa vigogo waliopewa dhamana ya uongozi wa nchi, si ajabu 'samaki n'changa' wakajitetea kwa msemo wao marufu 'tukale wapi!'

  Accountability inaanzia juu kurudi chini, sio chini kupanda juu. Haya mambo yalianzia kipindi kile wenye uwezo wachache walipokuwa wanapewa na 'walioshika mpini' vi-memo vyenye amri ya kutatuliwa shida zao na watendaji ngazi ya kati.   
 3. Kariakoo

  Kariakoo Member

  #3
  Dec 26, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wawe na independent AUDITING
   
Loading...