residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,020
- 9,609
Habari ndugu wana JF.
Weekend iliyopita nilibahatika kuwepo huko Mkuranga - Pwani.
Nikikutana na nyumba ndogo yangu ambayo ni mwalimu huko Halmashauri ya Mkuranga.
Kitu kilichonistaajabisha mpaka kufikia uamuzi wa kuuliza hii kitu hapa jukwaani, ni baada ya jana Jumatano asubuhi (11/01/2023) kuona mjadala kuhusu mapendekezo ya uboreshaji wa CBC (Competency - Based Curriculum) katika Citizen TV, huko Kenya.
Mjadala huo ukanikumbusha jambo la ajabu nililolishuhudia kwa walimu wetu wa hapa Tanzania - huko Mkuranga.
Mwalimu ananunua "schemes of works" na vitu vingine ambavyo vimeshaandaliwa na ambavyo alitakiwa aviandae yeye na kuviwakilisha kwa viongozi wake.
Nilimuuliza huyo mwalimu kuwa hiyo ni kawaida,akanijibu kuwa ni kawaida na hata wakuu wanajua hiyo.
Naomba niulize humu maana kuna wajuvi na viongozi wa kila sekta humu Jamii Forum.
Hivi haya maandalizi ya masomo/ au hizi kazi mwalimu anazotakiwa kuzifanya yeye binafsi ni sahihi wanavyofanya hivi kuzinunua!!??
Kwa mtindo huu hawa walimu kweli ni "competency - based teachers" ambao wanaweza kuzalisha wanafunzi walio bora!!?