Je ni Jinsi Gani serikali inaweza kudhibiti Mapato yake ya ndani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni Jinsi Gani serikali inaweza kudhibiti Mapato yake ya ndani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serendipity, Dec 20, 2009.

 1. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wana JF, Huwa najiuliza kila siku jinsi serekali inavyo poteze mapato yake ya kila siku lakini, Lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti hili. Kilicho nisukuma kuandika hapa,ni wito uliotolewa na Raisi JK wa JMT akiwasihi watumishi waache udokozi sehemu zao za kazi! Unaweza kusoma zaidi kwenye link hii: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16747

  Mimi nadhani, kama serikali ipo siriazi na inataka kweli kuzibiti mapato yake basi ingeiga mifanao ya serikali nyingine katika nchi zilizoendelea jinsi wanavyo dhibiti cash collection katika idara za serikali.
  Mfano, Tanzania,mathalani pale wizara ya ardhi, utakuta cashier anakusanya zaidi ya milioni 30 kwa siku, mshahara wake si zaidi ya laki 4 kwa mwezi, na utakuta huyu cashier hajafanya kazi zaidi ya miaka 3 lakini ameweza kujenga nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 200!(Ushaidi ninao)

  Pili, pale TRA, Kuna vijana wadogo lakini wana hela ya kufa mtu! zote wanazipata kwa njia zisizo halali!

  Tatu, Pale Kigamboni ferry, wale wanaokusanya hela madirishani pamoja na ma- supervisor wao(sio wale wanaochana ticket), wote mishahara yao haizidi laki 3 kwa mwezi lakini wana majumba ya kifahari na mali nyingine kibao, zinazozidi kipato chao halisi hata zaid ya mara 3000(Ushaidi ninao, nawe waweza kuchunguza hili!)
  Nne,Ubungo Bus terminal;Hili lilisha semwa sana na kudhibitishwa na CAG.

  Tano, Kmpuni ya NPS inayojihusisha na parking fees mjini DSM,(Hili halijajadiliwa sana, ila nilisha toa hoja hii, ila wna JF hawakuchangia, Lakini ushahidi ninao!)
  Hayo ni maeneo machache tu ambayo nimeweza kuya point kutokana na uzoefu wangu!

  Naomba ieleweke kwamba sina chuki binafsi na wahusika wanaofaidi(ambao wengine ni marafiki zangu, lakini nina uchungu zaidi na maendeleo ya taifa kuliko personal developments!)

  SUGESSTED SOLUTION
  Katika maeneo yote nyeti, yanayohusisha ukusanyaji wa hela, serekali itafute njia mbadala, baada ya kukusanya CASH money basi watumie Bank draft au Postal Money order au kutumia Laser cards(Kama TEMBO CARD ya CRDB) ili kudhibiti hawa ma-cashier kucheza na makaratasi!
  Kwanjia hii serekali itadhibiti mapato yake kwa asilimia 100%
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Unajaribu kupendekeza utatuzi wa tatizo; wakilitatua hilo tatizo wao watafanikiwaje?
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  TRA ni mabowara? unaenda kulipa kodi ya serikali inabidi uhonge? shame foleni, wafanyakazi hawana ari, aibu tupu kwa nchi ..I wish you Director general aone aibu..akusanye kodi kwa kuboresha utendaji ili walipa kodi wasiwe na sababu ya kutolipa..e.g. usumbufu, foleni nk

  Nchi zingine custom wako very sharp na ni aibu sana kwetu
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mzee M.K, Lakini hatuhitaji mafanikio ya watu binafsi(ambao ni wachache sana) Tunahitaji maendeleo ya taifa kwa ujumla!
  Wataalamu wa uchumi wanalalamika kwamba uchumi wa tanzania haukuwi, si kweli, uchumi ungeweza kukua kwa kasi kubwa kama hawa wahujumu uchumi wangedhibitiwa!
   
 5. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tumaini, wewe ungependekeza njia gani mbadala ili serikali iweze kuokoa mapato yake?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  inabidi uende kuonesha jinsi yakufanya siyo kuandika tu mapendekezo na kuchora chora kujaza daftari. Nadharia kama za kwako hazihitajiki kwa kweli; tunahitaji utendaji. Unafikiri wanasoma haya uliyoyaandika. Unafikiri yana faida yoyote ile?
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unajua Mkuu running a country is not much diferent from running a corner shop all the way to a conglamarate company a part from complexities that arise with expansion. Ndio maana watu huenda shule kujifunza ku deal na hizo complex situation

  Lakini the most important aspects to us humans is discipline; tuwe wa rangi gani. Mfano kama watu awachukuliwi hatua kwa wizi uliosema two questions arises usimamiaji mbovu from the management and luck of punishment for their actions. China awanyongi wezi wa mamilioni kwa kupenda bali ni message usijaribu. the results inawafanya watu wa respect government revenue discipline imposed.

  Im not suggesting watu wachukue adhabu ya China but questioning people assets is not a bad thing na ukigundua mtu ni mwizi unachukua assets zake na kifungo cha kweli labda mwaka tu. tayari umeshawapa watu message kwamba kuna adhabu.

  You only need better policing then ambayo kwa mujibu wa maneno yako na uhakika ulioleta kwamba ni hela nyingi inapotea we can afford to invest on them knowing future revenue will cover the cost.

  In simple tone ni kwamba creativity inahitajika ili kuwabana watu; na amini nikisema tabia aibadiriki iwapo humans do not see punishment for their actions hivi ndio mzungu anavyoanza ku deal na matatizo ya tamaa.

  Kwani hata ukileta system mpya watu still watatafuta namna ya kuiba na si jambo zuri mara nyingi modern technologies huja na kukata watu makazini.
   
 9. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na hoja za Juma Contena na mtoa hoja. Kama alivyosema Juma adhabu kali na yenye kuogofya ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda kama inavyotakiwa katika nchini yetu na kuhakikisha kuwa Rushwa tunaikomesha. Nawaomba msome Thread ya "Namna ya Kukomesha Rushwa Tanzania" ilyotolewa leo katika Jukwaa la Siasa.
   
Loading...