Je, ni hatua gani ya kuchukua pale kiwanja kinapovamiwa?

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,366
1,622
Naandika ujumbe huu kwa niaba ya dada mmoja anaitwa Joan, alinunua kiwanja kutoka kwa rafiki yake miaka ya nyuma na kupewa hati ya kijiji ambapo aliweka mashahidi watatu.

Aliyemuuzia kiwanja alisafiri kwenda njje ya nje ambako ameolewa na anaishi huko kwa sasa. Joan akaanza kujenga nyumba ya vyumba viwili katika kiwanja chake cha 20 x 20. Baada ya nyumba kufika dirishani kajitokeza mtu kasema kiwanja ni chake naye alinunua kwa huyo huyo aliyemuuzia.

Akamwambia kashtaki popote na ujenzi uliofanya nitakulipa, cha ajabu anaendelea na ujenzi katika nyumba ile na ana mpango wa kurasimisha ile ardhi kupitia serikali ya kijiji.

Amekuwa akitoa majibu ya dharau na kusisitiza kama Joan ana haki aende mahakamani. Hapa namUombea msaada wa kisheria ni hatua gani afuate ili kupata haki yake. Kutokana na kipato chake hawezi kumudu gharama za mwanasheria kwa sasa, lakini naamini akipata ushauri ataufanyia kazi na nitakuwa natoa mrejesho wa kinachoendelea.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Aende serikali za mitaa au ofisi ya kijiji kuthibitisha kuwa zile nyaraka za awali zilizompatia uhalali wa eneo la ardhi ni halali na yuko sahihi, pili kujua taarifa za yule aliyemuuzia kuwa huku alikuwa na ndugu au jamaa zake kona gani ili kumpa uelewa wa swala hilo maana muhisika yuko nje tayari, tatu aende mamlaka za ardhi atoe viambatanisho vyake mapema ili apate clearance ya kuona kuwa swala kwa upande wake ni batili ndipo aone tija ya kutafuta mwanasheria/wakili. Akianza mwenyewe haya atapunguza hata gharama za wakili hapo baadae kama jambo likiwa zito.
 
Wakuu nawashukuru sana. Hayo tutaanza nayo kutetea haki yake na mrejesho tutautoa jinsi mambo yanavyokwenda
 
Back
Top Bottom