Je, ni halali kwa Mkuu wa shule kumtoa mwanafunzi nje ya chumba cha mtihani na kumcharaza viboko kisa kusinzia?

Kuchitimbo

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
364
279
Wadau wa elimu naomba msaada.

Ni sahihi Mkuu wa shule kumtoa mwanafunzi nje ya chumba cha mtihani na kumcharaza viboko kisa kusinzia?

Mwanangu kaja na kunisimulia.
 
Ilikuwa sahihi tangu ulipomkabidhi mwanao katika shule hiyo katika mikono salama ya wataalamu wa malezi na makuzi... Kwa nini hukumwongezea fimbo mwanao kwa kusinzia kwenye chumba cha mtihani, au hukuwai kulipa ada.?
 
Ndiyo ni sahihi
Kama ninyi ni walimu basi tuna safari ndefu,
Kwani mkuu wa shule pia anaruhusiwa kuingia kwa chumba cha mtihani?.
Maana amesema alikuwa hasimamii.

Chumba kina msimamizi,kwa Nini asimuombe msimamizi kuwaamsha watoto walio lala?.

Je alipokuwa anawatoa nje na kuwachapa huoni walikuwa wanahathirika kisaikolojia ktk kujibu mtihani?.
Mwanangu anasoma shule moja hapa monduli.

Uliyenijibu kihuni Kama ndo wewe mkuu uliyefanya huo uhuni,ukome.
Siyo freshi kabisa maana nimewafata walimu nnao Kaa nao huku Kama wawili wakasema haruhusiwi kabisa.

Na hata kukanyaga kwenye chumba cha mtihani wakasema haruhusiwi kabisa.
Acheni upuuzi.
 
Walimu wana kazi sana.
Yaani mwanao yuko chumba cha mtihani. Anasinzia,M/Mkuu anampa adhabu,unaona kama mwanao ameonewa. Litoto lako likipata 0 unarudisha lawama kwa walimu.
Sasa ndugu yangu usingizi si unakuja tu wenyewe au?!
 
Samahani naomba nitoke nje ya mada kidogo japo wote tupo kwenye elimu. Nina mdogo wangu amemaliza form four na anapenda kusomea course za afya certificate but hajasoma Physics na Chemistry ila ada C,B na D za massomo mengine ikiwemo biology. Je ni course gani anaweza kusomea za afya?
 
sawa kabisa/

Utasinziaje kwenye chumba cha mtihani?

Mtihani kweli unakoroma.

Hii ni kama dharau.
 
Sasa ndugu yangu usingizi si unakuja tu wenyewe au?!
Mtoto alisema wakisha maliza kula chakula cha mchana watu wengi unakuta wanasinzia kwenye mtihani
Lakini uzuri alisema Kulikuwa na msimamizi kila chumba kwa nini asimuombe msimamizi awe anawaamsha Hadi awatoe kwenda kuwachapa?.
Huoni mtoto atakuwa amefanya mtihani hayuko sawa?
 
Ukiona mwanafunzi analala kwenye mtihani ujue kilaza Huyo, unakuwaje na contents then Unalala ????
## je angeachwa aendelee kulala angefanya mtihani vizur????

Mtoto alisema wakisha maliza kula chakula cha mchana watu wengi unakuta wanasinzia kwenye mtihani
Lakini uzuri alisema Kulikuwa na msimamizi kila chumba kwa nini asimuombe msimamizi awe anawaamsha Hadi awatoe kwenda kuwachapa?.
Huoni mtoto atakuwa amefanya mtihani hayuko sawa?
 
Kuchitimbo,
Wewe ndo mzazi mpuuzi kupita viwango, ni mpumbavu. Hivi unajua watoto wapo wangapi shuleni? Fikiria kila mzazo aje na proposal yake juu ya malezi ya mtoto wake wataweza kweli hao walimu? Ukitaka mchukue mwanao umfundishe wewe mwenyewe, kama umemkabidhi shuleni waachie wamnyooshe
 
SIO SAHIHI.Mwalimu kama mlezi na kama mwanataalumu hayuko sahihi .Mwalimu anapaswa kuongea na mwanafunzi kwanza kuelewa tatizo lake lipo vipi na linasababishwa na nini?Katika mazingira ya sasa kusinzia au kulala darasani linachangiwa na mambo mengi.Sisi ni mashahidi watu wanalala sana kwenye magari na katika maeneo ya mikusanyiko hii inamaana lipo tatizo linalosababishwa na hali ya hewa
Acheni uzungu Afrika, wewe ungelelewa hivyo shulen ungefaulu??
 
Samahani naomba nitoke nje ya mada kidogo japo wote tupo kwenye elimu. Nina mdogo wangu amemaliza form four na anapenda kusomea course za afya certificate but hajasoma Physics na Chemistry ila ada C,B na D za massomo mengine ikiwemo biology. Je ni course gani anaweza kusomea za afya?
Kama hajasoma Physics hakuna kozi yoyote ya afya anayeweza kuisoma. Mwambie akasome vitu vingine.
 
Wadau wa elimu naomba msaada.

Ni sahihi Mkuu wa shule kumtoa mwanafunzi nje ya chumba cha mtihani na kumcharaza viboko kisa kusinzia?

Mwanangu kaja na kunisimulia.
Ni halali kabisa na ungefaa na wewe mzazi ukapate na wewe viboko 70 kwa kumwacha mtoto kwenye TV mpaka usiku mnene
 
Kuna nursing certificate,environmental health
Samahani naomba nitoke nje ya mada kidogo japo wote tupo kwenye elimu. Nina mdogo wangu amemaliza form four na anapenda kusomea course za afya certificate but hajasoma Physics na Chemistry ila ada C,B na D za massomo mengine ikiwemo biology. Je ni course gani anaweza kusomea za afya?
 
SIO SAHIHI.Mwalimu kama mlezi na kama mwanataalumu hayuko sahihi .Mwalimu anapaswa kuongea na mwanafunzi kwanza kuelewa tatizo lake lipo vipi na linasababishwa na nini?Katika mazingira ya sasa kusinzia au kulala darasani linachangiwa na mambo mengi.Sisi ni mashahidi watu wanalala sana kwenye magari na katika maeneo ya mikusanyiko hii inamaana lipo tatizo linalosababishwa na hali ya hewa
ungekuwa huku Lingusenguse ningekununulia Lunch,copral punishments ni unyama at its highest level,tafiti zote za kisayansi zimekuja na majibu utumiaji wa adhabu hii hausaidii katika kudhibiti nidhamu na badala yake inaleta na kujenga chuki kati ya mwalimu na mwanafunzi,inaleta our next generations ziwe na hasira na visasi (matokeo yake tunayaona humu ndani,walioua kwa viboko hata michango yao ni ya kihasira)get rid of this shit.
 
Hu
Ni halali kabisa na ungefaa na wewe mzazi ukapate na wewe viboko 70 kwa kumwacha mtoto kwenye TV mpaka usiku mnene

Hamjaelewa ninacho maaanisha.
Kwani kumcharaza viboko baada ya kumtoa kwa chumba cha mtihani kitamuongezea Nini kwenye mtihani huo hata Kama Ni kilaza?.

Swali Ni hili,kwa Nini mkuu wa shule asitumie wasimamizi kwa kuwaomba kuwaamsha ili waendelee na mtihani?.
Kumbuka hiyo ya kushikwa na usingizi inatokea mchana baada ya chakula hivo inasababishwa na mmeng'enyo wa chakula .

Kwenye semina walielekezwa kuingia kwa mtihani na kuwatoa nje walio lala na kuwachapa viboko?.
Huyo mkuu ana matatizo,ipo siku yake
 
ACHA KUONYESHA AKILI NDOGO.MWANAO ANAPOSINZIA AU KULALA KABLA YA KULA HUWA UNAMUADHIBU? .DAWA YA MWANAFUNZI ANAYESINZIA NI KUWAMBIA ASIMAME TU.KAMA UMEENDA SHULE KUNA MAMBO YANAITWA YA HIARI NA AMBAYO SI YA HIARI.KUSINZIA SIO JAMBO LA HIARI KAMA UNAVYOWEZA KUPIGA MIAYO,AU KWIKWI.
Sawa
 
Back
Top Bottom