Je Ni Huruma kwa Walemavu; Ustaarabu Uliokubuhu au Kuiga Kupita Kiasi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Ni Huruma kwa Walemavu; Ustaarabu Uliokubuhu au Kuiga Kupita Kiasi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SURUMA, May 27, 2011.

 1. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nashangazwa na tabia yetu wa Tanzania ya kuaacha kutumia misamiati sahihi kwenye kutaja ulemavu unawakabiri binadamu wenzetu. Kipofu=asiyeona; Kiziwi=asiye na uwezo wa kusikia; Bubu=asiye na uwezo wa kunena maneno..nk. Kumekuwa na hali ya kuacha kutumia misamiati hii sahihi kabisa na badala yake kutumia sentensi ndefu kuelezea hali hizi. Mfano kipofu inatajwa kuwa MTU MWENYE HALI YA KUTOONA; Kiziwi=MTU MWENYE MATATIZO YA KUSIKIA; Taahira=MTU MWENYE MTINDIO WA AKILI...nk

  Naomba msaada wenu wana JF wenzangu; tatizo ni jamii kuwa na huruma sana kwa wenzetu hawa ikaona ni heri kutoita hali zao kwa jina sahihi bali kuielezea?? Au ni ustaarabu kuwa mkubwa na hivyo kuifanya lugh yetu ya kiswahili kuwa na staha zaidi??? Pia ningeshukuru kujua kama siyo kuelemewa kwetu na kasumba ya kuiga hata yasiyo na maana toka kwa wenzetu Ulaya??? Maana wao ndio wamenza huu mfumo wa kuiacha misamiati ya hali mbali mbali za ulemavu na kutumia maelezo ya hali husika...Mfano huwezi kusikia wakisema HE IS A BLIND MAN (he is a man with sight disability) ....etc.

  Je, si kwa kutumia style hii mpya kila tuzungumziapo hali ya ulemavu kutapoteza sababu ya kuwa na misamiati katika masuala ya maungo ya maumbile ya binadamu??? Nawakilisha nikiomba msaada kwenu
   
Loading...