Je, Ni hawa walioliangamiza Taifa hili la Tanzania hata kukosa mitaala bora ya Elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Ni hawa walioliangamiza Taifa hili la Tanzania hata kukosa mitaala bora ya Elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sitakuwafisadi, May 17, 2011.

 1. s

  sitakuwafisadi Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JE? MAWAZIRI HAWA NDIO WALIO UA ELIMU WAKISHIRIKIANA NA SEREKALI YA CHAMA CHA MAGAMBA (CCM)

  Mwaka 1960, Wizara ya Elimu iliundwa Oscar Kambona Solomon, Eliufoo 1962/1965, 1965/1970, Chediel Mgonja 1971/1974 Mchungaji Simon Chiwanga, Isaeli Elinawinga 1975/1977 na 1977/1978 .

  Kuhanga na Thabita Siwale 1979/1982 na1983/1985, Jackson Makweta Profesa Kighoma Malima 1986 hadi 1989. 1990, Amran Mayagila Charles Kabeho 1991/1994.

  Profesa Philemon Sarungi 1995 na 1995/1999, Profesa Juma Kapuya 2000/2005, Joseph Mungai 2005/2008, Margareth Sitta, Profesa Jumanne Maghembe na wengine wengi.

  HAWA KILA MMOJA ALIACHA UMAARUFU WAKE NA KUSAHAU JUKUMU LAO LA kuliendeleza taifa hili kielimu.

  NAOMBA KUWAKILISHA.

  Tuelimishane kwa manufaa ya vizazi vyetu historia itamhukumu kila mmoja kwa matendo yake.

  HAKUNA JAMBO LILILOSITIRIKA CHINI YA JUA hakuna siri itakayo baki kuwa siri duniani.
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  naona kuanzia hapo kwa kapuya mambo ndo yakaanza kuwa sio mambo kila kitu varangati
   
 3. s

  sitakuwafisadi Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Historia na mabadiliko ya Wizara ya Elimu tangu uhuru

  HISTORIA ya wizara ya elimu Tanzania inaweza kugawika katika vipindi vikubwa viwili ambavyo ni kabla na baada ya uhuru.

  Ukitoa tofauti ya kiuongozi na utendaji kati ya vipindi hivyo, historia ya wizara ya elimu hususan baada ya uhuru, imegubikwa na mabadiliko mbalimbali, mengi yakilenga namna ya kuboresha sekta ya elimu.

  Kwa kurejea kumbukumbu mbalimbali za kihistoria hususan tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, makala haya yanaeleza historia ya mawaziri wa elimu na baadhi ya mabadiliko makubwa na muhimu waliyoyafanya wakati wa madaraka yao.

  Mwaka 1960, Wizara ya Elimu iliundwa kama chombo kinachojitegemea kutoka idara kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa kikoloni.

  Oscar Kambona ndiye aliyepewa jukumu la kuisimamia wizara hii mpya.

  Kabla hajakabidhi kijiti kwa mwenzake, mabadiliko kadhaa yalitokea wakati wake yakiwemo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salam, kufanyika kwa tathmini ya kwanza ya mfumo wa elimu, kupigwa marufuku kwa mtihani wa darasa la tano, na kuanzishwa kwa mfumo wa usawa katika kuchagua wanafunzi wa sekondari bila kujali asili ya rangi ya mtu.

  Aliyempokea kijiti alikuwa Solomon Eliufoo aliyeiongoza wizara hiyo kutoka mwaka 1962 hadi 1965. Katika kipindi chake, Eliufoo alipiga marufuku ada kwa wanafunzi wa sekondari, kuendeleza ujenzi wa shule za msingi na sekondari na upanuzi wa mafunzo kwa walimu wa daraja A na C na elimu ya watu wazima.

  Mabadiliko mengine ni kuruhusiwa kwa Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia katika elimu ya msingi na Kiingereza sekondari, kupinga ubaguzi wa rangi katika elimu na elimu ya msingi kutangazwa kutolewa kwa miaka nane.

  Kipindi cha 1965 hadi 1970 chini ya Chediel Mgonja, kilishuhudia aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza , Julius Nyerere akitangaza rasmi falsafa mpya ya elimu iliyojulikana kwa jina la Elimu ya Kujitegemea, kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu na uundwaji wa baraza la Mitihani la Afrika Mashariki.

  Mabadiliko mengine katika kipindi hiki yalihusu kutungwa kwa sheria ya elimu ya mwaka 1969, shule za msingi kufundishwa na Watanzania pekee na kuimarishwa kwa kisomo cha watu wazima na chenye manufaa.

  Mwaka 1971 hadi 1974 majukumu ya wizara akapewa Mchungaji Simon Chiwanga ambaye uongozi wake pamoja na mambo mengine ulipiga marufuku ada kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na kuitangaza elimu ya msingi kuwa miaka saba.

  Mabadiliko mengine yalikuwa Tanzania kujitoa katika Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki, Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, kutolewa kwa tamko la elimu ya msingi kwa wote, ujenzi wa vituo vya ufundi kwa wahitimu wa elimu ya msingi na kuzuiwa kwa mtihani wa darasa la nne.

  Isaeli Elinawinga alichaguliwa kuwa waziri aliyekaa madarakani kutoka mwaka 1975 hadi 1977.

  Ndani ya kipindi hiki vyombo muhimu vya elimu vikaanzishwa ambavyo ni Taasisi ya Ukuzaji Mitaala na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

  Mwaka 1978 ulimtosha Nicholas Kuhanga kuongoza wizara hii ambayo historia inaonyesha ndicho kipindi ilipotungwa Sheria ya Elimu namba 25.

  Aliyefuatia alikuwa Thabita Siwale aliyeshikilia uongozi kutoka 1979 hadi 1982. Huyu akawa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya elimu ambapo chini ya uongozi wake wizara ilianzisha Taasisi ya Mafunzo kwa Watumishi wa Elimu (MANTEP) na kuchapisha rasmi ripoti ya Makweta.

  Miaka mitatu kutoka 1983 hadi 1985 ikamtosha Jackson Makweta kukalia kiti cha uongozi wa wizara ambapo atakumbukwa kwa kuanzisha ujenzi wa shule za umma.

  Profesa wa kwanza kuiongoza wizara hii aliteuliwa, huyu alikuwa Kighoma Malima aliyeongoza kutoka 1986 hadi 1989.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu za tovuti mambo makuu mawili yanaelezwa kutokea wakati wake ikiwemo kujitenga kwa Chuo Kikuu cha Sokoine kutoka Chuo Kiku cha Dar es Salaam na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Mbeya.

  Mwaka 1990, Amran Mayagila aliteuliwa kuongoza wizara ya hiyo kwa mwaka mmoja ulioshuhudia kuanzishwa kwa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu.

  Ikaja awamu ya Charles Kabeho iliyoanza mwaka 1991 hadi 1994, aliyefuatiwa na Profesa Philemon Sarungi mwaka 1995 ambaye hakudumu zaidi ya mwaka mmoja na kubahatika kutunga sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995.

  Kutoka mwaka 1995 hadi 1999, sekta ya elimu ikaongozwa na Profesa Juma Kapuya ambapo sasa ilijulikana kwa jina la Wizara ya Elimu Utamaduni na Michezo.

  Miongoni mwa mabadiliko makubwa katika kipindi hiki ni pamoja na kuanza kwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2000 hadi 2005, wizara hii ikabadilishwa jina, ikawa Wizara ya Elimu na Utamaduni.

  Joseph Mungai akapewa wadhifa wa kuiongoza. Mipango muhimu ya maendeleo katika sekta ya elimu ilianza ndani ya kipindi hiki ikiwemo Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES).

  2005 hadi 2008 Margareth Sitta akawa waziri huku jina la wizara likibadilika tena na kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Sitta aliendeleza zaidi utekelezaji wa mipango iliyotangulia hususan MMEM na MMES.

  Kipindi hiki pia kilishuhudia kuanza kwa shule za sekondari za kata.

  Aliyerithi mikoba ya Sitta alikuwa Profesa Jumanne Maghembe
   
Loading...