Je, ni Hisia au Akili; ni Mwili au Ubongo?

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Wengi tunafahamu au tunasikia kwamba wanyama wanaongozwa na hisia.
Kando na wanyama, utasikia watu wakisema, fulani hana akili au ana hisia kali.

Utaona hata hivyo, kwamba vitu hivi viwili yaani hisia na akili ni vya lazima kwa binadamu na wanyama.

Hisia ni mwili na akili ni ubongo. Tafsiri yake hapa ni hii:

Mwili ni milango mitano ya fahamu, ambapo mtu hupokea taarifa na taarifa hiyo hupelekwa kwenye ungwemgongo.

Akili ni ubongo wa mbele, ubongo wa kati na ubongo wa nyuma ambapo taarifa hupokelewa, huchakatwa na kuhifadhiwa.

Ambacho huitwa hisia au mwili ni pale taarifa haifiki kwenye ubongo wa mbele badala yake inaishia kwenye ungwemgongo na ungwemgongo unaamuru tendo linafanyika.

Katika hali ambayo taarifa haifiki kwenye ubongo wa mbele, inaishia kwenye ungwemgongo, hii huitwa hisia au mwili umetawala akili au ubongo.

Matendo au tabia, mwenendo au maamuzi katika hali hii ya kuongozwa na hisia au mwili huwa mara zote ya kuumiza.

Aidha, kujua ikiwa jambo au taarifa fulani ni matokeo ya hisia au mwili huchukua muda unaotofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine na mazingira. Huweza kuwa muda mfupi, kati na mrefu.

Ukiacha madhara ya hisia au mwili kutawala akili au ubongo, hisia au mwili ni lazima kwa mtu katika kufanya ukamilifu wake.

Watu wengi duniani wanaongozwa na hisia au mwili katika kufahamu, kuelewa, kujua na kuamua mambo. Hali hii hatahivyo, iko katika viwango tofautitofauti kutoka mtu hadi mtu.

Matendo au tabia au maamuzi ya akili au ubongo ni machache sana. Kati ya mambo 10 yanayoamriwa, mambo nane maamuzi yake yameongozwa na kutawaliwa na hisia. Hii inaanza kwenye familia, jamii na taifa.

Kupitia milango ya fahamu taarifa huchukuliwa kwenda kwenye ungwemgongo hapo taarifa hupelekwa kwenye ubongo wa mbele. Ubongo wa mbele hupeleka taarifa au jambo hilo kwenye ubongo wa kati hapa jambo hilo hujadiliwa na kisha hupelekwa kwenye ubongo wa nyuma kuhifadhiwa na badae kuwa tabia au mwenendo. Huu ndio utaratibu.

Katika utaratibu huo hapo juu tutaona matokeo mawili. Kwanza ni tabia au mwenendo au maamuzi ovu. Pili ni tabia au mwenendo au maamuzi mema. Katika haya mawili: uovu na wema, ouvu ni matokeo ya kuacha kufuata utaratibu; kuasi na wema ni matokeo ya kufuata utaratibu.
 
Mkuu ili niweze kutumia akili bila hisia nitumie njia gan
Pia ili taarifa zifike zinapotakiwa pasi na kuishia ugwemgongo Nini cha kufanya

Kwako mkuu
 
Hata sasa hivi wanasayansi wamekiri kuwa tuna milango zaidi ya mitano ya Fahamu japo wameshindwa kuidadavua. Kuna zaidi ya kusikia, kuhisi, kuona, kunusa, kutaste .... Kuna yale machale ambayo hukuepusha na hatari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom