Je, ni ipi nafasi ya wasanii wa kizazi kipya kumulika uhalisia wa jamii yetu?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Habarini za muda huu wakuu.

Natumai mu wazima wa afya. Kijana wenu nimejitupa jamvini leo nikiwa nahitaji tujadili kidogo namna sanaa ya nchi yetu inavyokwenda. Kijana wenu nilijaaliwa kusoma fasihi ya Kiswahili na sanaa kwa uchache sana. Aidha, katika harakati hizo za kusoma fasihi, nilijifunza kuwa miongoni mwa dhima za tanzu za kifasihi ni kuelimisha jamii. Katika dhima hiyo ya kuelimisha Mwalimu wangu alinambia kuwa mdani yake kuna dhima ya kuonya, hukosoa na kutoa mwongozo kwa jamii kwa kuzingatia hali inayoendelea katika jamii kwa wakati huo.

Kwa msingi huo, Muziki (nyimbo) za Kitanzania (Bongo Fleva) zikiwa miongoni mwa kazi za kifasihi, nilitegemea kuona namna dhima hizo za uelimishaji, ukosoaji na uonyaji zinaakisiwa katika muziki huu. Mathalani, katika wakati huu wa Uchaguzi wa Serikari za Mitaa nilitegemea kuwapo kwa nyimbo mbalimbali zinazotoa muongozo kwa Watanzania kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi huo. Vilevile, kutokana na hali mbalimbali zinazotokea nchini nilitegemea wajitokeze wasanii kumulika uhalisia uliopo katika jamii.

Nikiwa kama miongni mwa wafuatiliaji wa muziki na sanaa kwa ujumla naona nyimbo mbalimbali zinazotoka wakati huu jamii zimejikita zaidi katika kusifia uongozi na mambo ya aina hiyo. (hapa sina haja ya kuorodhesha nyimbo hizo maana naamini mnazifahamu). Si jambo baya kusififa, ila Jambo nalijiuliza je ni kweli kwa hali iliyopo tunapaswa kuwa aina ya muziki unaosifia pekee? Je hakuna wasanii wenye mtazamo tofauti na huo? kama wapo mbona siwasikii kabisa? zaidi nasikia nyimbo mpya za wasanii wakifanya remix ya nyimbo zao pendwa kusifia.

Ni ipi nafasi ya muziki wetu katika kumulika uhalisia wa jamii yetu? Je, dhima ya kukosoa au kuonya haipo katika sanaa ya Tanzania?

Naombeni mawazo yenu wakuu.
 
Mkuu umeandika vyema sana. Nadhani wasanii wa hapa Bongo wamesahau kama muziki wao unathamani, na hili si kwa watu walio kwenye muziki tu bali hata sanaa nyingine za hapa Bongo.

Hawathamini kazi zao, wamekuwa ni watu wa kununuliwa tu na kujikomba kwa wanasiasa (Huwasia hao zaidi). Leo unamwona mtu anakuaminisha kitu flani kuhusu upande huu, ndani ya siku mbili anakana au anakuaminisha upande mwingine tena kwa kuhijiapiza kabissa.

Nadani ifike wakati waanze kuheshimu kazi zao na watambue mafanikio ya sanaa yao hayapo kwenye fedha tu (japo kuwa hli ni fanikio kubwa) bali hata kwenye heshima wanayoingea, jamii wanavyoisaidia kimawazo na vingine vingi.

Sanaa ina kazi nyingi zaidi ya wanavyothani na inabidi wakumbushwe hili.
 
Back
Top Bottom