Je ni halali kwa manispaa ya shinyanga kukosa maji kwa wiki nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni halali kwa manispaa ya shinyanga kukosa maji kwa wiki nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Aug 25, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Serikali ilitumia gharama kubwa sana ama kwa pesa za kodi yetu au msaada wa wafadhili kuvuta maji kutoka ziwa Victoria na kuunganisha manispaa hii pamoja na viunga vyake,lakini cha ajabu mradi huo wa maji umekuwa ukiendeshwa kisiasa kuliko kusudi halisi la matakwa ya wananchi.

  Kumekuwa na mashirika mawili yaliyo pewa dhamana ya kuendesha mradi huu,moja linazalisha maji ambalo kwa jina linaitwa KASHWASA na lingine linauza maji kwa mlaji kwa jina la SHUWASA.Kwa mantiki hiyo basi KASHWASA ina muuzia maji SHUWASA na SHUWASA ina muuzia mlaji(mwananchi).Ajabu mradi huu wa maji umekuwa si sehemu ya huduma tena bali umegeuzwa kama Biashara kiasi cha kuwatesa mwananchi wa manispaa hii.

  Maji yanafungwa kwa makusudi na KASHWASA kwa kuwa tu inaidai SHUWASA bila kujali waathirika wakuu wa sakata hili ni wananchi wasiona na hatia.Iko wapi utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana ikiwa hata maji nayo yamegeuzwa biashara.

  Kulikuwa na haja gani kwa mradi huu kuendeshwa na makampuni mawili kwa gharama inayolipwa na mlaji na kushindwa kutoa huduma iliyo bora na yenye tija bila kumuathiri mlaji.Huduma hii ya maji angalau ingepatikana kwa asilimia 45% ingeleta tija kwa mwananchi.Wakazi wa manispaa hii waliwahi kuandamana na kutoa tamko kubwa kuhusiana na matatizo makubwa ya maji yanayo wakabili.Tamko hilo lisababisha kesho yake majikufunguliwa na wananchi kupata huduma,lakini cha ajabu hali hii imekuwa ikijirudia rudia kila wakati bila kupata suluhisho la kudumu

  Iko wapi wizara ya maji, kiasi cha kukaa kimya na kushindwa kuwa patia huduma bora za maji wananchi wake.Tumeona bajeti ya wizara hii jinsi ilivyopata taabu kupitisha bajeti yake,sasa na fikiri wanataka tutumie ile nguvu ya umma kudai haki yetu ya msingi.

  Kusimama kwa maandamano ya nguvu ya umma kumesababisha serikali yetu kulala usingizi,nafikiri kuna haja wakazi wa manispaa hii kurudi barabarani mpaka kieleweke.

  Tunaongea kwa uchungu kutokana na hali inayo wakumba wakazi wa manispaa hii kutokana na uzembe wa watu wachache waliomo ndani ya idara.Haiwezekani maji leo kufikia dumu moja shilingi 1000/- ilihali wananchi wa kima cha chini wanaishi chini ya dola moja ya Kimarekani.

  Tunaitaka serikali kuliangalia suala hili na kulitafutia uvumbuzi ikiwa ni pamoja na kuunganisha mashirika haya mawili na kuwa moja,pia tuna wasiwasi na hesabu za maji tunayolipa kama kweli zinafanya kazi kusudiwa,kwa mantiki hiyo basi tunamtaka CAG kufika mkoani humu na kukagua hesabu za mapato na matumizi ikibidi watakao patikana na hatia ya kuhujumu pesa za umma sheria ichukue mkondo wake.

  Mwisho maji ni uhai na si anasa,mkishindwa kutupatia huduma tutadai kwa kutumia nguvu ya umma.
   
Loading...