Je ni haki Kuwataumu wenye madaladala Tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni haki Kuwataumu wenye madaladala Tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PascalFlx, Feb 26, 2009.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo katika kuangalia angalia habari za nyumbani nilikongoli tofuti ya Darhotwire.com na picha niliyokutana nayo ni basi la Daladala huku wanafunzi kibao wakijitahidi kuingia ndani ya basi hilo bila mafanikio.

  Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana kichwani mwangu ambayo majibu yake mengi tunayo. Ila kwa mtanzania wa kawaida aliyekaa nyumbani (Tanzania) muda wote bila kusafiri safiri anaweza kuwatupia kwa asilimia 90 wamiliki wa Daladala,..., hata mwandishi wa habari ile naye vile vile alikuwa anawatupia wamiliki hao kwa tatizo hilo..,

  Je wadau hilo ni sawa? Ninaweza kuwa nimepotoka ila mimi msimamo wangu ni mwingine kabisa.

  Kwanza ikumbukwe huko nyuma ni mkoa wa Dar es salaam tu ndio uliokuwa na utaratibu wa magari ya usafiri ndani ya Jiji maarufu kwa jina la UDA, ila wateja walivyazidi kuwa wengi serikali ilitoa uhuru kwa watu binafsi KUSAIDIA hapo ndio yakaanza madaladala na nauli ilikuwa ni shilingi tano (au Dala) chanzo cha magari hayo kuitwa hivyo.

  Ila kadri siku zinavyozidi kujongea serikali ilianza kujitoa taratibu na matokeo yake DalaDala ndio zinakwa tegemezi na UDA zinasaidia pale Daladala zinaposhindwa kukidhi haja.., Kwa mtazamo wangu hili sio sahihi kabisa.

  Pamoja na kwamba serikali imeamua kujitoa katika biashara na jukumu lake limebaki katika kukusanya Kodi tu, ila Huduma muhimu kama usafiri si vizuri likategemea kwa asilimia 95 usafiri binafsi.

  Katika nchi nyingi Duniani suala la usafiri ndani ya miji ni la serikali na watu binafsi wanakuwa na magari yao ambapo wananchi hupanda kwa gharama ya juu kidogo ukilinganishwa na yale ya serikali. katika magari haya binafsi yanakuwa na ubora wa juu zaidi humu hakuna cha mwanafunzi wala mzee wote hulipa nauli sawa, ila yale ya serkali kunakuwa na bonus mbali mbali kuanzia wanafunzi, na katika nchi nyingine kama Urusi, Korea, Sweden hata senior citizen (Wastahafu na wazee) wanakuwa na punguzo lao vile vile, kwani ni jukumu la serikali moja kwa moja kutoa huduma kwa mafungu hayo mawili niliyoyataja.

  Nakutolea mfano mmoja hapo hapo Tanzania mbona wazee na watoto chini ya miaka mitano katika Hospitali za serikali wanakuwa na punguzo?, ukienda hospitali binafsi hilo lipo? (haiwezekani kwani asilimia 60 ya wagonjwa wanaangukia fungu hilo hivyo Hospitali zingekuwa zinaendeshwa kwa hasara).., sasa kwanini Leo tumlazimishe mwenye Daladala anayelipa kodi serikalini kwa biashara hiyo kubeba mzigo wa serikali?..,

  Cha maana hapa ili kuondoa hili tatizo ni Serikali kujikita katika kuboresha huduma hii na kuongeza magari yake binafsi... , Hivi Daladala wakigoma hata kwa wiki moja Serikali itahakikisha vipi wafanyakazi wake wanafika kazini kwa wakati nila kuathiri utendaji kazi mzima wa Serikali.

  Kama tunataka watoto wetu wasome katika mazingira mazuri na kuondokana na tatizo hili serikali iache kabisa kutegemea watu binafsi katika suala hili...

  Mimi kwa leo nawasilisha sijui wana jamii mnasemaje?
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mukulu heshima mbele,

  Tatizo la usafiri wa wanafunzi ni multi-dimensional.

  Tatizo la usafiri wa wanafunzi ni sehemu tu ya tatizo kubwa zaidi la HUDUMA MBOVU ZA USAFIRI.

  Tatizo la huduma mbovu za usafiri ni mutlidimensional.
  Tatizo la huduma mbovu za usafiri ni sehemu tu ya tatizo kubwa zaidi la KUWAKABIDHI WANASIASA MAJUKUMU YA KITAALAMU.


  Kwa mtazamo wangu, tatizo halitaondosheka iwapo sehemu niliyoi-bold, itaendelea kuwa hivyo.
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  tatizo limeelemea mno katika kuangalia tu watoa huduma hiyo badala ya watolewa huduma!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu,

  Kwa mwanasiasa hilo halimsumbui, maana inaweza hata asilione kuwa ni tatizo.

  Idadi kubwa ya watu kwa mji mkubwa kama Dar is enough asset kwa serikali inayojali raia zake, kuamua walau kuwekeza tu-billioni kadhaa ili kuwezesha kuwa na usafiri wa uhakika na hivyo kurahisisha mendeleo.

  Hebu fuatilia assumptions zifuatazo:

  1. Kwa makadirio ya chini idadi ya wakazi wa Dar, wanaofanya safari kwa siku, hawapungui 400,000.

  2. Iwapo kwa kiwango cha chini, watalipa sh 600 kwa siku kwa huduma bora za usafiri (zilizopo kichwani mwangu) watalipa jumla ya sh. milioni 240 kwa siku.(=Makusanyo ya kama 13.2 Bilioni kwa mwezi)


  Hii tenda kwa kweli sioni ni kwa jinsi gani isiwe sustainable, kwangu ingekuwa sababu tosha ya serikali kuichukua hii tenda.
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  mtindio! hizo bilioni 13.2 per moon! usishangae akapewa LIYUMBA & COMPANY ili yeye alete 30% ya pesa hiyo kwani ndo ubia wa serikali!
  wakati huo huo waathirika ni sisi KCC!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa mzee,

  BTW, nilisikia wafanyabiashara fulani wakidai kuwa wanampango wa kuleta mabasi ya hawa wanafunzi ; Hivi hili nalo limeishia wapi wadau? Maana naona bongo kila sehemu ni sinema tu hakuna vitu 'real'.
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo ndipo panapoididimiza tz.....
   
 8. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kujibu hoja, tumekuwa wepesi sana wa kuwalaumu wamiliki wa madaladala.

  Mimi sidhani kama wamiliki wa daladala ndio wanajukumu la kugharimia usafiri wa wanafunzi.

  Kama tunaamini kwamba, kwa maslahi ya kila mtu, wanafunzi hawa wanahitaji kusaidiwa hivyo, basi wote tuwe tayari kusaidia.

  Kwa mfano tunaweza sema kwenye kila nauli kila mtu aongeze sh. 50, na wanafunzi wote waende bure. Au wenye daladala wapewe ruzuku ya kusafirisha wanafunzi, na wanafunzi wote waende bure. Kama 20% tunayolipa ya VAT haitoshi kuendesha nchi, basi tuongeze kodi kidogo.

  Sasa kuna mwingine macho yatakuwa yanamtoka hapo akiambiwa na yeye inabidi achangie, lakini kusema mwenye daladala ampeleke mtoto wake shule bure kwake ndio sawa ... Yeye akijitutumua akapata kidaladala chake, macho yanamtoka tena akiambiwa aache wanafunzi wakalie siti ... lol
   
Loading...