ungonella wa ukweli
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 4,210
- 555
Wanabodi heshima kwenu. Kama mnavyojua wanabodi hapa jf,wakuu wa wilaya ni wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya ccm,na pia wakuu wa mikoa ni wajumbe wa kamati ya siasa ya ccm ya mikoa. Vilevile mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa rais katika mkoa. Pia na mkuu wa wilaya ni mwakilisha wa rais wilayani.kama mtakumbuka matamshi yaliyotolewa na viongozi wa ccm hivi karibuni kuwa wakuu wa wilaya wahakikishe viongozi wa kisiasa wanaotoa matamshi ya kumtukana ama kumkashifu rais wakamatwe.pia mtakumbuka la mkuu wa wilaya kule mwanza kuagiza kukamatwa kwa wabunge wa mwanza. Kwa mtiririko huo unadhani ni halali kulipwa mshahara na serikali ambayo inakusanya kodi kutoka kwa wananchi wote?