Je, ni ipi njia sahihi ya kuifanya pesa yangu benki iendelee kupanda thamani?

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Feb 9, 2019
859
1,012
Iko hivi:-

Kila kukicha pesa yetu inashuka thamani 10,000 ya leo kesho itakuwa ni pesa ya kununua kikombe cha chai.

Sasa maada yangu ipo hivi!:
Ikiwa nimeweka 100,000 benki leo hii baada ya miaka 30 itakuwa ni pesa ndogo kulingana na thamani ya shilingi yetu kuendelea kushuka hivyo waweza ona Nakuja itoa na kununua shati tu. Nami sitaki iwe hivyo.

Nimefikilia niwe naweka kwa ku exchange rate na kuwa dola na kuiweka kama dola Nakuja itoa kama dola ila bado naona kuna ugumu maana napenda niwe najaza pesa kwa kutumia simu ya mkononi kwenda kwenye akaunti.

Je, ni ipi njia sahihi ya kuifanya akiba yangu iendelee kupanda thamani?

Msaada tafadhali.
 
Mkuu whaaat the F! Miaka 30? Unaweza ya baadaye badala ya kuwaza sasa hivi? Miaka 30 come on man
Nategemea ile pesa ije inifae nikizeeka huko sasa usijeona Nakuja itoa nanunua chai chapati wakati sasa hivi na uwezo wa kununua toyo moja.

Je, ni ipi njia sahihi ya kuifanya akiba yangu iendelee kupanda thamani?
 
Uwe unanunua gold unatunza. Ndyo money value inayopanda thamani kwa haraka. Hata USD value yake inashuka.
 
Nategemea ile pesa ije inifae nikizeeka huko sasa usijeona Nakuja itoa nanunua chai chapati wakati sasa hivi na uwezo wa kununua toyo moja.
Je ni ipi njia sahihi ya kuifanya akiba yangu iendelee kupanda thamani?
Ukifa na korona kesho hyo peSa atatUmia NaNii
 
Uwe unanunua gold unatunza. Ndyo money value inayopanda thamani kwa haraka. Hata USD value yake inashuka.
Hapa kidogo nimekuelewe, ila shida inakuja kama nyumba ikaungua moto. Au wevi wakaja iba vitu ndani.
Na je siwezi nikaja tapeliwa hata kwenye uuzaji,. Nipe elimu kidogo juu ya hilo.
 
Hapa kidogo nimekuelewe, ila shida inakuja kama nyumba ikaungua moto. Au wevi wakaja iba vitu ndani.
Na je siwezi nikaja tapeliwa hata kwenye uuzaji,. Nipe elimu kidogo juu ya hilo.
Gold siku hizi zinauzwa hadi bank. Ilimradi tu usinunue mitaani. Bank pia kuna deposit box. Unaweza kutunza vitu vyako vya thamani tofaut na pesa.

Ila kama ni kidogo waweza tunza kwako ila kuwa makini.
 
Nunua Bitcoin leo ina around $46,000 kasoro ila miaka minne ijayo uhakika wa kuwa $200,000 upo. Unanunua kwa kiasi kila ukipata hela, unaweza nunua 0.00054 ya BTC moja. Kwa hiyo hata uwe na laki au milioni utanunua tu. Muhimu kuzingatia ulinzi wa kimtandao kama hii mambo ya online na mitandao imekupita kushoto sijui uifanyie nini hiyo hela.
 
Gold siku hizi zinauzwa hadi bank. Ilimradi tu usinunue mitaani. Bank pia kuna deposit box. Unaweza kutunza vitu vyako vya thamani tofaut na pesa.

Ila kama ni kidogo waweza tunza kwako ila kuwa makini.
Na kwenye uuzaji hali ikoje?
 
Nunua Bitcoin leo ina around $46,000 kasoro ila miaka minne ijayo uhakika wa kuwa $200,000 upo. Unanunua kwa kiasi kila ukipata hela, unaweza nunua 0.00054 ya BTC moja. Kwa hiyo hata uwe na laki au milioni utanunua tu. Muhimu kuzingatia ulinzi wa kimtandao kama hii mambo ya online na mitandao imekupita kushoto sijui uifanyie nini hiyo hela.Hiyo
Hiyo bitcoin inauzwa wapi, na Naanzia wapi?
 
Fungua fixed deposit account,fedha yako inazaa faida ndani ya mda maalumu mliokubaliana na bank,faida inatopatikana inazidi kabisa kiwango cha fedha kushuka thamani,kwa maelezo zaidi kuhusu fixed deposit account nenda kapate maelezo zaidi kwenye benki iliyokaribu nawe.
 
Iyo kitu ipo kwenye benki zote au ni baadhi tu.
 
Back
Top Bottom