Waziri wa Ujenzi Ndugu John Pombe Magufuli akihojiwa na waandishi kuhusu kutumia siasa chafu za kibaguzi kwenye kampeni mbalimbali kukibeba CCM alikwepa kujibu hoja ya dhambi yake na kumsukumia waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya waziri mkuu kuulizwa kwenye maswali ya hapo kwa papo bungeni. Miongoni mwa kauli za kibaguzi (siasa chafu) ni kwamba serikali haitapeleka maendeleo wakichagua upinzani katika maeneo husika. Huku ni kuvunja katiba na kinyume na taratibu. Magufuli akihojiwa alijibu "Sina la kujibu na kama ni suala la tuhuma hizo kamuulize Waziri mkuu kwani ndiye aliyeulizwa. Sasa unataka nini kwangu"Mwanachi april 14/2012.
Je Pinda ndo amekuwa katibu au msemaji wa Magufuli? Magufuli kushindwa kujibu hoja ni dalili za kufilisika kisiasa?
Je Pinda ndo amekuwa katibu au msemaji wa Magufuli? Magufuli kushindwa kujibu hoja ni dalili za kufilisika kisiasa?