Je ni halali kwa walinzi wa jadi (sungusungu) kuwa watu wenye itikadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni halali kwa walinzi wa jadi (sungusungu) kuwa watu wenye itikadi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Josephine, Feb 5, 2012.

 1. Josephine

  Josephine Verified User

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika nimeshtuka sana,kuona walinzi wa jadi kuwa ni watu ambao wanajibainisha kama wana CCM.

  Wana JF,

  Wengi wetu tunapenda mabadiliko ya sera ili kuirudisha Tanganyika yetu katika mfumo ambao ilikuwa ni ndoto ya Mwl. Nyerere na waasisi wa enzi hizo.

  Lakini kwa yale niliyosikia toka kwa mwenyekiti,ni kweli Nyenzo wanazo,rasilimali watu wanayo,na hivyo wanajipanga kuendeleza ukoloni mweusi.

  napozungumzia rasilimali watu,sizungumzi wananchi kama wananchi,bali ninaongelea Jeshi la polisi,maafisa wa serikali,maafisa usalama,Jeshi la wananchi,walinzi wa jadi na wafanyabihashara wakubwa na wadogo.

  Kundi hili la watu limekuwa ni tishio,kwani linatumia nguvu,ubabe,mabavu na pesa katikakutekeleza adhima zao.Niukweli uliodhahiri kwamba kama sisi wananchi ambao tunapenda mabadiliko kwa manufaa ya kizazi chetu,ni lazima tujipange kwa hoja nzito na si kuendekeza ushabiki katika mijadala mingi.kwani mabishano na kiburi havijengi bali hubomoa na kuleta kushindwa.

  kwa maana hiyo ni vema tukubali kubadili kufikiri kwetu na kutenda kwetu kwa pamoja kama kundi linalotaka mabadiliko na si kutegemea nguvu ya vyama pekee,Wote tunatambua chama pia kinapata ushindi kupitia sisi wananchi na wakereketwa.

  Tuamke ndugu zangu kusambaza propaganda kwa ndugu zetu,marafiki na wote tunaowajua ambao leo bado fikira na mawazo yao yako kifungoni.

  Kazi hii tuifanye mimi na wewe ili mabadiliko yatokane na sisi wenyewe.
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nilish
  angazwa na hilo!.
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi wasiwasi wangu ni kuwa CCM huenda ikabadili mbinu baada ya kuona green gurds wamebeba sura ya kigaidi wakawageukia sungusungu kwenye kuadhibu watu wanaowapinga hasa vijijini.
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi sana bado yanafuata mfumo wa chama kimoja mfano huwezi kupata mafunzo ya mgambo kama hauna kadi ya chama kikongwe
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wewe nae hiyo Tanganyika iko wapi? Rais wake nani? au Slaa?

  Walinzi wa Jadi, sungu sungu waliokwenda pale wote ni CCM wa chadema hawajaingia pale. Kinachokuchukiza ni nini?
   
 6. Josephine

  Josephine Verified User

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Rafiki FF,am only thinking of the solution,am not ready for argument and abuse in any way.

  Nilichosema ni tatizo lililo wazi tunatakiwa kuongelea suluhisho la ukombozi na si Chadema.

  Mfumo wa Chama cha mapandizi hauna uhalali ndani ya siasa za leo.ndiyo maana tunahitaji kutafata chakufanya.

  Tanzania jina zuri nalipenda,lakini naitambua Tanganyika,iliyofunikwa na mkoloni mweusi.
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa Sungusungu wanatambulika kisheria?......
   
 8. Josephine

  Josephine Verified User

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sungusungu wanatambuliwa kisheria kama,Parimentary service.

  Ndiyo maana hawapaswi kuwa sehemu au ndani ya Chama flani.

  Wasiwasi wangu ni kwanamna wanavyobebwa watatumiwa vibaya sana kufanya vitisho vya hali ya juu katika ngazi za vijiji na jamii kwa ujumla.
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ni halali kwa sungusungu,wanajeshi,polisi,usalama wa taifa n.k kuwa na itikadi lakini sio halali kwa wao kufanya kazi kwa misingi ya itikadi zao ziwe za dini au siasa.kitendo cha leo kinaleta mashaka kwa sungusungu kwa sababu wanaonyesha itikadi zao waziwazi.
   
 10. Josephine

  Josephine Verified User

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ufafanuzi mzuri.

  Natamani tujadili hilo ulilolifafanua,kwani mwisho wa siku tutapata suluhu.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako nini Sungu sungu au uwepo wa Tanganyika? Tanganyika ilifutwa na Nyerere zamani sana, kama tatizo lako ni hilo.

  Na sungu sungu ilianzisha na Nyerere zamani sana kama tatizo lako ni hilo.

  Hiyo Tanganyika unayoitambuwa wewe iko wapi? ilikuwepo na kwa sasa ni historia, labda itokee tena kufutwa kwenye historia Tanzania na irudi Tanganyika, lakini kwa sasa haipo hata ukiitambuwa, iko wapi? Rais wake nani? labda Slaa, maana nasikia wengine wanamuita Rais. Sasa kama wewe hulipendi hilo, kazi ni kwako. Kwa sasa tuna Tanzania, jina alilotoa Muhindi wa Tanga, na tuna Dar Es Salaam jina alilotowa Mwaarabu. yatawachaje kuwa mazuri? ulisikia jina la kihindi likawa baya? baniani tu ndio mbaya lakini kiatu chake dawa!
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wanatambulika kama wanavyotambulika green guards, blue guards, magwanda guards.
   
 13. S

  Sam Upendo Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sungusungu wa Mwanza kuanzia sasa hawaaminiki tena. hawafai kulinda kura za uchaguzi (2015) kwa sababu wana magamba.
   
 14. Josephine

  Josephine Verified User

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekupata kwa kiwango chako,naomba tuendelee kujadili Uhalali wa sungusungu kuendelea kuwa na itikadi ya chama waziwazi,hasa leo tunapokuwa na mfumo wa vyama vingi.
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wasiwasi wako ndio maradhi yako. Sungu sungu ndio wapo, na ndio leo umeona gwaride lao, na umeona walivyopendeza, sasa kama una zaidi, si una Mbunge wako hapo unapoishi? kalalamike kule mwambie apeleke hoja Bungeni, kuwa CCM wanatumia askari wa jadi kufanya sherehe zao, na hilo mimi Josephine silipendi kabisa, ili lifutwe.

  Lakini leo ndio imetoka hiyo, na wamependeza sana na nguo zao za kijani na njano. Hongera CCM kwa besdei iliyofana.
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Sungu sungu ndio wapo, na hao waliokuja hawakulazimishwa, kama kati yao wapo wa magwanda na wakaamuwa kwenda pale, basi ni ulofa wao uliowapeleka. Sidhani kama kuna aliyelazimishwa pale, au hawa sungu sungu wanalipwa na serikali?
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Ndio kitu gani hicho?(hapo penye nyekundu iliyokolea)
   
 18. Josephine

  Josephine Verified User

  #18
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sorry typing error nili takakuandika Paramilitary service,am sorry i was busy with another issue inayoelekea na neno nililoandika lakini maana yake nisawa na mgambo.
   
 19. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2013
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 280
  Wakati tunafanya Mchakato wa Katiba Mpya madudu kama haya yanatakiwa kuondolewa mara moja.
  Tabia na mwenendo huu wa Kila Taasisi kuwa na Walinzi wake ni hatari kwa ustawi wa jamii hasa kati vyama Vya Siasa.

  Kama kweli Jeshi la Polisi lina mahitaji ya rasilimali watu linatakiwa kuajiri moja kwa moja askari hawa wa Sungu Sungu kwa masharti na kanuni zilizopo za jeshi la Polisi na sivinginevyo.
   
Loading...