Je, ni halali kuwapeleka watoto kwa Bibi/Babu wakati wa likizo?

Tonytz

Senior Member
Jul 18, 2022
159
1,142
Nawasalimu wadau wote wa JF.

Leo nimewiwa kutaka kushirikishana kwenye hili jambo. Kumekuwa na tabia ya wazazi ikifika kipindi cha likizo ya wanafunzi, huwapeleka watoto wao Kwa Babu au bibi ambao pengine huishi vijijini, au pengine watu wanaoishi vijijini,mtoto akiwa likizo au kumalizia std 7, utakuta wazazi wanafurahia mtoto kwenda kuishi mjini kwa ndugu. Hapa napata kujiuliza KUWA JE, Hali hii haiwi sababu ya watoto kubadilika kitabia hasa KUWA Hasi katika jamii?

Maana ninahisi wazazi Wana deni katika kutotimiza malezi kwa watoto wao. Lakini pia kumekuwa na desturi,hata kama wanawaruhusu kurudi likizo, utakuta likizo za misimu ya shughuli za mashambani, wazazi hao huwa hawawaruhusu watoto wao kwenda vijijini misimu hiyo. Hapa nieleweke KUWA siyo wazazi wote, ni baadhi tu ambao hawataki watoto wao wapate shida katika maisha Yao.

Mimi nadhani jamii ibadilike, wazazi wachukue jukumu la kufuatilia na kusimamia malezi ya watoto wao Ili kuepukana na mabadiliko mabaya ya kitabia kwa watoto wao.

Nini maono yako au nyongeza yako msomaji mwenzangu? Ni mawazo yangu tu.
 
Back
Top Bottom