Je, ni halali kwa abiria kutumia masaa 12 kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, ni halali kwa abiria kutumia masaa 12 kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzalendowetu, Jul 9, 2012.

 1. M

  Mzalendowetu Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kwa muda mrefu, kuna boti za abiria zinazotoka Zanzibar/Unguja saa 1 jioni na kufika Dar saa 12 Asubuhi. Hii ni kwa sababu kwa sheria za usafiri wa majini, boti ya abiria hairuhusiwi kufika aidha Dar es Salaam au Zanzibar si zaidi ya saa 12 jioni. Kwa vile sheria hiyo inazuia kusafiri majini usiku, kuna baadhi ya boti kama Seagul, Flying Horse etc Zimekuwa zikiondoka Zanzibar jioni na kutia nanga mara kadhaa katikati ya safari kwa masaa kadhaa. Inapofika saa 1 asubuhi, boti hizo huwasili katika bandari ya Dar es Salaam.
  Maswali ninayojiuliza:
  1. Ni kwa nini abiria hawa wamekuwa wakiteseka kwa kusafiri kwa masaa 12 badala ya masaa 2?
  2. Mamlaka husika inafahamu hatari ya kuwasafirisha abiria hawa wakiwemo watoto baharini kwa masaa 12?
  3. Kwa nini boti hizi zisingekuwa zinaondoka Zanzibar asubuhi mapema na badala yake kuondoka saa 1 jioni?
  4. Ni nini agenda ya siri ya hizi boti kufanya kama ambavyo wanafanya?
  5. Je huu si unyama dhidi ya binadamu/abiria hawa?
   
 2. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Mkuu,achana na Seagul na Flying horse,hao wapo kimizigo zaidi, wanabeba mizigo zaidi ndio maana wanakomaa usiku,next time panda Kilimanjaro III.
   
 3. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,351
  Likes Received: 2,986
  Trophy Points: 280
  Kilimanjaro ni masaa mawili tu,Mkuu zingatia ushauri wa@Mshuza2 hata nami nimewahi tumia huduma za ni nzuri sana.
   
 4. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Achana na hizo sepide panda kili3 lakini suala la kulala baharini nadhani nikwasababu kwa Tanganyika, Zanzibar 'ni nchi ya nje'.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  mnona mie nasafiri na kilimanjaro nakuja nafanya mitikasi yangu na kurudi the same day? Achana na ma flyinghorse, masaa kumi na mbili kwenye maji?
   
Loading...